Afyeka nyeti zake, aagiza zipelekwe kwa wanawake 2 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Afyeka nyeti zake, aagiza zipelekwe kwa wanawake 2

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Msharika, Feb 29, 2012.

 1. M

  Msharika JF-Expert Member

  #1
  Feb 29, 2012
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 936
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  KIJANA Priva Elian (29) anayeishi Useri wilayani Rombo mkoani Kilimanjaro, amefyeka sehemu zake za siri na kuziondoa, kwa kile kilichoelezwa kuwa ni kugombaniwa na wanawake wawili.

  Wakizungumza na gazeti hili, baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo, walidai kijana huyo anayefanya biashara kati ya miji ya Rombo na Nairobi nchini Kenya, alifikia uamuzi huo baada ya wanawake wawili kumgombea.

  Walidai kuwa alifikia uamuzi huo Februari 27, mwaka huu saa 1:30 asubuhi baada ya kupandwa na ghadhabu kutokana na usumbufu mwingi aliokuwa akiupata kutoka kwa wanawake hao.

  Walieleza kuwa mara baada ya kuchukua uamuzi huo, alimwita mdogo wake ambaye hakutambulika jina na kumweleza kuwa achukue viungo hivyo na kuwapelekea wanawake hao ili wavigombee.

  “Hatujui alitumia kifaa gani kujifyeka kwani kinaonesha ni kikali sana, kwani baada ya kukata sehemu hizo nyeti, alimpa mdogo wake ili awapelekee wanawake hao kwani ndicho kitu muhimu kwao na siyo yeye,” alisema mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo la kusikitisha.

  Kutokana na kuvuja damu nyingi, majeruhi huyo alipelekwa katika Hospitali ya Wilaya ya Huruma iliyopo wilayani humo akiwa amepoteza fahamu na hawezi kuzungumza.

  Gazeti hili lilimtafuta Mganga Mkuu wa Hosptali ya Huruma anapopatiwa matibabu majeruhi huyo, lakini simu yake ilipokelewa na daktari mwingine ambaye alikiri kupokelewa kwa mgonjwa huyo.

  “Nikweli tumempokea mgonjwa huyo jana na tulimwingiza katika chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu (ICU), kutokana na hali yake kuwa mbaya sana iliyosababishwa na kuvuja damu nyingi, lakini kwa sasa amehamishwa na yupo wodini,” alisema daktari huyo ambaye hakutaka kutaja jina lake.

  Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Mkoa wa Kilimanjaro, Ramadhan Ng’anzi, alithibitisha ajali hiyo na kwamba Polisi inafanya uchunguzi ili kubaini kuwa kama wanawake hao kama ni wake wenza wa majeruhi, au mmojawapo.

   
 2. The Hunter

  The Hunter JF-Expert Member

  #2
  Feb 29, 2012
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 1,049
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Phuuu! Kweli ule mwisho umekaribia!
   
 3. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #3
  Feb 29, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,120
  Likes Received: 6,604
  Trophy Points: 280
  Akome akomae
   
 4. O

  Otorong'ong'o JF-Expert Member

  #4
  Feb 29, 2012
  Joined: Aug 17, 2011
  Messages: 31,212
  Likes Received: 10,550
  Trophy Points: 280
  akili finyu kweli yan jamaa mawazo yake alizani hao wakina dada wanamtaka kimpenzi!
  Ningemuona wa maana kama angetoa mali zake au fedha halafu awapelekee hao kinadada wagawane coz alikuwa mfanya biashara. laiti angejua hao kinadada were after his money wala asingekata hizo mambo zake.
  kakosa mambo mengi..lol
   
 5. O

  Otorong'ong'o JF-Expert Member

  #5
  Feb 29, 2012
  Joined: Aug 17, 2011
  Messages: 31,212
  Likes Received: 10,550
  Trophy Points: 280
  Hivi atakojoaje au watamtoboa kitobo hapo khaa..
   
 6. Lyamungo

  Lyamungo Member

  #6
  Feb 29, 2012
  Joined: Aug 17, 2011
  Messages: 91
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  juju bana
   
 7. S

  Shansila Senior Member

  #7
  Feb 29, 2012
  Joined: Jan 28, 2012
  Messages: 189
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kiruuuuuuuuuuuuuuuuu!kibooooooooooooooooo!
   
 8. Mtanzania haswa

  Mtanzania haswa JF-Expert Member

  #8
  Feb 29, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 665
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  sasa huo uchunguzi wa polisi kuchunguza kama ni wake wenza then what?
   
 9. bucho

  bucho JF-Expert Member

  #9
  Feb 29, 2012
  Joined: Jul 13, 2010
  Messages: 4,547
  Likes Received: 428
  Trophy Points: 180
  Wajinga ndio waliwao . Kweli amekubali kukatia chini utamu kisa ujinga ?
   
 10. Acha Uvivu

  Acha Uvivu JF-Expert Member

  #10
  Feb 29, 2012
  Joined: Apr 28, 2011
  Messages: 528
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  kitobo hakijatoka wewe sema watamuongezea pipe ili mkojo uruke mbali.
   
 11. Acha Uvivu

  Acha Uvivu JF-Expert Member

  #11
  Feb 29, 2012
  Joined: Apr 28, 2011
  Messages: 528
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Kweli kushika mkwanja haihitaji elimu. Maana jamaa alikuwa na mshiko lakini alikuwa hana elimu kuwa wanawake wa siku hizi wanataka fedha sio nonino.
   
 12. Bondpost

  Bondpost JF-Expert Member

  #12
  Feb 29, 2012
  Joined: Oct 16, 2011
  Messages: 1,981
  Likes Received: 508
  Trophy Points: 280
  Dah, jamaa bora afanyiwe upasuaji kubadili jinsia, maana sasa pachupachu ndio atakosa!
   
 13. Watu8

  Watu8 JF-Expert Member

  #13
  Feb 29, 2012
  Joined: Feb 19, 2010
  Messages: 47,347
  Likes Received: 2,683
  Trophy Points: 280
  atakua anakojoa ka demu ni mwendo wa kuchuchumaa
   
 14. Tajy

  Tajy JF-Expert Member

  #14
  Feb 29, 2012
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 298
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hujafa,hujaumbika!
   
 15. Blaki Womani

  Blaki Womani JF-Expert Member

  #15
  Feb 29, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 8,467
  Likes Received: 3,732
  Trophy Points: 280
  Imani za kishirikina maana hawa wafanyabiashara wanavituko. Pole zake apone aje kujutia upumbavu aliofanya
   
 16. mama D

  mama D JF-Expert Member

  #16
  Feb 29, 2012
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 1,755
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  hapa ndio wahenga wanasema majuto mjukuu......akipona atajuuuta
  ila hazikua akili zake nadhani
   
 17. Amyner

  Amyner JF-Expert Member

  #17
  Feb 29, 2012
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 2,404
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  Pole yake..
   
 18. mama D

  mama D JF-Expert Member

  #18
  Feb 29, 2012
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 1,755
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  hapa ndio wahenga wanasema majuto mjukuu......akipona atajuuuta
  ila hazikua akili zake nadhani
   
 19. doctorz

  doctorz JF-Expert Member

  #19
  Feb 29, 2012
  Joined: Aug 10, 2010
  Messages: 907
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Ameogopa kwa vile hana uwezo wa kuwa ridhisha na amejitafutia kisingizio kuwa hana hiyo firimbi.

  Strange things happen in this world. Nampa pole sana. Akitaka mchango wa kwenda kupasuliwa ili apatiwe jinsia nyingine msisite kumchangia. FRAUDIAN THEORY.
   
 20. Mulhat Mpunga

  Mulhat Mpunga JF-Expert Member

  #20
  Feb 29, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 25,538
  Likes Received: 12,799
  Trophy Points: 280
  huku ccp naona wabadili mitaala ya kuwafunza hawa manjagu,kila kitu uchunguzi hata visivyohitaji uchunguzi

  nonsense!
   
Loading...