Afutiwa kesi ya uhujumu uchumi na kufunguliwa nyingine ya jinai

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
3,822
2,000
kesi pc

Dar es Salaam. Aliyekuwa Mkurugenzi wa Mipango, Ufuatiliaji na Tathimini wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Kulthum Ahmed (57) amefutiwa kesi ya uhujumu uchumi na kisha kufunguliwa kesi ya jinai yenye mashtaka saba yakiwemo ya kujipatia Sh34 milioni kwa njia ya udanganyifu.

Kulthum anadaiwa kujipatia Sh34milioni, kutoka kwa watumishi sita wa Takukuru kwa madai kuwa angewauzia viwanja, wakati akijua ni uongo.

Awali Kulthum alikuwa anakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi namba 26/2019 yenye mashtaka nane, likiwemo la kutakatisha fedha kiasi cha Sh1.4bilioni katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Uamuzi wa kuifuta kesi hiyo ya uhujumu uchumi umetolewa leo, Julai 19, 2021 na Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi baada ya upande wa mashtaka kuwasilisha hati ya kuondoka kesi ya uhujumu uchumi.

Wakili wa Serikali, Ester Martin ameieleza mahakama hiyo kuwa DPP amewasilisha hati ya kutokuwa na nia ya kuendelea na kesi ya uhujumu uchumi dhidi ya mshtakiwa huyo.

Mshtakiwa baada ya kufutiwa kesi hiyo, alikamatwa tena na kufunguliwa kesi ya jinai 118/2021 yenye mashtaka saba na kisha kusomewa mashtaka mapya.

Akisomewa kesi mpya, wakili wa Serikali, Sylvia Mitanto akisaidia na Yusph Abood, amedai katika shtaka la kwanza ambalo ni kughushi, mshtakiwa anadaiwa kutenda kosa hilo, kati ya Januari 2013 na Mei, 2018, ambapo akiwa Makao Makuu ya Takukuru eneo la Upanga, kwa nia ovu ya kutenda kosa alighushi barua ya ofa ikionyesha barua hiyo imetoka katika halmashauri ya Bagamoyo huku akijua kufanya hivyo ni kosa la kisheria.

Kosa la pili, kati ya Januari 2012 na Mei 2017 akiwa eneo la Upanga mshitakiwa alijipatia fedha kwa njia ya udanganyifu kiasi cha Sh5.2milioni kutoka kwa mtumishi wa Takukuru, Alex Mavika kama malipo ya kiwanja kilichopo kijiji cha Ukuni wilayani Bagamoyo, wakati akijua kuwa yeye sio mmliki wa eneo hilo na hawezi kumuuzia mtumishi huyo.

Kosa la tatu siku na maeneo hayo, alijipatia fedha kwa njia ya udanganyifu kiasi cha Sh3 milioni, kutoka kwa mtumishi wa Takukuru, Wakati Katondo

Shtaka la nne, alijipatia fedha kwa njia ya udanganyifu Sh5 milioni kutoka kwa mtumishi wa Takukuru, Gogo Migutah.

Kosa la tano, alijipatia fedha kwa njia ya udanganyifu kiasi cha Sh7 milioni kutoka kwa mtumishi wa Takukuru, Ekwabi Majungu.

Katika kosa la sita anadaiwa kujipatia Sh7milioni kutoka kwa mtumishi wa Takukuru, Nkwabi Majungu huku shtaka la saba alikijipatia fedha kiasi cha Sh7 milioni kutoka kwa Rose Shigela.

Mshtakiwa baada ya kusomewa mashtaka yake alikana na upande wa mashtaka umedai upelelezi haujakamilika, hivyo wanaomba tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa.

Wakili wa mshtakiwa, Elia Mwingira aliiomba mahakama itoe dhamana kwa mteja wake kwani mashtaka yanayomkabili yanadhaminika.

Hakimu Shaidi alitaja mashtaka ya dhamana ambayo, mshtakiwa ametakiwa kuwa na wadhamani wawili wenye barua kutoka taasisi zinazotambulika kisheria pamoja kitambulisho cha Taifa watakaosaini Bondi ya Sh20 milioni.

Mashtakiwa amefanikiwa kutimiza masharti na kuachiwa kwa dhamana.

Hakimu Shaidi ameahirisha kesi hiyo hadi Agosti 3, 2021 itakapotajwa.

Mwananchi
 

PSPA Pure'12 udsm

JF-Expert Member
Jan 11, 2013
818
500
Alafu anatokea mtu mmoja kutoka kusikojulikana anakwambia JPM aliletwa na Mungu...unamwanagaliaa weeeee, unamwacha siku ya mwisho akaendelee kuongozwa hko alikotangulia.

Even though mama alipiga, sio kuhujum uchumi. Miaka mitano iliyopita nchi hii ilikua na wahujumu uchumi na watakatisha fedha pekee...shame!
 

Pakawa

JF-Expert Member
Mar 11, 2009
6,787
2,000
Hawa wakati mwingine si wa kuwahurumia
Kuna wafanyakazi huko kwenye idara wizara vitengo wanaumiza watu khe
Hawana huruma roho za ukatili dhuluma
Mahospitalini ndio balaa
WaTz hizi roho mbaya zinachangia kurudisha maendeleo ya watu
Sasa huyu naye akalipe ujira wake
Dhuluma mbaya
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom