Afuata Nyayo za Baba Yake Kwa Kujiua Kwenye Reli | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Afuata Nyayo za Baba Yake Kwa Kujiua Kwenye Reli

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mbonea, Nov 8, 2009.

 1. Mbonea

  Mbonea JF-Expert Member

  #1
  Nov 8, 2009
  Joined: Jul 14, 2009
  Messages: 640
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  </SPAN>
  Sunday, November 08, 2009 4:01 AM
  Mwanamke nchini Uingereza amefariki kwa kusagwasagwa na treni baada ya kujilaza kwenye reli wakati treni iliyokuwa kwenye spidi ikikatiza zikiwa ni siku tatu tu baada ya baba yake kujiua sehemu hiyo hiyo na kwa staili hiyo hiyo.


  Colleen O'Connor, 39, alikutwa amefariki juu ya reli mwili wake ukiwa umesagwasagwa na treni baada ya kujilaza juu ya reli katika kitongoji cha Kidderminster, Worcestershire.

  Colleen aliamua kujiua siku tatu baada ya baba yake Barney O'Connor, 64, kujiua kwa kujilaza kwenye reli wakati treni ikikatiza.

  Colleen alijiua katika eneo la reli hiyo ambalo baba yake alijiua siku tatu zilizopita.

  Baba yake Colleen inaaminika aliamua kujiua baada ya ndoa yake kuvunjika na mkewe kuolewa na mwanaume mwingine.

  Taarifa zilisema kwamba Colleen alisafiri kutoka nyumbani kwake katika mji mwingine wa Dorset hadi katika eneo ambalo baba yake alijiua na yeye pia kujiua kwa njia ile ile aliyoitumia baba yake.

  Taarifa iliyotolewa na familia ya O'Connor ilisema kwamba wamehuzunishwa na vifo hivyo na walivitaka vyombo vya habari viwape nafasi ya kuombeleza kwa kukaa mbali na eneo ambalo waombelezaji wamekusanyika.

  Bwana O’Connor alifariki baada ya kugongwa na treni alipojilaza kwenye reli siku ya alhamisi oktoba 29 kwenye majira ya saa 12 na nusu jioni.

  Colleen alijiua kwenye eneo hilo hilo siku ya jumapili novemba 1 kwenye majira ya saa mbili na nusu usiku.
  </SPAN>

  Source: NIFAHAMISHE
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Nov 8, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Too bad to digest!

  Kuna jamaa hapa ndani anaitwa Pdidy alileta Thread inayohusu mambo ya KUKABILIANA NA MACHUNGU YA KUACHWA. Mimi binafsi niliguswa sana na lile Bandiko!

  Haya ni katika madhara ya aina hiyohiyo, ambapo mtu anakuwa amekosa ujasiri wa kuendelea kuishi baada ya kuachwa, na anaona njia pekee ni kujiua, matokeo yake uchungu huu unakuwa hasara kubwa zaidi kwa familia, maana wanatokea wengine wanaochukua mkondo wa mzazi, wanaamua kujimaliza, kuliko kuendelea na maumivu...too bad!

  Hapa Tanzania hakuna, au labda niseme kunasehemu chache mno za counselling, ambapo zingekuwa muhimu mno kwa watu wanaochukua maamuzi ya haraka na ya kughafirika kama hivyo.
  Poleni sana familia hii...Ninajua uchungu alioupata huyu mzee!...Wanawake Bwana...we waache tu!
   
 3. Dr. Chapa Kiuno

  Dr. Chapa Kiuno JF-Expert Member

  #3
  Nov 8, 2009
  Joined: Sep 11, 2009
  Messages: 445
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Totally ryt bro.
   
 4. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #4
  Nov 8, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,168
  Likes Received: 5,594
  Trophy Points: 280
  Mkuu Paka jimmy tuko pamoja ndugu

  hakika tunaitaji mungu aingilie kati...leo hii kuna mhubiri mmoja kutoka Nigeria alikuwa akifundisha swala la ndoa kwa kweli ni vitu vya kusikitisha jinsi watu wanavyoamua kudharau hili jambo na kwenda kinyume na MUNGU kwa kuamua kumwacha mwenzako bila kujua madhara yatakayotokea baadae...baya zaidi wapo amabo wamebahatika kuzaa kwenye ndoa bila kuangalia tunaachana watoto watatunzwaje...familia zitaishije......
   
 5. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #5
  Nov 8, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,168
  Likes Received: 5,594
  Trophy Points: 280
  Ndugu zanguni kuna njia nyingi za kutengeneza ndoa zetu...ni kweli mtu anaweza kuona hata haya ninayosema amejaribu lakini bila mafanikio...ndugu yangu,baba mama dada kaka...bila kujali umri MUNGU pekee ndie kimbilio letu...ukiwa ndani ya msuko suko wa ndoa naomba usikate tamaa ya miahsa kama ndugu zetu..wengi watakuja kumsingizia shetani kwa waliofanya lakini si kweli ni sisi binadamu ndio waanzilishi wa vilio kama hivi vya ndugu zetu huko uk..
  jambo la kufanya ukiwa ndani ya ndoa usisubiri yalipuke

  1)tengeneza amani muda wote kwenye ndoa yako...hii nikimannisha wapo wengi wanaoachana kwa huzuni kubwa kisa kutokuwa na amani...wapo wanaoachana kisa kutopikiwa chakula mapema,,kuchelewa kurudi usiku,kutofua nguo muda muafaka..kutokaribishwa chakula baada ya mapishi...na mengineyo haya yote tukiwa kama binadamu tunaitaji kujua weakness za wenzetu na wewe kama unaweza kubadilika vyema ukarekebisha jambo hilo mapema ili muwe na amani...ni jambo la mzaha lakini ni ukweli halisi mh apo juu alikosa amani nyumbani na kuishia kujiua

  2)MUOMBEE MWENZIO KILA UAMKAPO NA ULALAPO
  Ndugu wapendwa hakuna kinachomuumiza shetani kama maombi ya wapendanao...wapo watu wengi wasiojua siri hii lakini mimi nimemwona mungu live....ukiingia kwenye ndoa uusisubiri kulipuke uanze ngonjera za kumlilia MUNGU...NO anza sasa kila uamkapo mwombee MME/MKE wako mwambi MUNGU amlinde na mabaya yote na kama unajua udhaifu wake taja kwa mdomo mwambie MUNGU kila mwanamke atakaesogelewa na mmme wangu awe KINYAA mbeleyake..jamani kuna NGUVU ya matamshi hatujui tu kutumia katika sala..kwa hili hata zile nguvu za shetani za kuwarudisha wanandoa usiku azisogei nawahahakikishia....
  MUNGU AKAPATE LINDA NDOA YAKO WEWE UNAESOMA IN JESUS NAME
   
 6. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #6
  Nov 8, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,168
  Likes Received: 5,594
  Trophy Points: 280
  3)FURAHIA +VE ZAKE
  Hapa naongelea swala la kumkubali mwenzi wako..ndoa nyingi zinakuwa na migongano katika swala la acceptance...ukiwa kama mmwanandoa unatakiwa kumu accept mwennzio wako...usisubiri kuona jambo baya anafanya then uanze kumsema na hata kutukana nana...leo hii shetani ametawala ndoa nyingi sana...yupo mama yangu mdogo aliolewa akiwa na umbo la umodo...walipendana sana ndoa yao na mpaka wengine waliowahi kuogopa ndoa wakaamua kutafuta wenzio wao...mama baada ya watoto 3 mwili ukaanza kunenepa wenyewe...jamani mi sitaki kuwa shaidi ila ukweli halisi sijui nimuite baba mdogo...alianza kutoka nje ya ndoa kama ametupiwa jini maahaba...akiulizwa mbona mme wangu umebadilika hivi analalamami siwezi bwana nimekuoa ukiwa mwembamba iweje leo hiiunenepe kama tipwa tipwa...mama wa watu akaanza kunywa alovera...kunywa tianshi..kunywa kila dawa anayotangaziwa kuondoa unene...siku moja wakiwa kanisani na mumewe wala si mbali pale ubungo assemblies kutoa shukran ya mttoto wao wa tatu..Mungu aliamua kumtumia mchngaji alimwaga neno...la kumkubali mwenzio katika ndoa....yule baba jamani alitoa machozi alilia ...leo hii afichi mtu kumwambia anmpenda mwenzake jinsi alivyo...alivyomaliza kanisan akaulizwa mbona umelia akasema mchungaji neno la leo nahisi ni neno langu...hata wewe unaemdharau mwenzio wake kwa sababu ya maumbile..kiungo chake chochote...pesa zake ama hana kazi...ndugu mkubali alivo huyo ndieMUNGU AMEKUPA...IPO SIKU ATAMBADILISHA

  4)MWOMBE ROHO MTAKATIFU AWE KIONGOZI WA NDOA YENU
  Watu wengi wamekuwa wakiamini wanauwezo wa kuoa ama kuolewa na kuishi kwa uwezo wao binafsi..ndugu leo hii nikupe siri kubwa ya ndoa zenye baraka....mkaribishe roh mtakatifu ndani mwakoaw kiongozi wako..ukiwa unasali mkumbushe MUNGU akusaidie kwenye NDOA yako sina mengi usikuu huu

  NAWATAKIA WOTE NDOA NJEMA ZENYE FURAHA NA AMANI,,BARAKA ZIKIWA ZIMEJAA NA KUSHINDWA MAHALI PA KUWEKEA USIKU/ASBH/MCHANA MWEMA WOTE
   
 7. Mbonea

  Mbonea JF-Expert Member

  #7
  Nov 10, 2009
  Joined: Jul 14, 2009
  Messages: 640
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kwa kweli Mungu anaitajika kwa hili.
   
Loading...