Afya Tanzania: Njoo tuwaze pamoja na tuzungumze kirafiki

Masalu Jacob

JF-Expert Member
Jul 26, 2017
948
1,093
Habari Tanzania !

Poleni kwa uchovu wa mwili na akili. Leo napenda tufanye mazungumzo kidogo kuhusu taifa letu upande wa afya kwa jamii yetu kwa ujumla.

1. Je, haiwezi kufaa tukaanzisha bima ya pamoja ya kijiji/ mtaa mmoja mmoja na tukaachana na bima za muundo uliopo ili hiyo bima kijiji au bima mtaa iweze kuhudumia mwana au wanajamii wa kutoka eneo husika anapougua?

2. Je, hatuwezi kuamua na tukamaanisha kuwa watoto wa miaka chini ya 7 na wazee kuanzia miaka 45 wakatibiwa bure tofauti na sera ya sasa ?

3. Je, hatuwezi tukachochea kwa kujenga hospitali kwa kila taasisi tukaondokana na changamoto tulizonazo kifedha na kiutendaji kwa mfumo uliopo?

4. Je, hatuwezi kuanzisha dawa na vifaa tiba vyetu vya mazingira yetu kwa watu wetu na viwe maalumu kwa ajili ya nchi na raia pekee kimatumizi?

5. Je, hatuwezi kubadilisha mfumo wetu wa elimu na mafunzo kuhusu afya na upatikanaji wa wataalamu tukaachana na mfumo wa king'ambo uliopo sasa?

Angalizo

Afya sio biashara na sio ufahali kuona mwananchi au wananchi wenzako kuumia au kukosa huduma sababu mfumo wa afya sio rafiki au ukosefu wa fedha kubaki kuwa kikwazo.

Karibu.
 
Back
Top Bottom