Afya ya Uzazi Upangaji familia na Ulezi

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
41,266
31,053
Wanawake wengi hujiuliza “Na je, kama nina mimba?” wakati mwingine maishani. Kama unajiuliza kama una mimba una maswali mengine Chunguza Beehive’s pregnancy & parenting kupata ujumbe zaidi kuhusu upangaji familia, jinsi ya kujua kama una mimba na chaguzi ulionazo kama una mimba.Unaweza pia kujua kuhusu fungu lawamu za mimba, umuhimu wa utunzi wa mzazi wa mapema, unachofaa kufanya wakati wa kujifungua na jinsi ya kulea mtoto awe na afya nzuri.

Kumtunza mtoto wako

Caring-for-Child1.jpg
Ni jambo la busara kujitunza wewe na mwanao. Kutunza mtoto wako linaweza kuwa jambo la kukufurahisha, lakini ni kazi ngumu. Utampatia mtoto chakula/utamlisha mtoto mara ngapi na baada ua wakati mgani? Wewe hufanya nini mwanao anapolia au anapougua? Unozuia maradhia aje?

Unaweza kuwa mwepesi kushtuka/utakuwa na wasiwasi au lakini utayagundua hayo haraka. Utashtuliwa na ambayo unajua tayari. Katika sehemu hii, utapata kujua unayofaa kufanya utakapomleta mwanao nyumbani

Kumpeleka mwanao nyumbani


Mtoto aliyezaliwa anajiratibisha na ulimwengu ulio tofauti na joto na usalama wa tumbo la mamake. Watoto hawa wanastahili kupendwa,kulishwa, kuwekwa safi na wakiwa na joto inayofaa. Kuna mambo mengi mapya wazazi wanapaswa kujua.

Afya ya mwanao
Unafaa kumwita/kumpigia daktari wako kama utaona uafuatayo kwa mwanao:

 • Kukosa kula/kukataa chakula
 • Kuwa na rangi isiyostahili
 • Nguvu kidogo
 • Joto la juu ya 380c chini ya kwapa
 • Ghasia/fujo zisio za kawaida
 • Kulala zaidi ya kawaida
 • Kutapika au kuhara
 • Shida za kupumua
 

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
41,266
31,053
Kumbadilisha napi


Usimwache mwanao juu ya meza ya kumbadilishia nguo sababu anaweza kuanguka na kuumia. Weka kila kitu unachohitaji juu ya meza hii au karibu nawe. Wakati unasafiri, beba kila kitu kwa kifuko cha ‘diaper’.

Jinsi ya kumbadilisha napi

 • Mlaze mwanao mahali dhabiti na tambarare kama kwa meza kasha ufungue diaper iliyochafuliwa.
 • Inua miguu ya mwanao kwa kuishikia kwenye kufundo na utoe ‘diaper’ hio.
 • Osha mwanao vizuri kwa kutumia katani na maji moto (kwa watoto wachanga sana).
 • Hakikisha umempamgusa mwanao mbile na nyuma ili kinyesi kisitapakae kea sehemu zingine za mwili.
 • Tumia uvumbi wa wanga wa nafaka (comstarch powder) au Fulter’s Earth na usiguze uso. Usitumie uvumbi huu kwa watoto wachanga mno.
 • Pitisha diaper chini ya mtoto. Vuta sehemu ia mbele kati ya miguu na ufunge.

Vipele visabishwao na napi

Mtoto hutumia diaper kama kumi kwa siku. Kama hutomgeuzia mtoto wako ‘diaper’ atapata vipele. Hili hutokea kama mwanao atakuwa na maji maji (ulowevu) akiwa amevishwa diaper. Huu upele hukaa mwekundu na hukaa kwa siku chache. ‘Diaper rash inaweza sababishwa pia na sabuni ya vumbi ya kuosha ilizo na nguvu sana au vitu vya kufanya ngozi iwe nyororo, kwa hivyo kama kumweka mwanao safi na mkavu hakusaidii geuza bidhaa unazo muosha nazo.

Jinsi ya kushughulikia vipele vya napi
Unapongeuzia mwanao diaper mwache kwa dakika 10 ili apunge hewa
Lowesha nyuma ya mwanao kwa maji moto kisha ipanguze kwa tahadhari
Geuzia mwanao Diaper ma utumie napi kwa muda au kama unatumia napi geuza na uanze kutumia diaper kwa muda
Usitumie suruali za ndani zitakazo hifadhi ulowecu kwa diaper
Tumia cream’ kama Fissmn Paste kwa ‘rash’. Usitumie uvumbi au ‘lotion’

Kama vipele havittoweka baada ya siku tatu au mtoto anaanza kupata malengelenge, muone daktari wa watoto.
 

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
41,266
31,053
Kumnyonyesha mwanao


Kwa watoto wengi, maziwa ya mama ndicho chakula bora zaidi. Ni rahisi kwa watoto wako kulisaga kulicho ya kununua (infont fomula). Maziwa ya mama humlinda mtoto kutokana na maradhi Fulani na waru wengine hudhani pia husaidia kumfanya mwanao mwerevu. Maziwa ya mama pia huwa na viwango vistahilivyo vya mafuta, sukari, maji na protein. Kumnyonyesha mwanao pia huhifadhi wakati na pesa.

Mnyonyesha mwanao anapokuwa na njaa au baada ya masaa 2-3. Kama mtoto wako anapata kuzichafua (kukonjolea na kukumia) nappy 6-8 ni ishara ya kwamba anashiba. Unafaa kungoja hadi mwanao atakapokuea na miezi 4-6 ili kuanza kumlisha chakula kikavu. Ni jambo la busara kuuliza daktari wako aina ya chakula unachofaa kumlisha mwanao au wakati unataka kumpatia chakula kipya ambacho hujawahi kumpatia tena.

Kumpa maziwa kwa chupa


Kama unamlisha mwanao kwa chupa, hakikisha umechanganya maziwa hayo sawasawa ili mtoto apate malisho yanayofaa. Pia zungumza na daktari wako wakati utaanza kumlisha mwanao mchanganyiko (familia) ulio na ‘iro’.

Vipi, lini na nini unalisha mtoto wako ni muhimu. Kila kitu kutoka aina yamchanganyika, joto la mchanganyiko na aina ya chupa unazotumia hujalisha. Unaweza ujumbe huu kutoka kwa daktari wako au kliniki.

Hakikisha umemuliza daktari wako kuhusu utakapoanzia kumpa mtoto wako chakula kikavu. Hata kama mtoto wako ataanza kujaribu kukifikia/kushika kijiko, ni vizuri umuulize daktari kwanza.

Kumuosha mwanao


Ni vizuri kumweka mwanao safi na mkavu km. kumgeuzia ‘nappy’ mara kwa mara. Hakikisha kuosha napi vizuri baada ya kuchafuliwa. Uso, sehemu za siri na mikono ya mtoto wako zinafaa kuoshwa kwa sifongo (sponge) kila siku. Unafaa kumwosha mwili wote baada ya siki mbili au tatu. Watoto wachaga bado wana ugue wa kitovu. Unapaswa kumwosha kwa sifongo hadi wakati ugue huu utakatika kabisa. Uoshe ugue huu kwa uangalifu mwingi na utumie mvinyo (spirit) wa upasuaji uliotiwa kwa kitakia cha katani. Usivute ugue wa kitovu unapaswa kujiangusha mwenyewe.

Usije ukamwacha mwanao ndani ya karai la kuogea. Watoto wanaweza kufa maji yaliyofika inchi mbili tu. Unapomwosha, hakikisha una vifaa vyaa kumwoshea, sabuni na kadhalika ili usimwache mwanao kwa karai la kuogea bila wakumwangalia unapoenda kuvichukua.

Maji yaliyo moto sana huenda yakamchoma mwanao. Kama unakifaa cha kupasha maji moto weak kwa joto la 49oC . Pima joto la maji kwa kiko cha mkono wako. Kabla hujamweka mwanao ndani na uhakikishe maji ni vuguvugu
 

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
41,266
31,053
Kumvisha nguo • Mvishe mwanao na kunjo moja zaidi wakati yu mchanga na jiepushe na kumwacha mwanao kuliko na baridi kwa muda mrefu.
 • Watoto hupoteza joto haraka sana, hivyo hakikisha umewafunika kichwa na miguu
 • Wakati kuna joto jingi, mweke mwanao mbali na jua. Linda mwanao kna nguo za mikono-mirefu(long-sleeve), nyepesi na umweke kivulini
 • Nguo zote mpya zinafaa kufuliwa kabla ya kutumia

Kuota meno


Mtoto wako atakapofikisha miezi sita, ataanza kuota meno. Watoto wengine huanza kkuudhika kwani huumia kabla meno hayajatokea kwa ufizi. Watoto wengi humwaga mate sana na hutaka kutafunatafuna vitu. Wakati mwingine watoto hutapika au kuhara wakiota meno.

Kwa kawaida kuota meno hakufanyi mtoto kupandwa na joto. Kama mtoto wako atapata joto. Kama mtoto wako atapata joto, yaweza kuwa jambo lingine. Hakikisha umemwona daktari wa watoto.

Mawaidha wakati mtoto anaota meno

 • Wakati wa kulala, weka kitambaa safi chini ya kichwa cha mwanao ambapo ule utamwagika. Unaweza kibadilisha kitambaa hichi kitakapo loweka ute.
 • Mpatie mtoto kitu cha kutafuna ambacho hakitamdhuru. Usimpatie kitu kidogo sana kwani anaweza kukimeza. Unaweza kumpatia vidunde vya mpira visivyokuwa na majimaji ndani kwani vyaweza kupasuka. Unaweza kumpa kijiko cha mpira au kitambaa safi.
 • Usifungilie kidunde cha kutafuna kwa shingo ya mwanao. Kinaweza kushikwa na kummyonga.
 • Kuna dawa nyingi dukani za kupiunguza maumivu wakati mwanao anaota meno. Hata hivyo, mwone daktari wa watoto kabla jujampa mwanao dawa yoyote

Baada ya mwanao kuota meno hakikisha unayatunza
 

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
41,266
31,053
Maambukizi ya Kuvu – Yeast Infection

Wanawake wengi watapata maambukizi haya katika maisha yao. Maambukizi haya huwasha, ni chungu lakini ni rahisi kutibu. Walio na ugonjwa wa Sukari huambukizwa haraka kwa sababu ya sukari nyingi katika damu yao. Pia kwa wanao ugua Ukimwi. Daktari atakupa madawa ya kutibu.
Nini dalili za maambukizi ya kuvu?

 • Kuwashwa ndani na nje ya uke.
 • Golegole nzito yenye gamu kutoka kwenye uke
 • Uchungu au hali ya kuchomeka unapokojoa au kushiriki ngono
 • Ngozi iliyogeuka nyekundu sehemu ya uke
 • Golegole inayotoka katika uke yenye harufu mbaya
 • Ishara kujitokeza juma moja kabla ya kwenda hedhi.
Unatibu vipi maambukizi haya.

Kama umewahi kuambukizwa basi unaweza kununua kirimu ya anti-fungal na ujipake, ikiwa hujawahi kuambukizwa basi muone daktari akushauri.

Utazuia vipi maambukizi ya ukungu

 • Wacha kutumia dawa za kuua bakteria - antibiotics ikiwa si lazima
 • Kunywa maziwa mala - yorghurt kupiga vita bakteria
 • Usivae chupi zinazokubana sana. Vaa chupi za nyuzi za pamba na zisizikubane
 • Osha mikono na iwe imekauka kila wakati
 • Jaribu usitumie marashi, poda na sabuni za marashi kuosha sehemu nyeti
 • Osha sehemu nyeti kila mara na uhakikishe umekausha vizuri
 • Jaribu kuimarisha kiwango cha sukari katika damu yako
 • Tumia kondomu na wacha kushiriki ngono ukitumia midomo.
 

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
41,266
31,053
Maambukizi ya mfereji wa mkojo.

Hutendeka bakteria zikiingia katika kibofu cha mkojo. Unapokojoa, unahisi moto, usipotibu inaweza kuzidisha maambukizi. Hali hii huletwa na kushiriki ngono, na magonjwa ya zinaa.
Ishara za mfereji wa mikojo kuambukizwa

 • Kukojoa mara nyingi
 • Ghafla kuhisi kukojoa
 • Uchungu au moto unapokojoa
 • Uchovu, damu katika mikojo, kuumwa na mgongo sehemu ya chini, kuumwa na tumbo
Unatibu vipi?

 • Muone daktari na tumia antibiotics
 • Kunywa maji mengi
 • Meza vidonge vya kumaliza maumivu kama Tylenol na Panado
Utazuia vipi ugonjwa huu

 • Kunywa maji mengi ili kuondoa baKteria mwilini
 • Jiweke msafi sehemu zako za siri
 • Kojoa unapojihisi
 • Jipanguze kutoka mbele hadi nyuma
 • Usitumie vipodozi vya kujipulizia
 • Vaa chupi zilizotengezwa kwa pamba
 • Nenda Toilet baada ya kushiriki ngono, hakikisha mikono yako ni safi.
 

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
41,266
31,053
Magonjwa ya Zinaa

Watu wengi hawapendi kuzungumzia magonjwa ya zinaa, lakini wengi huambulia kuyapata mara moja katika maisha yao. Kunyamaza hakusaidii.
Wanawake wamo hatarini zaidi.

Kwa sababu ya vile maumbile yao yalivyo, wana nafasi kubwa kupata magonjwa ya zinaa. Magonjwa kama kaswende, kisonono, Chlamydia huwa hayaonyeshi dalili zozote kwa wanawake. Wasipotibiwa, maambukizi huleta ugumba, wasiweze kupata mimba kabisa. Magonjwa mengine kama HPV, Herpes, na Ukimwi huwa ya maisha. HPV yaweza kuleta saratani baadaye unapozeeka.

Waweza kuzuia na kutibu magonjwa ya zinaa

Jifunze jinsi ya kuongea na mpenzi wako ili kushiriki ngono kwa usalama. Tumia kondomu, jifunze kujizuia au zingatia mke mmoja. Hata kama wewe ni msagaji (lesbian), pia unahitaji kushiriki ngono kwa usalama.
 

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
41,266
31,053
Ngono za Usalama.

Ngono salama: Fanya jambo la sawa
Ngono ni sehemu muhimu kwa maisha ya mtu mzima, lakini usipojikinga waweza kupata mambo usio tarajia, au magonjwa ya zinaa ambayo ni hatari kama ukimwi. Mnaposhiriki ngono na mpenzi wako tumieni mipira ya kondomu, mnapofanya mapenzi bila kondomu, hatari ya kuambukizana magonjwa ipo.

Jinsi gani ya kushiriki ngono kwa usalama?

Unapomfahamu mpenzi wako ndio bora na salama. Ngono ya usalama ni hatua yoyote unayochukuwa kupunguza magonjwa ya zinaa. Magonjwa mengi ya zinaa husababisha ugumba/tasa, ulemavu wa watoto na maumivu. Kujikinga, kuwa muaminifu kwa mpenzi mmoja na fanya maamuzi ya busara.

Ni zipi njia bora za kuzuia maambukizi?

 • Tumia kondomu
 • Usiguse vidonda vitokanavyo na magonjwa ya zinaa
 • Msishiriki ngono ikiwa mpenzi wako ana vidonda sehemu nyeti au maambukizi yoyote.
 • Nenda kwa uchunguzi kwa daktari kila mara
 • Ukiwa umeambukizwa pata matibabu mara moja.
 

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
41,266
31,053
PMS- Shida Wakati wa Hedhi

Wanawake wengi huwa na mabadiliko ya kimwili na hisia kabla, baada na wakati wa hedhi. Haijulikani vizuri ni nini kinachosababisha PMS. Dalili huja wiki moja au mbili kabla ya hedhi. Watu wengi hutoa mzaha kuhusu PMS na hawaichukulii kwa uzito. Ukweli ni kuwa hali hii huweko. Waweza kuwa hamu kubwa ya chakula fulani, kuumwa na matiti, kuvimba mwili na mabadiliko katika hisia.
Ishara zake ni zipi?

 • Kubadilika kwa hisia
 • Kukasirika upesi
 • Kulia bila sababu
 • Kuwa na wasiwasi
 • Tamaa ya chakula
 • Maumivu tumboni au mgongoni
 • Kufura au kuumwa na matiti
 • Kuvimba mwili
Utatibu vipi PMS?

Kati ya wanawake 5 mmoja ana PMS. Mabadiliko ya hormone huleta dalili za PMS. Kuna mambo unaweza kufanya ilikukufanya uwe na raha.

 • Kula vyakula bora vya kujenga mwili
 • Pumzika, fanya mazoezi ya uvutaji pumzi ndani na nje
 • Meza dawa za kutuliza maumivu kama Panadol
 • Tumia chupa yenye moto kujikanda sehemu ya tumbo inayouma
 • Mueleze daktari wako maumivu yakizidi.
 

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
41,266
31,053
Uchunguzi Wa Matiti

Katika nchi nyingi saratani ya matiti ndio inayojulikana sana miongoni mwa wanawake.Kutambua mapema ikiwa unayo shida kutasaidia kuokowa maisha yako.

Kuna njia mbili za kuhakikisha maisha bora.

Jifanyie uchunguzi wa matiti kila mwezi.

Kila mwezi jichunguze , ili ufahamu kama kuna mabadiliko katika matiti yako.Chunguza vibonge na ishara zingine mapema.

Jifunze mengi kuhusu saratani ya matiti na jinsi ya kujichunguza mwenyewe.

Fanya Mammogram kila mwaka
Mammogram ni picha za x-ray zinazo onyesha matiti kwa undani.Daktari hutumia picha hizi kuhakikisha vibonge vya aina yoyote havimo ndani ya matiti,hii ndio njia mwafaka ya kuchunguza saratani ya matiti

Ukiwa na umri unaozidi miaka 40 unahitaji kufanya uchunguzi wa Mammogram kila mwaka.Kama jamaa yako wa karibu, mama , nyanya, au shangazi wamewahi kupatikana na saratani ya matiti,basi anza kufanyiwa uchunguzi miaka 10 mapema.

Mammograms husaidia kuvumbua asilimia 85-90% ya kesi zote za saratani ya matiti. Jichunguze na daktari wako akuchunguze kila mara.
 

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
41,266
31,053
Uchunguzi wa fupa nyongo - Pelvic Exams

Uchunguzi wa fupa nyongo (pap-smear) kila wakati ndio njia bora kuangalia afya yako. Chunguzwa magonjwa ya zinaa, mimba na saratani za mlango wa kizazi nakadhalika. Uchunguzi huu unaweza kuupata katika hospitali za mikoa na kliniki za jamii bure au kwa daktari wa kina mama (gynaecologist)

Uwe kijana au mzee, umeolewa au la, mwenye hisia nyingi za ngono au la, uwe msagaji au mwenye wapenzi wengi, uchunguzi wa afya yako utaokoa maisha yako.

Uchunguzi wa fupa nyongo unahusu nini?

 • Kuelezea kujihusu, historia yako na ya familia ya kiafya
 • Uchunguzi katika maabara kuhusu magonjwa ya zinaa
 • Kushauriwa
 • Uchunguzi wa matiti
 • Uchunguzi wa fupa nyongo.

Ukingo wa Uzazi

Ukingo wa uzazi ni nini?
Huu ni wakati wanawake hufikia kikomo cha kupata damu ya hedhi na kutoweza kuzaa. Muda huu huanza kutoka umri wa miaka 40. Hali hii yaweza kuanza polepole au kwa ghafla. Ukingo wa uzazi huathiri kila mwanamke tofauti.
Kuna aina za upasuliwaji unaoweza kuleta hali hii. Kwa mfano, katika 'hysterectomy' tumbo la uzazi likiiondolewa, itasimamisha hedhi zako . Pia ovari zote mbili zikitolewa, hali hii huja mara moja licha ya umri wako.

Dalili za ukingo wa uzazi

 • Siku za hedhi kubadilika badilika
 • Kuumwa na viungo
 • Hali ya kusahau mambo
 • Mabadiliko ya hisia za kimapenzi
 • Kutokwa jasho kwa wingi
 • Kuumwa na kichwa
 • Kukojoa kila mara
 • Kuamka mapema kuliko kawaida
 • Hali ya kukauka ukeni
 • Kubadilika kwa hisia
 • Kukosa usingizi
 • Kutokwa jasho usiku
Utapambana vipi na dalili hizi?

 • Matibabu ya hormone, kama vile; vidonge na krimu ya kuweka ukeni
 • Fanyisha viungo vyote mazoezi, fanya mazoezi ya kuinua uzito na kunyorosha misuli.
 • Kula kwa wingi matunda na mboga na vyakula visivyo na mafuta nyingi. Pia kula vyakula vilivyo tengenezwa na soya.
 • Wanawake wengi pia hufaidika na ushauri wa mtaalamu wa afya ya akili wakati huu wa maisha yao.
 
0 Reactions
Reply
Top Bottom