Afukuzwa kazi kwa kutopokea simu ya Trump

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,498
9,279
pic+afukuzwa.jpg



Kwa ufupi
Bharara aliambia shirika la habari la ABC kwamba alihisi simu hizo kutoka kwa Rais Trump zilikuwa zimevuka mipaka ya kawaida inayotenganisha ofisi ya rais na uchunguzi huru wa uhalifu.

Washington, Marekani. Mwendesha mashtaka mkuu wa zamani wa New York, Preet Bharara amefichua siri kwamba alifutwa kazi na Rais Donald Trump baada ya kupokea simu kadhaa zisizokuwa za kawaida kutoka kwa rais huyo.

Bharara aliambia shirika la habari la ABC kwamba alihisi simu hizo kutoka kwa Rais Trump zilikuwa zimevuka mipaka ya kawaida inayotenganisha ofisi ya rais na uchunguzi huru wa uhalifu.

Katika mahojiano hayo Bharara alisema alifutwa kazi baada ya kukataa kupokea simu ya tatu ya Trump. Ikulu ya White House haikujibu mara moja madai hayo.

Bharara ambaye aliteuliwa na Rais Barack Obama kufanya kazi Manhattan alisema kuwa Trump alionekana kujaribu kujenga uhusiano fulani baada ya wawili hao kukutana mwaka 2016.

"Rais Obama hakunipigia simu hata mara moja katika kipindi cha miaka saba unusu," alisema Bharara.



Chanzo; mwananchi
 
ahahahahaha, makubwa hayo, acha nicheke mie!!! Ukubwa ni shida sana, bora mie
 
Back
Top Bottom