Afumaniwa na dada yake akijivinjari na shemeji yake

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,318
33,125
MSICHANA mmoja wa Shule ya Sekondari Mbezi Beach jijini Dar es Salaam jana alileta kituko cha mwaka baada ya kufumaniwa na dada yake akijivinjari na shemeji yake chumbani kwa dada yake huyo mkazi wa Magomeni jijini Dar es Salam. Msichana huyo anayesoma kidato cha tano katika Shule ya Sekondari Mbezi Beach alifumaniwa jana akiwa katika zoezi la kujaribu kumpa uroda shemeji yake ambaye ni mume wa dada yake binamu.

Ama kweli siku za mwizi ni arobaini wahenga walisema, msichana huyo aliyetambulika kwa jina la Joyce Asenga alikuwa akiishi na dada yake binamu aliyejitambulisha kwa jina moja la Mary,walikuwa wakiishi huko Magomeni Makanya eneo linalojulikana Kanisani jijini Dar es Salaam.

Akiongea na NIFAHAMISHE katika kituo cha polisi dada wa msichana huyo alisema jana alipokuwa kazini walipata taarifa kuwa kuna mwenzao mmoja alipatwa na matatizo alifiwa na mzazi wake na taarifa hizo kufikishwa kazini hapo na ilibidi baadhi ya wafanyakazi kwenda eneo la msibani kwa kumfariji mwenzao huyo.

Alisema wakati anataka kuelekea msibani huko alijikuta hayupo katika mazingira ya kwenda msibani mana alitinga sketi fupi maarufu kama “mini skirt” hali ambayo asingeweza kwenda nayo kwenye msiba huo.

Alisema ilimladhimu akimbie mara moja nyumbani kwake ili akachukue kanga ama kitenge ili aweze kujihifadhi aeleke msibani huko maeneo ya Kigamboni.

Alisema wakati anafika nyumbani kwake hapo alijua kama kawaida kusingekuwa na mtu mana anaishi na mumewe na mdogo wake huyo, alifungua geti ulifunguka.

Sasa wakati anajitayarisha achukue funguo wa kuingilia chumbani kwake alishangaa mlango kuwa wazi alijua labda kuna wezi walivamia na kuiba.

Ghafla alipofungua mlango huo ndipo alipomkuta mumewe na mdogo wake huyo wakiwa chumbani hali ambayo ilifanya ashangae mana asubuhi waliongozana wote kila moja akiwa anaenda kazini na msichana huyo kuelekea shuleni.

Alisema alichokifanya ni kutoka nje kufunga mlango huo wa chumbani na kutoka na kufunga geti na kutaarifu baadhi ya ndugu waliopo jirani ili waweze kuwakuta kwa ushahidi zaidi na kisha kukimbilia kituo cha polisi.

Aliomba msaada wa kituo cha Polisi kilichopo Magomeni ili wawachukue wawaweke selo.

Akihojiwa na askari kituoni hapo msichana huyo alisema kuwa hajawahi kufanya nae kitu chochote kwa kuwa shemeji yake huyo alikuwa anamuhitaji kewa muda mrefu nay eye alikuwa ahitaji kuwa nae kimapenzi, ila siku hiyo shemeji yake huyo alimpa mkwara kuwa kama asingemkubalia basi asingeweza kuendelea na masomo yaani asingeweza kumsaidia tena kumlipia ada.

Ndipo alipojitosa kwa siku hiyo ili aweze kumridhisha ili aweze kuendelea na shule ambayo alitegemea ndiyo ingekuwa mkombozi wake katika maisha.

Hata hivyo dada huyo aliyefumania alisema na kuwataka polisi wamuweke msichana huyo na mume wake huyo ndani ili waweze kupata adabu kwa kitendo chao cha utovu wa nidhamu walichokifanya chumbani kwake.

“Unajua hatukatai wname ni ewachafu sana tunajua hilo ila kwea nini afanye mapenzi na mdogo wangu chumbani kwangu angeenda sehemu nyingine hata gesti hii ni dharau” alisema

Alisema mume wake huyo ni mfanyakazi wa Wizara ya Ardhi huku yeye mwenyewe akiwa anafanyia kazi Shirika la Hifadhi ya Jamii [NSSSF]

Hata hivyo dada huyo hakuwa tayari kutaja jina la mumuwe kwa kuwa alidai angedhalilika zaidi.

NIFAHAMISHE ilipojaribu kufanya mahojiano na baba huyo haikufanikiwa mana hakuwa tayari kuongelea kitu chochote dhidi ya tukio hilo.

Hivyo NIFAHAMISHE ilipoondoka eneo la kituoni hapo waliacha waharifu hao wakiwa bado kituoni hapo na dada huyo kudai kuwa kwa kitendo alichokifanya mume wake huyo hayuko tayari kuishi nae na mdogo wake huyo atamrudisha kwa wazazi wake na atafute mfadhili mwingine wa kumsomesha.
 
Kaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaazi kweli kweli!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Do huyo dogo alilemewa na msongo wa mawazo kuhusu shule
ndio maana huyo jamaa akatake advantage ya weeknes point ili
apige mambo yetu yale sister anatakiwa aongee na dogo wake mara
mbili pia amuiotie mumewe wazee wamkanye cha msingi asijaribu lipiza kisasi
kama ilivyo kawaida ya wadada inawezakuleta madhara makubwa pia kuhusu
mdogo wake amsaidie amalize skuli kwakuwa inaonekana ana malengo freshi na elimu
so uzalendo ulimshinda ndio maana ikawa hivyo
 
Mhhh..ndo utakatifu wetu wa kileo. Kila kitu ruksa.Hatuna mwiko tena!Duuh, sijui tutafikaje mwisho wa safari mana
 
Naomba kuuliza. Hivi kisheria unaweza kwenda kuchukua Polisi waje kukamata wagoni wako, mmoja akiwa mumeo??
 
Ulimwengu umekwisha kwa kweli.....
Ina maana jamaa alikacha kazi siku hiyo kwa ajili ya shughuli nzito hiyo, kumbe ameumbuka......
Dada mtu hongera sana, na afadhali mungu amekuongoza kuona kwa macho yako. Na kama utaamua kutaendelea na mumeo, ni heri mkapime kwanza, maana unaweza kukuta huyo mmeo hiyo ni tabia yake mpaka huko kazini kwake.

Take care of your life (maisha yako ni bora kuliko kazi uliyonayo)
 
Granted kama report ni accurate huyu jamaa ni bonge la bazazi.

Funny huyu dada hataki kutaja jina la mumen wake kwa sababu mumewe ataadhirika wakati kataja jina la mdogo wake, mwanafunzi wa shule ambaye inawezekana kabisa alifanyiwa "statutory rape".

Halafu wanawake wanaweza kulalamikia "mfumodume" kweli?

Kama kweli alikuwa na concern ya familia kudhalilika kwa nini kaenda polisi after all? Halafu hizo licentious comments zina maana gani? Kwamba angefanya gesti ingekuwa sawa?

At the risk of blaming the victim, wanawake wengine wanakuwa wajinga sana kwenye haya mambo.
 
kuna wengi wanaofanya mambo machafu kama haya ila familia inaficha uchafu wao na aibu hiyo
 
Ingekuwa ni mimi huyo mwenye mume ningeanza kwa kutaja jina la huyo mume ili aaibike zaidi maana hana adabu. Unajua hakuna kitu cha aibu kama kutongoza shemeji yako hata ndugu wa mume. likewise kwa wake zetu kutembea au kukubali kutongozwa na ndugu wa mume. Hiyo ndoa ni walakini unless kama wanaishi tu kiswahili bila urasmi wowote, maana ukiona mwanaume/mwanamke amabaye anapendezewa na ndoa zisizo rasmi ujue kuna hitilafu fulani.

Bado huyo mke aliendelea au ataendelea kuishi na huyo mume!!!?? Asalale!!!!
 
Lakini na wanawake nao wanatafuta lawala tu wakati mwingine,kama mdogo yupo bomba na alama za nyakati zinaonyesha muelekeo,na asipokuwepo dada mtu tunabaki wawili tu hapo home,aah jamani..lolote laweza kutokea bana,simlaumu sana huyo jamaa!!
 
Naona shemeji alikuwa anataka apewe fadhila za kumsomesha,unajua hawa watoto wa siku hizi wanapendeza sana,unakuta kenyewe kamevaa tukanga tumoja alafu kana jipitisha mbele ya shemejiwe unategemea kitu gani hapo kitafuata kwa mwanaume mkware?kama sio kuomba kamchezo kama hivyo alivyo fanya jamaa.wa kinadada kuweni sana makini na wadogo zenu mnaoishi nao.
 
unajuw nwanawake wavumivu sana tena sana kuliko wanamume, wewe utaona baada ya muda hanamsamehe mumewe na wanaendelea kuishi ila sisi wagumu sana , jamani wanaume tuwe na moyo wa kusamehe
 
teh teh, kwani mkeo ukimfuma na kaka yako au Jirani yako ipi itakuuma mi naona afazali mdogo mtu...Kwani ule mswazi wakisema kizuri kuna na ndugu yako unaimanisha nini?...
 
Granted kama report ni accurate huyu jamaa ni bonge la bazazi.

Funny huyu dada hataki kutaja jina la mumen wake kwa sababu mumewe ataadhirika wakati kataja jina la mdogo wake, mwanafunzi wa shule ambaye inawezekana kabisa alifanyiwa "statutory rape".

Halafu wanawake wanaweza kulalamikia "mfumodume" kweli?

Kama kweli alikuwa na concern ya familia kudhalilika kwa nini kaenda polisi after all? Halafu hizo licentious comments zina maana gani? Kwamba angefanya gesti ingekuwa sawa?

At the risk of blaming the victim, wanawake wengine wanakuwa wajinga sana kwenye haya mambo.

Duu, aliye tendewa kosa ndo kaisha kuwa mjinga? si afadhali hata alipata akili ya kuita polisi, kuliko angeibua panga na kummaliza mwizi wake?

Haya mambo yasikie tu kwa mwenzio, yakikuta wewe ndipo utathamini hekima ya mwenzio, kumbuka hapo kinachokuwa kinafanya kazi si 'brain' ni 'adrenalin' mkuu!
 
unajuw nwanawake wavumivu sana tena sana kuliko wanamume, wewe utaona baada ya muda hanamsamehe mumewe na wanaendelea kuishi ila sisi wagumu sana , jamani wanaume tuwe na moyo wa kusamehe

teh teh, kwani mkeo ukimfuma na kaka yako au Jirani yako ipi itakuuma mi naona afazali mdogo mtu...Kwani ule mswazi wakisema kizuri kuna na ndugu yako unaimanisha nini?...

Kizuri kula na ndugu yako!

Sure thing.

Acheni kushabikia maovu.
Mume wa namna hii hafai maana anapandikiza mbegu mbaya ya uchonganishi kwenye familia.
 
Back
Top Bottom