Afya ya rais ni muhimu zaidi kuliko pesa za escro na kujiuzuru kwa mawaziri na watendaji wa serikali

Izack Mwanahapa

JF-Expert Member
Apr 21, 2011
497
236
Rais ni kiongizi mkuu wa nchi hivyo ni wazi kwamba afya ya Rais ikiyumba nchi itatikisika. Ndio maana nchi zote duniani hjali afya na ulinzi wa maraisi wao.

Hongera sana Rais Jakaya Kikwete kwa kupona na kuwa wazi kuhusu ugonjwa wako, ni viongozi wachache sana duniani wenye uwezo wa kuwaweka wazi na kueleza kwa undani kuhusu magonjwa yao kwa umma. Kaonesha mfano na katoa elimu tosha kwa watanzania kuchukua tahadhari kuhusu ugonjwa wa Tezi dume.

Nimesikitishwa na baadhi ya watanzania walioanza kutuma ujumbe wa kashfa kwenye mitandao ya kijamii wakilalamikia hatua ya TBC1 na TBC Taifa kuanza kurusha hotuba ya ujio wa Rais iliyoelezea kwa kina kuhusu ugonjwa uliokuwa ukimsibu wakisema kuwa eti Rais anazuwia kurushwa matangazo ya Bunge ambalo linatarajiwa kufanya maamuzi kuhusu jambo kubwa la kitaifa (Escrow saga) wakisahau kuwa hatma njema ya jambo hili inategemea sana afya ya Rais ili afanye maamuzi dhidi ya wateule wake wanaolalamikiwa.

Tuwe wazalendo, tuitendee haki nchi yetu tusiendeshwe na mihemko hasi turuhusu uhalisia uchukue nafasi.

NCHI HII NI YETU WOTE TUIHESHIMU.
 
Hongera kwakuanzisha thread......
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom