AFYA: Jinsi ya kumsaidia mtoto wako aweze kutambaa

OCC Doctors

Member
Jul 20, 2018
48
125
Jinsi ya kumsaidia mtoto aweze kutambaa, haswa kwa wale watoto ambao wameshafikisha umri wa kutambaa lakini hawataki kutambaa wala kusimamia vitu.

Namna ya kumsaidia unatakiwa kumpa mtoto muda mwingi wa kulalia tumbo (Tummy time), unamlaza mtoto kwa tumbo akiwa macho na chini ya usimamizi, hii husaidia mtoto kukaza misuli ya shingo na mabega ambapo viungo hivyo hupata nguvu na uwimara. Weka kiganja chako cha mkono nyuma ya miguu ya mtoto wako wakati anapotandaza mikono na miguu yake.

Pia njia hii humsaidia mtoto kutokuwepo na kichwa mparazo kwa nyuma (positional plagiocephaly) ambacho ni kichwa kisicho na uchogo kiko flat kwa nyuma.

Mhimize mtoto wako afikie vitu vya kuchezea ambavyo anapendezwa navyo. Hakikisha mtoto ana nafasi ya kucheza ambayo ni salama. Midoli yenye umbo za kiroho haipendezwi kutumika kuwavutia watoto wadogo, mnunulie toys zenye rangi mchanganyiko na ambazo hazina maumbile ya mnyama wala binaadamu.

tummy-time.jpgbaby-hip-joints.jpg


Zizu-opens-hip-joints.jpg
 

safuher

JF-Expert Member
Feb 11, 2019
6,758
2,000
Pia njia hii humsaidia mtoto kutokuwepo na kichwa mparazo kwa nyuma (positional plagiocephaly) ambacho ni kichwa kisicho na uchogo kiko flat kwa nyuma
Hapa sijakuelewa mkuu,mtoto kalalia tumbo kunaepusha vipi kuwa na kichwa mparazo cha kizenji mkuu ?
 

OCC Doctors

Member
Jul 20, 2018
48
125
Hapa sijakuelewa mkuu,mtoto kalalia tumbo kunaepusha vipi kuwa na kichwa mparazo cha kizenji mkuu ?
Kichwa mparazo hutokea wakati mtoto anapotumia muda mwingi kulala chali. Hivyo basi kubadilisha msimamo au mlazo wa kichwa cha mtoto kunaweza kusaidia kuepuka hali hiyo, na moja ya njia hiyo ni kupendelea kumlaza mtoto kwa tumbo anapokuwa macho tena chini ya uwangalizi.
 

safuher

JF-Expert Member
Feb 11, 2019
6,758
2,000
Kichwa mparazo hutokea wakati mtoto anapotumia muda mwingi kulala chali. Hivyo basi kubadilisha msimamo au mlazo wa kichwa cha mtoto kunaweza kusaidia kuepuka hali hiyo, na moja ya njia hiyo ni kupendelea kumlaza mtoto kwa tumbo anapokuwa macho tena chini ya uwangalizi.
Duuh hivi ndo vichwa vya kizenji ambavyo havina visogo sio ?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom