Afungua kesi mahakama ya Mwanzo Ilala kudai talaka baada ya kunyimwa tendo la ndoa kwa miaka mitano

Idugunde

JF-Expert Member
May 21, 2020
6,273
6,637
Ndoa zimekuwa na utata kila kukicha, sasa mtu ana miaka 62 anataka kumuaacha kwa nini? Au ndio kutaka kugawana mali mapema?

Adela Ngogolo (42) amefungua kesi ya madai mahakama ya mwanzo Ilala akiomba kupewa talaka na mumewe, Alcado Mkondola (62) kwa madai kuwa ameshindwa kumpatiwa haki yake ya tendo la ndoa kwa miaka mitano. Adela na mumewe kwa pamoja wanaishi Tabata Kimanga jijini Dar es Salaam.

Kwa hisani ya Dar Mpya.
 
HAPO KINACHOTAFTWA NI KUGAWANA MALI WALA SI TENDO LA NDOA!
Na ukichunguza sana unakuta huyo mwanamke ndo alianza kuchepuka mzee akaamua kutokumpa talaka kuhofia Mali,
Huenda mzee Mali kaona azihamishe taratibu kwa watoto!
Huyo mwanamke kagundua mchezo kaona aje na ombi la talaka kwa kukosa unyumba!

LAKINI LENGO NI MALI NA NYUMBA!
Kama watoto wa huyo mzee ni wakubwa wanajitambua;
Dawa ni kupita naye hivi huyo mwanamke mapema sana! Kosakosa aokote hata makopo potelea mbali
 
Back
Top Bottom