Afungwa jela maisha kwa kulawiti kubaka mpwa wake Mbeya

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Aug 2, 2021
1,023
1,609
Aidha, kijana huyo anadaiwa kumwambukiza mtoto huyo magonjwa ya zinaa.

Hukumu hiyo ilitolewa juzi na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Chunya, James Mhanusi, baada ya kusikiliza pande zote mbili na kujiridhisha pasi na shaka kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo.

Awali, akisoma mashtaka katika kesi hiyo ya jinai namba 64 ya mwaka 2022, Mwendesha Mashitaka wa Polisi, Mazoya Luchagula, aliiambia mahakama kuwa mshtakiwa alitenda makosa hayo kwa nyakati tofauti kati ya Aprili na Mei 5, mwaka huu.

Mazoya alisema makosa hayo ni kinyume cha kifungu namba 130(1)(2) na kifungu namba 131(1), Sura ya 16 ya Sheria ya Makosa ya Jinai iliyofanyiwa marejeo mwaka 2019.

Mtuhumiwa alikana mashtaka yote na ndipo upande wa mashtaka ukalazimika kuleta mashahidi mbalimbali mahakamani hapo.

Miongoni mwa mashahidi waliofikishwa mahakamani hapo ni pamoja na mtoto aliyefanyiwa ukatili huo, ambaye alimtambua mshitakiwa kwa kumwita β€˜anko’ (mjomba).

Mashahidi wengine wa mashtaka waliotoa ushahidi wao mahakamani hapo ni mama mzazi wa mtoto, askari, ofisa ustawi wa jamii wa wilaya na daktari aliyewasilisha fomu ya polisi namba tatu (PF3) iliyoambatana na vipimo vilivyoonesha mtoto kubakwa na kuingiliwa kinyume cha maumbile.

Baada ya Hakimu Mhanusi kusikiliza upande wa mashtaka na upande wa mshtakiwa, alisema mahakama iliridhika na ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka na kwamba mshtakiwa ana kesi ya kujibu.

Akijitetea mbele ya mahakama hiyo, mshtakiwa Mawanga alidai kuwa hakutenda makosa hayo na kwamba anasingiziwa, huku akiiomba mahakama kumwachia huru kwa kuwa mama yake, mke na wadogo zake wanamtegemea.

Upande wa mashtaka ulidai kuwa licha ya mshtakiwa kutokuwa na matukio mengine ya uhalifu, unaiomba mahakama kutoa adhabu kali kwa mshtakiwa ikizingatiwa mtoto aliyefanyiwa ukatili ana umri wa miaka minne na isitoshe ni mtoto wa dada yake.

Hakimu Mhanusi baada ya kuzisikiliza pande zote, alisema Mahakama inamtia hatiani kwa makosa yote mawili, ya kumbaka mtoto chini ya miaka 18 na kumlawiti ambayo kifungo chake ni cha maisha jela.

Hakimu Mhanusi alisema adhabu hiyo iwe fundisho kwa mshtakiwa na watu wengine wanaojihusisha na vitendo hivyo hasa kutokana na kukithiri ubakaji na ulawiti kwa watoto wilayani Chunya.

Vitendo vya ulawiti na ubakaji wa watoto wilayani Chunya vinahusishwa na imani za kishirikina kwa madai kuwa watu wanaweza kupata dhahabu punde wanapojamiiana au kuwalawiti watoto wadogo.

Hakimu Mhanusi alisema kwa makosa yote mawili mshitakiwa atatumikia adhabu zote mbili kwa pamoja gerezani.


Chanzo: Nipashe
 
Nakazia afungwe na yeye alawitiwe 3X365X50
Tumechoka hii nchi kuona wangese kama hawa.
Hayo mambo jela hayapo labda utake wewe na wajelajela wasikushike au wasijue utajuta

Sana sana ataenda lima huyo ,atalala cello nzuri,atakula msosi mzuri tofauti na wenzake huwa vifungo vya maisha wanazingatiwa


Ingetakiwa wanyongwe kabisa
 
Jamaa kashindwa kabisa hata kununua malaya wa bukubuku hapo mafiati

Fala sana huyu
MKUU π™·πšžπš”πš˜ πš—πš’ πšŒπš‘πšžπš—πš’πšŠ ,𝚊𝚏𝚞 πš—πšπšŠπš—πš’ πš’πšŠπš”πšŽ πš”πšžπš—πšŠ πš’πš–πšŠπš—πš’ 𝚣𝚊 πš”πš’πšœπš‘πš’πš›πš’πš”πš’πš—πšŠ
 
MKUU π™·πšžπš”πš˜ πš—πš’ πšŒπš‘πšžπš—πš’πšŠ ,𝚊𝚏𝚞 πš—πšπšŠπš—πš’ πš’πšŠπš”πšŽ πš”πšžπš—πšŠ πš’πš–πšŠπš—πš’ 𝚣𝚊 πš”πš’πšœπš‘πš’πš›πš’πš”πš’πš—πšŠ
Aisee basi itakuwa ni imani ya kishirikina sio ugumu
 
kati ya habari zinazo huzunisha sana ni hizi za kubaka, kulawiti watoto.
watoto wana haribika sana kiasaikolojia, kiakili, kimwili na kiimani.

Miaka 30 haitoshi
 
Back
Top Bottom