Afya ya akili ya Robert Mugabe iko sawa ?

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,362
217,394
Sasa ni dhahiri akili ya Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe anayekaribia miaka 100 tangu kuzaliwa kwake imepungua , nadhani ni kutokana na umri mkubwa na maradhi ya uzee yanayomuandama.

Kitendo chake cha kusikiliza ushauri wa mke wake na kumtimua kazi Makamu wake wa Urais Mnangagwa si tu kinadhalilisha Zimbabwe na Africa nzima , bali kinawadhalilisha watu wote weusi popote walipo duniani .

Haiwezekani nchi yenye watu wasomi kama Zimbabwe kukubali kuendelea kuongozwa na mtu mwenye dalili za ugonjwa wa akili kama Mugabe , huyu mzee anatakiwa kung'olewa madarakani kwa njia ya amani ili kuepusha aibu zaidi kwa waafrika .
............................................................

Updates - Aliyekuwa Makamu wa Rais wa Zimbabwe amekimbia nchi hiyo kwa kuhofia usalama wake .
.....................................................

UPDATES - Hatimaye Robert Mugabe ametimuliwa kwa aibu baada ya kuvuliwa uenyekiti wa ZANU - PF .

Hili lichukuliwe kama onyo kwa madikteta wote wa nchi za maziwa makuu .
...............................................

UPDATES - Hatimaye MBUYU Mugabe umeng'oka rasmi kwenye urais wa Zimbabwe baada ya kuwasilisha barua ya kujiuzulu kwa spika wa bunge
 
Back
Top Bottom