SoC01 Afya ya Fikra - Amani ya Maisha

Stories of Change - 2021 Competition

Ntiyakama

Member
Sep 19, 2021
32
37
"Amenikosea sana | nimekasirika mno kwa sababu yake | amenikwaza kwa kweli | sikutarajia kama angalinihuzunisha namna hii | amenivunja moyo kabisa | ameniondolea amani yangu"

Katika mkoa mmoja, nilikuwa nikitafuta chumba cha kupanga (niliambatana na rafiki zangu wawili).

Tulipita nyumba kadhaa, mojawapo ni hii ambayo tulibisha hodi (kwa kutumia kengele iliyokuwepo getini), aliyekuja kufungua geti ni mtoto (wa umri kama miaka sita hivi) akatukaribisha ndani;

“Hujambo, wakubwa wapo?”

“Sijambo; ndio, yupo mama ndani”

”Mwambie kuna wageni wanashida nae” yule mtoto aliingia ndani kisha akatoka. “Mnashida gani, niambieni nikamwambie; amesema mama”

“Sawa kamwambie tunashida na vyumba vya kupanga kama vipo” mtoto aliingia ndani kisha akatoka

“Amesema vipo, njooni niwaonyeshe.”

Tulifurahi sana kwani tulihisi kufanikiwa sana kupata chumba katika sehemu nzuri kama ile iliyeoonekana kuwa na usalama na nafasi ya kutosha (kwani zilikuwepo nyumba za uani ukiacha kubwa iliyokuwepo pia).

Sawa ahsante; tulimwambia na kumfuata mtoto ambaye alituongoza kuelekea huko viliko vyumba.

“Mama ameniambia niwaonyeshe hivi hapa;” vilikuwa vyumba viwili vidogo vya nje.

Loo! Hatukuamini tulichokiona vyumba vile; kimoja kilikuwa choo na kingine bafu!

“Unauhakika hapa ndipo ulipoambiwa utuonyeshe?”

“Ndio” alijibu yule mtoto akijiami haswa!

Nilipo wageukia rafiki zangu; mmoja alikuwa amekasirika waziwazi huku mwingie akiwa mwenye mshangao bado, nikawaambia “tafadhari tuondoke haraka.”

“Ametudharau sana; yaani katuona sisi wa kuishi chooni!!! ameniudhi mno, sikutaka kuondoka bila kumuona huyu mama ni wa namna gani, nisingemvumilia kama ningelimwona, nilitamani hata kumpiga makofi yule mtoto...

... Kila mara umekuwa ukituambia tuwe tunatafakari mema katika kila jambo tunalo kutana nalo, haya niambie sasa katika hili jema lipi unaweza kutafakari kuhusu mama huyu??” (alisema na kisha kuniuliza [kwa hasira] rafiki yangu mmoja).

• Je, ungechagua nini, kukasirika, kushangaa, kuto tilia maanani? (kuona kuwa ni namna ambayo mama huyu amechagua kutualifu kuwa hapangishi katika nyumba yake)

• Ungemjibu nini rafiki yangu huyu?

• Ungalibakia na amani yako baada ya hili?

Nilicho mjibu [Rafiki yangu] kilimtia moyo wa kuendelea; baada ya muda kidogo tulipata mahara pengine tulivu, salama na nafuu. Tukaishi hapo.

Katika dunia hii yenye wingi wa changamoto, shida na makwazo ya kila namna; amani ya ndani (ya fikra) ni kitu cha muhimu zaidi sana kukitilia maanani, ni hazina ambayo kila mtu anahitaji ingawa wachache wanaweza kuipata na ni wachache zaidi wanafanya jitihada kuitafuta.

Mara zote haiwezekani kuibadilisha hali ya nje, ingawa inawezekana kabisa kubadilisha mitazamo yetu dhidi ya hali hizo, huku tukijifunza namna ya kuzuia shinikizo kutoka nje kuathiri utulivu wa fikra na amani ndani mwetu.

Halikuwa ndani ya uwezo wetu kubadili kilichotokea katika nyumba ile; tulichobakiwa nacho ilikuwa ni kuchagua, eidha kukasirika, kushangaa, au kupuuza na kusonga mbele, tukibakiwa na amani yetu.

Kila jambo linaloonekana leo katika upeo wa macho ya binadamu (maghorofa, magari, ndege, simu, kompyuta vifaa na mitambo mbalimbali) lilikuwa na msingi wake katika mawazo | fikra za binadamu zilizo fanyiwa kazi kuwa vitu tunavyo viona na kuvitumia sasa.

Hali kadharika vita, ugomvi, mafarakano, mapigano, kukosa maelewano, hasira, dharau, kiburi, kupuuza mambo ya msingi, kutukuza yasiyofaa na mengine yote yanayoweza kusababisha upotevu wa amani huwa na msingi wake katika fikra zetu (wanadamu).

Utulivu, furaha na usalama uonekanao nje na kutafsiliwa kama amani unao msingi wake ndani ya kila mmoja wetu (ndani yangu, ndani yako).

Amani ya fikra ni hali ya kubaki tulivu (salama) kiakili na kiimani, ukiwa na maarifa na ufahamu wa kutosha ili kubakia thabiti uzikaribiapo changamoto.

Katika hali ya wasiwasi, uchovu, kukasilishwa, kuumizwa, kukatishwa tamaa na kuvunjwa moyo, watu wengi huwa wakifanya jitihada kuitafuta amani ya fikra zao kutoka katika mgandamizo wa mawazo hayo yenye kuleta hisia za maumivu.

Baadhi (wengi) huamua; kuangalia TV, kusikiliza muziki, kutoka kwenda matembezi, kuzungumza na marafiki, kulala, kufanya mazoezi au kutoka kwa chakula: mambo ambayo kwa sehemu hufanyika msaada, ingawa huleta amani idumuyo kwa kitambo tu (wakati ufanyapo kitendo hicho), hasa pale sababu (kitu) inavyo jeruhi fikra zako itaendelea kuwepo kwenye maisha yako kwa muda mrefu zaidi.

Shughuri hizo hazibadilishi msingi wa fikra zinazokuondolea amani, bali huhamisha fikra zako kwa muda kuzielekeza katika kile ulichoamua kikifanya, ingawa uwezekano ni mkubwa kuwa fikra zako zinaweza kuulejea msingi wa kukosekana utulivu na amani ambao tayari upo akilini mwako.

Mawazo (mtazamo) hasi ni msingi wa kukosekana amani ya fikra; unapo ruhusu mtazamo hasi ukutawale, unaweka agano la kuwa muhanga wa kuikosa amani ndani yako.

Kila mara litokeapo jambo ambalo hukulitarajia, utahisi ni wewe tu aliyelengwa kuegemewa, kukandamizwa, kuumizwa, kuzarauriwa na kuwekewa vikwazo ili usipige hatua.

Mtazamo chanya ni msingi wa amani ya fikra zako; tazama jambo lolote linalokupata katika mtazamo unaoleta faida kwako; kujifunza, kupata uzoefu mpya, kuwa makini wakati mwingine, kufahamu yupi wa kushirikiana nae, kufahamu aina ya watu wa kuwaomba ushauri n.k.

Jioni siku ya Jumapili, saa kumi na moja hivi, kulikwa na manyunyu ya mvua kidogo yakiambatana na ukungu. Nilipaswa kwenda kumpokea mdogo wangu ambaye alikuja nilipokuwa nikiishi.

Nilitakiwa kutumia kama Tsh. 20,000/= kumfuata aliposhukia basi na kumpeleka nilipo kuwa nikiishi (kama ningalitumia gari au bajaji)
Niliamua kuchukua pikipiki ambayo nilitakiwa kuweka mafuta ya Tsh. 5,000/= tu, ili kukwepa gharama!

Nikiwa njiani kwa sababu ya mvua na ukungu, uoni ulikuwa hafifu, dereva wa gari lililokuwa mbele yangu hatua kama nne hivi alifunga breki kwa ghafra sana (akasimama; sikufahamu kwanini!).

Ilikuwa karibu mno sikufanikiwa kusimama kabla ya kulifikia gari lile; nilijigonga kwa nyuma, nikaanguka chini (ajali); pikipiki iliharibika sana (ilinigharimu zaidi ya Tsh. 20,000/= kutengeneza pikipiki), simu (ya Tsh. 175,000/=) niliyokuwa nayo mfukoni ilivunjika na haikuweza kufanya kazi tena, nikapoteza taarifa za wadeni wangu ambazo nilikuwa nimeziandika kwenye note book ya simu hiyo.

Ahsante Mungu, nilipata michubuko kidogo tu.

Badala ya kubakia nikilalamika kwa yote niliyopoteza, nikiumia kwa maumivu niliyo yapata, nikimlaumu dereva aliye nisababishia ajari, niliamua kutafakari nini napaswa kujifunza kutoka katika tukio hili. niliandika haya;

1. Kabla ya kuangalia nitapoteza nini, napaswa kujihakikishia usalama wa maisha yangu kwanza.

2. Sipaswi kukwepa gharama ambazo zinaonekana kuwa za lazima (reasonable).

3. Sipaswi kutunza taarifa muhimu kwenye simu au kupyuta, nitatunza kwenye email au kuandika nakala ngumu (hard copy).

Sikuchagua kubaki katika kukosa amani kwa kufikiria kwanini ni mimi niliyepata ajari, niliyeharibikiwa simu yangu, niliyepoteza taarifa muhimu, niliyeingia gharama zaidi ya ilivyonipasa.

Ukikataliwa leo, kazini, sehemu unapofanyia biashara, kwenye kikundi au kwenye mahusiano, usiipoteze amani yako kwa kufikiria kuwa wewe ni duni, usiyeweza chochote, usiye faa kila mahali wala usiyependwa na yeyote.

Ijaze amani ndani yako kwa kufikiria mazuri Mungu aliyokujalia, tafakari ya kuwa umekataliwa si kwasababu hufai bali hapakufai sehemu hiyo, hakufai huyo mwenza aliyekukataa.

Ipo sehemu yako ikufaayo zaidi, yupo mwenza unaye endana nae zaidi ambaye umekataliwa huku ili ufike kwakwe.

"Ukifungwa mlango mmoja mbele yako, endelea kutembea pembezoni mwa ukuta. Kuna milango mingine mingi utaikuta wazi kwaajiri yako"

Think positive, be positive, and serve your inner peace.
 
Back
Top Bottom