Afya, taaluma iliyoshindwa

samsun

JF-Expert Member
Feb 9, 2014
7,386
5,953
Wakuu najua mko poa.

Kati ya taaluma nyingi duniani nadhani hii taaluma ni muhimu kuliko hizo nyingine zote hapa duniani kama si ulimwenguni kwa ujumla. Lakini acha niseme ukweli kabisa kuwa HII TAALUMA IMESHINDWA KUTATUA MATATIZO MENGI YA MWANADAMU.
Haya hapa ni baadhi ya magonjwa kutatuliwa na hii taaluma japo ni ya siku nyingi.

1.Ukimwi (Aids) tangu mwaka 1981.
2.Sukari. ni miaka mingi.
3.Kansa karibia aina zote.
4.BP upo miaka kibao
5.Wafupi warefuke na warefu wapungue,hii toka kuumbwa kwa dunia.
6.Dawa ya kutokupata magonjwa.

Mengine ongezeeni,lakini kiujumla HII TAAALUMA NI KATI YA TAALUMA ZILIZOSHINDWA KUTATUA CHANGAMOTO NYINGI ZA MWANADAMU.

Wewe una maoni gani ???

natanguliza shukrani kwenu.
 
umetumia mizania ipi? hebu taja mafanikio yake ambayo ni maelfu kwa maelfu.. halafu linganisha na hayo 6 uliyoyataja
nadhan utapata jibu.
kuna orodha ya magonjwa zaidi ya mia ambayo yalikuwepo kabla hujazaliwa na yamekuwa eradicated kabisa kwenye uso wa dunia kwa kutumia hiyo hiyo taaluma unayoiponda
 
tatizo sio kutibu sema mfumo wa maisha hasa ulaji mbovu!!!! ukiweza hapo magonjwa mengi utayaepuka !!! sio kibugia sumu mazoezi hufanyi ukipatwa na kansa au BP utegemee kupona kabisa
 
Mada yako inavutia ...ingawa umeipima afya kwenye magonjwa machache na pia hujaangalia mazingira mengine yaliyopelekea kushindikana kwa magonjwa hayo.

kwa mrengo wa hoja yako ni kwamba walioshindwa ni watafiti au wagunduzi wa dawa ambao hawa ni tawi dogo tu unapoongelea afya.

Kwa mantiki yako ninaweza kuanzisha hoja ya kwamba taaluma ya uchumi ndio taaluma iliyoshindwa haswa kutatua tatizo la umasikini.
 
Mimi ninavyojua kuna kanuni ya kutibu, kukinga na kupunguza. lakini ukiangalia sana wataalamu wetu wa tiba wamefanikisha zaidi kutibu ila kuzuia/kukinga hawajafanikiwa.
 
Mada yako inavutia ...ingawa umeipima afya kwenye magonjwa machache na pia hujaangalia mazingira mengine yaliyopelekea kushindikana kwa magonjwa hayo.

kwa mrengo wa hoja yako ni kwamba walioshindwa ni watafiti au wagunduzi wa dawa ambao hawa ni tawi dogo tu unapoongelea afya.

Kwa mantiki yako ninaweza kuanzisha hoja ya kwamba taaluma ya uchumi ndio taaluma iliyoshindwa haswa kutatua tatizo la umasikini.
Wewe umenielewa vizuri,japo siwezi kupingana na wewe ni taaluma ipi iko vizuri. Angalia wanaanga walivyosonga,angalia mawasiliano,vyombo vya moto,wajenzi,na wengine wengi tu wamefanikisha kwa upande wao changamoto iliyomsumbua mwanadamu. Lakini hii ya tiba hadi leo hii wameshindwa kutuletea dawa ya kukuzuia na magonjwa imebaki kuambiwa isifanye hiki usile kile na ukiangalia karibia kila kitu unaambiwa ni sumu.
 
umetumia mizania ipi? hebu taja mafanikio yake ambayo ni maelfu kwa maelfu.. halafu linganisha na hayo 6 uliyoyataja
nadhan utapata jibu.
kuna orodha ya magonjwa zaidi ya mia ambayo yalikuwepo kabla hujazaliwa na yamekuwa eradicated kabisa kwenye uso wa dunia kwa kutumia hiyo hiyo taaluma unayoiponda
Nimetumia kigezo cha ulinganisho na taaaluma nyingine,kama watu wa anga,mawasiliano,vyombo vya moto na taaluma nyingine nyingi zilizofanikiwa.
 
Wewe umenielewa vizuri,japo siwezi kupingana na wewe ni taaluma ipi iko vizuri. Angalia wanaanga walivyosonga,angalia mawasiliano,vyombo vya moto,wajenzi,na wengine wengi tu wamefanikisha kwa upande wao changamoto iliyomsumbua mwanadamu. Lakini hii ya tiba hadi leo hii wameshindwa kutuletea dawa ya kukuzuia na magonjwa imebaki kuambiwa isifanye hiki usile kile na ukiangalia karibia kila kitu unaambiwa ni sumu.
hayo unayoambiwa usifanye ni sahihi na ndio maendeleo yenyewe kwenye taaluma ya afya...
Unaisifia taaluma ya anga ambayo imeshindwa kuzuia kuanguka kwa ndege...au taaluma ya ujenzi inayoshindwa kuzuia majengo kuanguka.

Jaribu kuipiga picha taaluma ya tiba toka kipindi cha mitishamba hadi leo matibabu yanatumia laser...hayo ni maendeleo makubwa ...jaribu kuingalia taaluma hii yaafya kwa jicho la kimarekani na sio Tanzania.
 
Nashukuru we ni mwepesi kuelewa na mimi nimekuelewa, na hasa hapo uliposema nitazame kwa jicho la Marekani,lakini tatizo kubwa limebaki kwenye magonjwa sugu yaliyo ya miaka mingi sana, wakati ktk hali halisi wangepata dawa inayoweza kumfanya asiugue au asipate magonjwa fulani ambayo ni sugu ingepunguza sana kutafuta dawa ya hivi vigonjwa vilivyopo.
 
Wakuu najua mko poa.

Kati ya taaluma nyingi duniani nadhani hii taaluma ni muhimu kuliko hizo nyingine zote hapa duniani kama si ulimwenguni kwa ujumla. Lakini acha niseme ukweli kabisa kuwa HII TAALUMA IMESHINDWA KUTATUA MATATIZO MENGI YA MWANADAMU.
Haya hapa ni baadhi ya magonjwa kutatuliwa na hii taaluma japo ni ya siku nyingi.

1.Ukimwi (Aids) tangu mwaka 1981.
2.Sukari. ni miaka mingi.
3.Kansa karibia aina zote.
4.BP upo miaka kibao
5.Wafupi warefuke na warefu wapungue,hii toka kuumbwa kwa dunia.
6.Dawa ya kutokupata magonjwa.

Mengine ongezeeni,lakini kiujumla HII TAAALUMA NI KATI YA TAALUMA ZILIZOSHINDWA KUTATUA CHANGAMOTO NYINGI ZA MWANADAMU.

Wewe una maoni gani ???

natanguliza shukrani kwenu.
Mafua Yaliua Watu Yamepatiwa Dawa Naona Hujaongelea Hilo

Ukoma Uliua Watu

Tetanus Iliua Watu

Kifua Kikuu

Naona Hayo Yote Hujaona...kila Kitu kina Muda Wake Kitapata Dawa Kulingana Na Mapenzi yake Mungu mwenyewe
 
Nashukuru we ni mwepesi kuelewa na mimi nimekuelewa, na hasa hapo uliposema nitazame kwa jicho la Marekani,lakini tatizo kubwa limebaki kwenye magonjwa sugu yaliyo ya miaka mingi sana, wakati ktk hali halisi wangepata dawa inayoweza kumfanya asiugue au asipate magonjwa fulani ambayo ni sugu ingepunguza sana kutafuta dawa ya hivi vigonjwa vilivyopo.
Una hoja ya msingi sana...kwa mfano kabla ya ugunduzi wa antibiotics dunia ilipata shida sana katika kukabiliana na magonjwa yanayosababishwa na bacteria na baada ya ugunduzi huu dunia ilishuhudia kupungua kwa magonjwa hayo na vifo vitokanavyo.

Bado ninaamini utafiti na ugunduzi unaendelea kwa kasi hasa hasa katika eneo la kukinga magonjwa.

Chanjo kadhaa zimegunduliwa ingawa ukiwa Tanzania huwezi kuzishuhudia sana...mfano chanjo ya magonjwa ya kuhara kwa watoto chini ya miaka mitano ilikuwepo muda mrefu tu lakini kwa Tanzania imeingia hivi karibuni na manufaa yake yameanza kuonekana.

Kuna magonjwa kama kifua kikuu tukifanikiwa kuwagundua wagonjwa wote wa kifua kikuu na kuwapa dawa hatimaye tutatangaza kuwa T.B ni historia duniani.

Kuna ugonjwa kama polio ...dunia inahangaika kuutokomeza kabisa lakini kuna baadhi ya maeneo jamii inakataa kuchanjwa kwa kisingizio kuwa chanjo hiyo inasababisha ugumba.

Kwa ufupi naweza kusema kuwa ili mada yako iwe valid ni lazima ukaangalia factors kadhaa zinazopelekea ill health ambazo kwa kiasi kikubwa jamii ya wataalamu wa afya wamezigundua ingawa preventive approach zinategemea sana other sectors.

leo hii dawa ya kumuua bacteria wa kipindupindu ipo kiasi kwamba kama kila sector ikiplay role yake basi bacteria hao wanawezwa kumalizwa kabisa.
 
Mafua Yaliua Watu Yamepatiwa Dawa Naona Hujaongelea Hilo

Ukoma Uliua Watu

Tetanus Iliua Watu

Kifua Kikuu

Naona Hayo Yote Hujaona...kila Kitu kina Muda Wake Kitapata Dawa Kulingana Na Mapenzi yake Mungu mwenyewe
Nimekupata mkuu.
 
Una hoja ya msingi sana...kwa mfano kabla ya ugunduzi wa antibiotics dunia ilipata shida sana katika kukabiliana na magonjwa yanayosababishwa na bacteria na baada ya ugunduzi huu dunia ilishuhudia kupungua kwa magonjwa hayo na vifo vitokanavyo.

Bado ninaamini utafiti na ugunduzi unaendelea kwa kasi hasa hasa katika eneo la kukinga magonjwa.

Chanjo kadhaa zimegunduliwa ingawa ukiwa Tanzania huwezi kuzishuhudia sana...mfano chanjo ya magonjwa ya kuhara kwa watoto chini ya miaka mitano ilikuwepo muda mrefu tu lakini kwa Tanzania imeingia hivi karibuni na manufaa yake yameanza kuonekana.

Kuna magonjwa kama kifua kikuu tukifanikiwa kuwagundua wagonjwa wote wa kifua kikuu na kuwapa dawa hatimaye tutatangaza kuwa T.B ni historia duniani.

Kuna ugonjwa kama polio ...dunia inahangaika kuutokomeza kabisa lakini kuna baadhi ya maeneo jamii inakataa kuchanjwa kwa kisingizio kuwa chanjo hiyo inasababisha ugumba.

Kwa ufupi naweza kusema kuwa ili mada yako iwe valid ni lazima ukaangalia factors kadhaa zinazopelekea il health ambazo kwa kiasi kikubwa jamii ya wataalamu wa afya wamezigundua ingawa preventive approach zinategemea sana other sectors.

leo hii dawa ya kumuua bacteria wa kipindupindu ipo kiasi kwamba kama kila sector ikiplay role yake basi bacteria hao wanawezwa kumalizwa kabisa.
Poa nimepata darasa zuri sana kutoka kwako.
 
Similar Discussions

1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom