AFYA YA MTAGWA: 'Tunasubiri afe tugharamie mazishi yake?' | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

AFYA YA MTAGWA: 'Tunasubiri afe tugharamie mazishi yake?'

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Jan 3, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Jan 3, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  UKIZUNGUMZIA nyota waliowahi kutesa katika medani ya soka ya Tanzania kwenye miaka ya sabini hadi mwanzoni mwa themanini basi huwezi kuacha kulitaja jina la Jellah Mtagwa nyota wa zamani klabu za Yanga, Pan African na Taifa Stars.

  Nahodha huyo wa kikosi cha Stars kilichoshiriki kwa mara ya kwanza fainali za Mataifa ya Afrika nchini Nigeria mwaka 1980 bado hali yake ni mbaya tangu alipopata ugonjwa wa kiharusi miaka minne iliyopita.

  Ukimwona alivyo Mtagwa kwa sasa na maisha anayoishi kwa hakika hauwezi kusema kuwa huyu ndiye ambaye picha zake zilitumika kwenye Stempu pamoja na kuteingenezea nchi heshima ambayo hadi sasa imeshindwa kufikia kwa zaidi ya miaka 30 sasa.

  Kutokana na ugonjwa huo wa kiharusi, Mtagwa hana tena uwezo wa kufanya kazi ya aina yoyote ya kumwezesha kupata kipato cha kukidhi mahitaji yake ya kila siku jambo linalomfanya kuwa kama omba omba kwa kutegemea msaada.

  Hivi karibuni mara baada ya mwandishi wa gazeti hili kupata taarifa kuwa mchezaji huyo mkongwe bado hali yake si nzuri alifika nyumbani kwake Magomeni Kagera na kumkuta akiwa katika hali ambayo kwa hakika inasikitisha na kutia huruma.

  Kwa taratibu na unyonge huku akitembea kwa kuvuta mguu wake wa kushoto Mtagwa alitoka chumbani kwake uso wake ulionekana wenye simanzi kubwa na ambao unahitaji msaada wowote ule ili aweze kukabiliana na tatizo hilo ikiwa ni pamoja na maisha yake ya kila siku.

  ''Kama unavyoniona sina kitu chochote wala sehemu yoyote ambayo naitegemea ili kukabiliana na hali niliyonayo zaidi ya kutegemea msaada kutoka kwa baadhi ya marafiki wa karibu ambao wamekuwa na mimi tangu nilipokumbwa na tatizo hili mwaka 2006.

  ''Rafiki zangu hao wamekuwa wakinisaidia sana kila ninapohitaji msaada wao hivyo siwezi kusema vibaya, lakini kwa hakika bado nahitaji msaada zaidi ili niweze kurudi katika hali yangu ya kaiwada,'' alisema Mtagwa kwa sauti ya unyonge ambayo ilisabisha mmoja wa watoto wake kudondosha machozi.

  Mtagwa aliendelea kusema kuwa zaidi ya kupata msaada kutoka kwa rafiki zake hao hajawahi kupata msaada wowote kutoka kwa klabu zote alizozitumikia hata Shirikisho la Soka Tanzania TFF.

  ''Sio TFF wala Yanga au Pan African ambazo zimewahi kunisaidia, lakini kubwa zaidi namshukuru Mungu kwa kile kidogo anachowajalia baadhi ya rafiki zangu nao hunikumbuka kwa kunilipia matibabu na wakati mwiningine fedha za kunisaidia chakula hapa nyumbani.

  ''Vilevile hata leo hii mambo si mazuri kiuchumi mpaka sasa bado sijatia kitu chochote kinywani kwangu, lakini nashukuru Mungu kwa kila jambo linalotokea mbele yangu na ninaamini ipo siku nitarejea katika hali yangu ya kawaida,'' alisema Mtagwa.


  Katika hatua nyingine uongozi wa Chama cha Wachezaji soka Tanzania (Sputanza) baada ya kuulizwa na Mwananchi kama kuna utaratibu wowote wa kumsaidia Mtagwa ambaye ni wanachama wake ulisema kuwa umeandaa utaratibu kwa kuwaandika barua wadau pamoja na wapenzi mbalimbali wa soka nchini wenye mapenzi mema ili waweze kumsadia mchezji huyo.

  ''Chama chetu ni kichanga na hakina fedha za kutosha kumsaidia mchezo huyo isipokuwa tuliandaa utaratibu wa kuandika barua na kuzisambaza sehemu mbalimbali kwa lengo la kuwaomba wadau na wapenzi wa soka nchini kumsaidia Mtagwa pamoja na mwanachama mwezetu na mchezaji wa zamani wa Yanga na timu ya Taifa Stars, Allan Shomary ambaye kwa sasa amepata upofu,'' alisema Katibu msaidizi wa Sputanza, Abeid Kasabalala.

  Nakala ya barua iliyoandikwa na Sputanza na kusambazwa kwa wadau mbalimbali wa soka nchini kwa lengo la kusaidia Mtagwa na Shomary ilisomeka.

  SOCCER PLAYERS UNION OF TANZANIA.
  Taarifa kwa Wadau wote wa soka Tanzania

  Bwana Jellah A Mtagwa ni mchezaji wa zamani wa Pan Afrika, Yanga na aliyekuwa Nahodha wa timu ya Taifa, Taifa Stars'' ambaye kwa sasa amepatwa na matatizo ya kiharusi (Stroke) hivyo kumfanya awe mlemavu wa mkono na mguu.

  Kwa kuthamini mchango wake wa soka katika Tanzania na kwa kutambua nafasi yako katika duru la mchezo huo, Sputanza inakuomba tumchangie mwenzetu huyu kwa hali na mali ili familia yake ipate kujikwamua na hali ngumu inayomkabili kwa kumchangia kiasi chochote ulichonacho kupitia namba yake ya M Pesa 0755 693330.

  Kwa maelezo zaidi au makabidhiano ya hundi kwa mlengwa wasiliana na Katibu wa Sputanza kwa namba 0754 270815 na 0713 455255.
   
 2. m_kishuri

  m_kishuri JF-Expert Member

  #2
  Jan 4, 2011
  Joined: Jan 27, 2010
  Messages: 1,489
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Ndio maana nakorofishana sana na wadogo zangu kuhusu suala la kuchagua mpira kama career huko nyumbani. Concept yangu ni moja; soma kwanza, halafu ndio ucheze mpira, vinginevyo unautafuta umaskini. Yanayowauta Jella Mtagwa na Allan Shomari, ni mfano wa yanayowakuta wachezaji wengi sana Tanzania.
   
 3. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #3
  Jan 4, 2011
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  dah kuna wakati nilikuwa nacheza sana mpira timu nyingi zikininyemelea lkn marehemu mzee wangu hakupenda sana mie niendelee kucheza mpira aliona mbali sana kwa mpira wetu wa bongo hii, sasa nikiwa mdogo hawa ndo watu niliokuwa naota nije kuwa km wao kimpira sasa leo maisha yao yamejaa mashaka matupu. yanga jamani, tff viingilio vyote uwanjani mnashindwa kuwasaidia wachezaji, dah allan shomari kumbe haoni tena inauma saaana, kesho utasikia tff wanakuja na blabla kibaooo. ombi langu moja plse tff siku mtakayosikia Octavian Mrope au Peter Tino international ni wagonjwa mkimbie haraka sana mkawalipie matibabu, sijajua tu beki mstaarabu samli ayoub yupo wapi na aboubakar salum sure boy mkizembea tff ntajitoa mhanga pale kwenye ofisi zenu karume nijilipue wote twende akheraaaa, sikuwa nafika saa sita uwanjani pale majimaji kuwahi kuingia ili niione mido yangu mrope na predetor tino international wakizibanjua timu pinzani bureee, hao ni heros wangu eti. tff tunzeni ma veterans plse.
   
 4. m_kishuri

  m_kishuri JF-Expert Member

  #4
  Jan 4, 2011
  Joined: Jan 27, 2010
  Messages: 1,489
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  [​IMG]

  Jella Mtagwa.

  * Kweli fainali uzeeni.
   
 5. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #5
  Jan 4, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,681
  Likes Received: 82,533
  Trophy Points: 280
  Duh! Kuna mechi moja ya ligi kuu Pan African na Yanga jamaa alicheza mkoba mmoja wa uhakika sana huku akiwa ametulia. Kama kumbukumbu zangu ni nzuri Pan ilishinda 3-2 lakini kama si uchezaji wake basi matokeo yangekuwa tofauti sana.

   
 6. m_kishuri

  m_kishuri JF-Expert Member

  #6
  Jan 4, 2011
  Joined: Jan 27, 2010
  Messages: 1,489
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  [​IMG]

  Binadamu haujafa haujaumbika.
   
 7. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #7
  Jan 4, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,681
  Likes Received: 82,533
  Trophy Points: 280
  Kama tukichagua Wachezaji 100 (katika nafasi zote) wazuri sana tangu tupate uhuru. Mtagwa ni lazima awepo kwenye list hiyo, jamaa alikuwa ana uwezo mkubwa sana kama mchezaji pamoja na kuwa alikuwa si hodari kwenye mazoezi na pia kilaji alikipenda sana sijui kama siku hizi ameacha.
   
 8. Paw

  Paw Content Manager Staff Member

  #8
  Jan 4, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 2,032
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  Mungu amsaidie
   
 9. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #9
  Jan 4, 2011
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Jamani kwani JF hatuwezi kuanzisha kamfuko ka kusaidia ishu kama hizi?? tumwombe Invisible aweke mfumo mzuri ili tuweke senti zetu humo. halafu kama kuna ishu kama za wazee wetu hawa zinaibuka tunaanza kwa kutoa mfano kuwapatia ili jamii iweze kufunguka na kuchukua jukumu.
  Nadhani hii idea itasaidia hata kama mwanaJF anaugua tunaweza kumsaidia.

  Hili la kusaidia wenye shida halina itikadi wala imani maana endapo utajibidiisha kuwajali wenye mahitaji basi you will be rewarded. Ni kumkopesha Mungu (wenye kuamini yupo) naye atakulipa bila kujali wewe upo karibu naye au la
   
 10. m

  mzambia JF-Expert Member

  #10
  Jan 4, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 885
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Lakini tff akifa utasikia kina tenga alikuwa muhimu sana huyu sasa muda huu wako wapi?

  Tenga si alicheza naye huyu?
   
 11. l

  limited JF-Expert Member

  #11
  Jan 4, 2011
  Joined: Feb 18, 2009
  Messages: 300
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  nakumbuka jella mkoba pembeni tenga chila adolf rihard e acha tu mbele peter tino. tenga pl help the guy
   
 12. Dadii

  Dadii Senior Member

  #12
  Jan 4, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 142
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35

  Yanga na Simba Mko wapi Jamani? Acheni roho mbaya msijifanye hamuoni mateso ya wachezaji wenu wa zamani!!
   
Loading...