AfroIT inahitaji maoni yako

Kilongwe

JF-Expert Member
Feb 7, 2008
423
114
Kwa original post,tembelea Hapa

Walenga walisema polepole ndio mwendo,siku zote mwenye subira basi hujiwa na heri.AfroIT tangu uzinduzi wake hadi leo hii tuna muda wa mwaka mmoja.Kwani mnamo Sep 2009 tuliizindua AfroIT forums kama ni kijiwe cha wana ICT ambapo lengo lilikuwa ni kupashana habari,kubadilishana maarifa ya ICT na pia kutatua matatizo ya ICT pale yanapojiri kwani forums inajumuisha wanajamii kedekede ambao wamejikita ipasavyo kwenye hii fani.

Tangu uzinduzi wa forums pale 2009 hadi tukaja na website kamili ya AfroIT Tech Suite mnamo Juni 2010,tumekuwa tukikabiliana na changamoto nyingi ambapo tumejitahidi kuziruka hadi kufikia hapa tulipo,changamoto hizi ni kama

Matumizi ya lugha.


Lengo kubwa la AfroIT ni kuihalisisha ICT,hapa tunamaanisha kufikisha elimu husika kwa jamii husika ya kitanzania,sisi kama AfroIT lengo letu ni siku ya mwisho kuwa ni chombo kinachotegemewa kwenye masuala ya ICT kwa Tanzania na Afrika ya mashariki kwa ujumla.Hivyo lugha kuu ya AfroIT ni kiswahili.Ila changamoto ambayo tunayo ni jinsi ya kufikisha maarifa kwa kutumia lugha hii.Kazi bado inaendelea na hadi tutakapomaliza phase ya tatu ni imani kuwa AfroIT yote itakuwa ni ya kiswahili na kila kitu kitakuwa kwa kiswahili na kwa jamii yetu.

Ufahamikaji


Njia kadha wa kadha zimetumika katika kujitangaza ili kuhakikisha kila mtanzania mwenye uwezo wa kutumia Internet anafahamu kuwa AfroIT ni kitovu cha matatizo yake.Kwani AfroIT ni jamii ya ICT ikishirikisha mimi na wewe.Harakati kadhaa bado ziinaendelea ili kuhakikisha jamii inafahamu zaidi uwepo wa AfroIT na kufahamu matumizi na faida za kutumia AfroIT.


Michango ya kiufundi

Hapa ndio utata mkubwa ambao tumekuwa tukikumbana nao,kwani jamii yetu wataalam wengi wa ICT hawapo tayari kushirikiana au kuchangia ufahamu wao.Ukweli ni kuwa hata Roma haikujengwa kwa siku moja na hakuna mtu aliye kamilika,hivyomichango ya niini unafahamu au nini nimekosea na kunielimisha kiufasaha ni muhimu mno.Tumekuwa tukipokea michango hafifu mno toka kwa wana ICT wa kitanzania.Wengi wamesema kuwa ni ngumu kutokana na lugha,mazingira au hata kutokana na teknolojia.Ukweli uunabaki palepale sisi kama wana ICT ni jukumu letu kutumia maairifa tulio nayo hata kwa uchache wake kuifikishia jamii.Kuna wakati kidogo unachokijua wewe ni gunia kwa mwenzako,hivyo juhudi bado zinaendelea kuhakikisha tunashirikiana na wadau ili kuongeza makala za teknolojia za kiswahili.Vilevile kuna baadhi wamezania kuwa jukumu la kuchangia mada ni la timu ya AfroIT pekee,ukweli ni kuwa AfroIT ni ya jamii nzima na sisi kama timu jukumu letu ni kuandaa mazingira mazuri ya ushirikiano wa wanajamii kwenye ICT.


Ukiondoa changamoto ambazo tumekumbana nazo,pia tumepata mafanikio ambayo yanatupa moyo sisi wapenda ICT na jamii kwa upana wake,mafanikio hayo ni kama ifuatavyo:

Kukua kwa timu ya AfroIT

AfroIT imeweza kutanua wigo wake kwa kuongeza timu yake,mnamo 2009 AfroIT ilianza ikiwa na mtu mmoja ambapo hadi leo tuna timu ya watu kumi,pia milango bado ipo wazi kukaribisha vipaji mbalimbali vya kitanzania ambavyo kwa njia moja au nyingine wapo tayari kushirikiana nasi katika kuhakikisha tunasonga mbele.Wakina dada na akina mama tunawakaribisha kwa mikono mikunjufu kabisa kujiunga na timu ya AfroIT.
timu(1).jpg


Ushirikiano

Tunashukuru ushirikiano tulioupata toka kwa jamii,wamiliki wa tovuti mbalimbali na wamiliki wa blog ambao kwa njia moja au nyingine wameonesha ushirikiano nasi,siwezi kuzitaja zote ila shukurani za pekee ziwaendee kwa wamiliki wa Jamiiforums,Michuzi blog,Jiachie Blog,Haki Ngowi blog,Mwendo mdudndo website,Lady Jay Dee blog,Mt Kilimanjaro blog,ICT-Pub blog, na wengine ambao sio rahisi kuwaorodhesha kwa ushirikiano wao ambapo hawakusita kwa njia moja au nyingine kuweka makala mbalimbali za ICT toka AfroIT.

Watumiaji


Ingawa idadi ya wadau wanaotembelea AfroIT haijafikia malengo yetu,ila hadi sasa tumepiga hatua kubwa kwani tumeweza kupata watembeleaji wa wastani wa mia mbili hadi tatu kwa siku,kitu cha muhimu zaidi ni kuwa wadau hao wametokea nchi mbalimbali duniani kama inavyoonekana kwenye picha.Hii sio tuu kwa watembeleaji wapya bali pia wanaorudikwa mara kadhaa(returning visitors) na huku muda wanaotumia kwenye tovuti yetu umekuwa toka wastani wa sekunde 50 pale mwaka 2009 hadi dakika 3:46 kwa wiki hii.Hii ni hatua nzuri kwa tovuti za Teknolojia mabapo sio wengi wamekuwa wakitembelea.Vilevile tumefanikiwa kupunguza watumiaji wanaoboreka na kuondoka(bouncing rate) toka asilimia 50% hadi 15% huku tukipunguza uwiano wa watembeleaji wapya kwa wa zamani toka 80% hadi 50.5% kitu kinachoonesha utashi wa watembeleaji(Visitor loyalty) imeongezeka.

afroit2(1).jpgMipango ya baadae.


Kama tulivyoelezea katika Mission na Vission zetu,lengo kubwa la AfroIT ni kuwa kitivo cha teknolojia kwa Tanzania na Afrika kwa ujumla,hivyo kwa sasa tunajiandaa na mambo yafuatayo:

1.Kutanua wigo Zaidi


BD_iLoveIT.jpg
Lengo la AfroIT ni kuiwezesha jamii husika,hivyo tupo kwenye mchakato ambapo tutashirikiana na wadau,vyuo,mashule na hata vituo vinavyotoa maarifa mbalimbali.Tunatarajia kuzindua AfroIT Club ambayo itakuwa na matawi kwenye Vyuo vyote na mashule,pia hata makazini kwa wale wapendao ICT.Lengo la kuingia mashuleni ni kuhakikisha vijana wanaandaliwa vizuri kwenye masuala ya ICT huku tukiongeza au kutia chachu upenzi wa hii fani ambayo ni muhimu kwa maendeleo ya taifa letu la Tanzania.Ndani ya hizo club kutakuwa na mambo mengi mno yanayohusu ICT,mkazo mkubwa umewekwa katika kuhakikisha tunaifikia jamii kikamilifu.Hivyo kama hili litafanikiwa tutakuwa tumeifikia jamii zaidi na kushirikisha wadau wengi zaidi ambapo itasaidia kuifikia na kuiwezesha jamii zaidi.Kauli mbiu yetu itakuwa ICT na mimi.


2.Kuimarisha zaidi huduma yetu ya online(Phase III)


Tupo katika mchakato wa maandalizi ya kuja na phase ya III ya tovuti ya AfroIT ambapo tunatarajia kuigeuza(transform) AfroIT kuwa platform ambayo itakuwa na kila kitu kinachohusu ICT huku tukitilia mkazo zaidi uhalisishaji wa hii ICT ili iendane na mazingira na jamii ya kitanzania.Awamu hii itakuja na teknolojia kubwa zaidi ambapo ni dhahiri itakuwa ni mkombozi wa Tanzania na Afrika ya mashariki kwa ujumla.Michango na maoni zaidi yanapokelewa juu ya ni jinsi gani tutaweza kuifanya iwe na manufaa kwa jamii husika.Kwenye hatua hii tarajia kujionea mambo mengi sana ya tekinolojia ndani ya AfroIT ambayo wengi wetu tumekuwa tukitarajia au kuwaza juu ya kitu kama hiki.Ndani ya phase III tutawagusa sana madeveloper,wanafunzi,wanajamii,waajiri na mageek halisia wa kitanzania.

3.Makazi ya kudumu(ofisi)


Hadi sasa,AfroIT imekuwa ikifanya kazi zake zote online,hii imepelekea baadhi ya wadau kupata usumbufu pia kutoweza kufikia malengo kwa ufanisi,Hivyo tunaandaa makazi ya kudumu ya AfroIT kwenye baadhi ya miji nyumbani Tanzania.Matayarisho yakikamilika basi tutawaeleza ni jinsi gani munaweza kutupata AfroIT.Hii itaendana na mpango namba 1 hapo juu.

Mchango wa jamii.


changia.jpg
Ukweli ni kuwa maendeleo ya Tanzania yataletwa na watanzania wenyewe pale watakapoamua kujitolea kwa hali na mali katika kuijenga nchi yao.Hivyo sisi kama wanajamii wa kitanzania tumeonesha moyo wa kuwa tunaweza na sasa wewe kama mwana jamii mchango wako ni muhimu katika kuhakikisha malengo,dhamira na utashi wa AfroIT hauishii hewani kwa kukosa ushirikiano.
Je wewe mwanajamii una mawazo,maoni,maono,mchango au ushauri gani kwa AfroIT katika kuhakikisha tunafikia malengo? Zingatia mchango wako unaweza kuwa juu ya huduma zinazotolea kwa sasa,tunazotarajia kuzitoa au ambazo hatujaziorodhesha ila wewe unaona kama zitakuwepo zinaweza kuwa na mchango kwa jamii.
Tuandikie kwa kuacha maoni chini ya mada hii au kutuma kwenda kwenye anuani zifuatazo: E mail- webmaster@afroit.com Simu: +255779216010
AfroIT
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom