Afya ya Dr. Idrisa Rashid Aliye kuwa Gavana ni ??

bado tunafikira za kale,kufichaficha mambo hata ya kijinga,et kila kitu ni haki ya mtu.tukisema kweli siku zote tutapiga hatua hata kama ukweli huo unauma kwa kiasi gani,watanzania tumekuwa waongo hata pale pasipo sitahili bila kuwa na sababu za msingi.
Siku zote ukitaka kummaliza nguvu adui yako mwambie ukweli hatakosa la kusema.sijaona viongozi wa kweli mpaka sasa huyo idrisa hanatofauti na balali,mkapa,chenge,jk,el,mudhihiri,kingunge,na wengine wanaofanana kwa sura

Kuna jamaa alitangaza kwenye msiba wa ndugu yake kwamba kafa kwa AIDS, ndugu walimtenga. Bahati nzuri jamaa hakukata tamaa na sasa
kapunguza athari za AIDS kwa ndugu zake through kuongea wazi wazi na kupeana ushauri.

Ujinga wetu ndio unatumaliza, matokeo yake, mtu anajua kabisa yule bwana au yule dada bwanake/mke wake kafa kwa AIDS lakini wao wamo tu kujimwaga nao. Labda tuanze kusema bila kuona aibu kama mtu kafa kwa AIDS ili kuokoa wanaobaki.
 
Hata Mzee Nelson Mandela alitangaza waziwazi msibani kuwa mwanae Makgatho alikufa kwa UKIMWI, lakini haya masuala yako katika utawala wa familia husika, wao ndio wenye uhuru huo na hiari hiyo. Hatuna haki sisi wengine kuwaingilia kwenye mambo yao ya ndani ya familia yao.
 
Kuna watu wana unayanyapa humu nini ?

Mimi nachofahamu Idrisa atakuwa na maadui wengi tu kutokana na msimamo wake,Baadhi ya maadui wake ni
1. Viongozi wa chama cha wafanyakazia Tuico -Tanesco kwa kuwa amewakatia mirija aya Ulaji wao
2.viongozi wa Tanesco waliokuwa wamezoea kula kufyonza Tanesco bila huruma

3.Wanaboard na watu wao wa karibu

4. Wananchi amboa wanadhani kubada kwa bei ya umeme kunasababisha na Dr Idrisa wala sio makosa ya Serikali ya kulibebesha mzigo shirika hilo mzigo wa malipo kwa ajili ya Capacity Charge kwa wazalisha umeme wa dharura .

Hao maadui wanaweza kusema chochote hapa

Kwa hiyo Dr. Idrissa Rashidi anafanya kazi na nani kwa faida ya nani, ikiwa hao hapo juu ambao ndiyo wadau wakuu na kiini cha Tanesco ni maadui zake?
 
mbona mnakazania kutajana ngoma .. mbona wenye kisukari hamuwataji...kisukari pia hakitibiki..ila unaishi kwa matumaini....!!
 
halafu mie sipendi kuzungumzia mamabo ya magonjwa

Fitna kama imekaa sehemu iache ya nini kuanza kuitokonyoa wakati imetulia?
 
Back
Top Bottom