Story of Change Afya: Unataka uanze kufanya mazoezi? Fuata hatua hizi...

Feb 17, 2018
24
45
Ni matumaini yangu kuwa wote ni wazima wa afya. Leo napenda kuzungumzia juu ya afya, na katika afya nitajikita kwenye eneo la kufanya mazoezi ya mwili. Nimechagua eneo hili, kwani kuna vitu vingi binadamu anatakiwa kuvifanya karibia kila siku au mara moja moja ili kuimarisha afya yake. Kwa kutaja baadhi ya vitu hivyo; kula vyakula vizuri vinavyoboresha afya, kuwa na fikra chanya, kuwa kwenye mahusiano mazuri na jamii inayomzunguka n.k. Vitu vingi vinachangia mtu kuwa mwenye afya nzuri.

Watu wengi wanatamani kuanza kufanya mazoezi kwa sababu tofauti tofauti. Wengine wanafanya mazoezi kwa sababu ya kupunguza uzito uliopitiliza, wengine wanafanya mazoezi ili kujitibu ugonjwa fulani, wengine wanafanya mazoezi ili kuongeza mvuto na muonekano wao, wengine wanafanya mazoezi kwa lengo la kujisikia vizuri kadri wanavyoziendea siku zao, wengine wanafanya kwa sababu ameambiwa na daktari afanye mazoezi n.k. Kila mmoja anafanya mazoezi kwa sababu zake. Hata hivyo katika jamii yetu, watu wanaofanya mazoezi angalau mara 3 kwa wiki ni wachache sana licha ya kujua faida za kufanya mazoezi. Inashangaza kuona sehemu yenye watu zaidi ya laki moja ila ni watu 1000 ndiyo wafanya mazoezi.

Wengi wanatamani kuanza kufanya mazoezi ila hawajui waanzie wapi. Na ni kweli kuanza kufanya mazoezi kama hujazoea kufanya ni ngumu sana kama hujajiandaa vizuri kiakili na kimwili. Kujiandaa vizuri kimwili na kiakili kuna kuja kwa mtu kujua faida za kufanya mazoezi, bila kujua faida za mazoezi mtu hatachukua hatua ya kufanya mazoezi. Sasa leo nimeamua nitoe elimu juu ya hatua anazoweza kuchukua mtu anayetaka kuanza kufanya mazoezi. Kwa kujua hatua hizi mtu ataweza fanya mazoezi.

 • Jua faida za kufanya mazoezi. Angalia utanufaika vipi kama utaanza kufanya mazoezi leo hii. Au kama ungelianza kufanya mazoezi siku, wiki, miezi iliyopita leo hii afya yako ingekuwaje? Orodhesha faida utakazopata kama utaanza kufanya mazoezi.
 • Amua kuanza kufanya mazoezi. Amu kiakili na kimwili kuanza kufanya mazoezi ili kuboresha afya yako.
 • Ukisha amua kiakili na kimwili, andaa vifaa vya kufanyia mazoezi. Hapa unaandaa mavazi kwa ajili ya kufanyia mazoezi, eneo gani utakuwa unafanyia mazoezi yako, mazoezi gani utaanza kufanya, wakati gani utakuwa unafanya mazoezi na utatumia muda gani kufanya mazoezi yako.
 • Anza kufanya mazoezi yako. Umeamua kiakili na kimwili kuanza kufanya mazoezi, sasa ni wakati wa kuanza kufanya mazoezi kwa vitendo. Kama ni asubuhi, basi amka vaa mavazi yako ya kufanyia mazoezi na nenda kafanye mazoezi. Fanya mazoezi yako kwa muda uliopanga na maliza kufanya mazoezi yako. Kama umepanga kufanya mazoezi yako wakati wa jioni, basi muda ukifika nenda uwanjani kafanye mazoezi yako.
 • Fanya mazoezi kadri ulivyopanga ratiba yako. Kama umepanga kufanya kila siku, basi kila siku fanya hivyo bila kukosa, na kama umepanga kufanya mara tano kwa wiki basi fanya hivyo bila kukosa. Ingawa kwa mtazamo wangu, ningekushauri ufanye kila siku, kama wewe ndiyo kwanza unaanza safari ya kufanya mazoezi. Kwa kufanya kila siku utajijengea tabia ya kufanya mazoezi mapema sana. Mtu anaye anza kufanya mazoezi, halafu akawa anafanya mazoezi kila siku itakuwa rahisi kujijengea tabia hiyo mapema, kuliko mtu anayeanza kufanya mazoezi, halafu ananfanya mara moja moja kwa wiki.
 • Tegemea maumivu na kujisikia vibaya unapoanza kufanya mazoezi. Wengine huhisi kuzunguzungu, wengine huhisi kichefuchefu na kutapika, na wengine huhisi maumivu makali kifuani. Hii ni hali ya kawaida kabisa kutokea kwa mtu ambaye hajazoea kufanya mazoezi. Lakini kama mtu ataendelea kufanya mazoezi hayo kila siku, atagundua kuwa hali hiyo itazidi kupungua kadri siku zinavyoenda na hatimaye maumivu hayo huisha kabisa na mtu kurejea kwenye hali yake ya kawaida. Tambua kuwa akili yako na mwili wako haujazoea kufanya mazoezi, hivyo inakubidi uzoeshe mwili wako kufanya mazoezi. Miezi au miaka mingi hujafanya mazoezi, hivyo usitarajie mwili wako kuwa kawaida wakati bado haujazoea kufanya mazoezi.
 • Usikate tamaa. Wengi wakihisi maumivu na kujisikia vibay huishia kukata tamaa. Hudhani hali hiyo huendelea, kumbe huwa ni hali ya muda mfupi na kama mtu hataishia njiani basi maumivu na kujisikia vibaya hukata ndani ya wiki kwanza.
Hizi ni baadhi ya hatua ambazo mtu anayetamani kuanza kufanya mazoezi ya mwili anaweza kufuata. Nimekuwa nikifanya mazoezi kwa zaidi ya miaka nane sasa, na nimewafundisha na watu wengine waliokuwa wanatamani kufanya mazoezi na matokeo yamekuwa ni mazuri sana. Na wewe pia unaweza kufuata hatua hizi.

Watu wengi hawajui kuwa watu wengi wenye miili mizuri na mwonekano wa kuvutia ni watu wanaofanya mazoezi. Wasanii, na Viongozi na watu wengi wenye ushawishi, wanaoonekana kuvutia ni watu ambao mazoezi hawaruki katika ratiba zao za kila siku. Siyo mazoezi pekee na sababu nyingine pia zinachangia.
 
Upvote 8

Abrianna

JF-Expert Member
Mar 30, 2021
4,575
2,000

Ngoja nianze kufuata hizi hatua
 
Nipo huru

JF-Expert Member
Jul 20, 2021
854
1,000
Mbona hujazungumzia umuhimu wa kumuona daktari kupata ushauri wa kitaalamu na aina ya mazoezi yanayokufaa kulingana na afya yako.
 
Feb 17, 2018
24
45
Mbona hujazungumzia umuhimu wa kumuona daktari kupata ushauri wa kitaalamu na aina ya mazoezi yanayokufaa kulingana na afya yako.
[/QUOTE
Mkuu mtu anafanya mazoezi kulingana na hali ya afya yake kwa wakati huo. Lakini pia mazoezi yapo ya aina nyingi magumu na mepesi. Kwa mtu anayeanza kufanya mazoezi, nategemea ataanza na mazoezi mepesi ambayo yatamfanya azoee kufanya mazoezi. Na akishamaliza mazoezi mepesi anaweza kuanza kufanya mazoezi magumu kulingana na hali ya afya yake wakati huo.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom