Afrika tunapenda kulialia/kulalamika sana

Abu Ubaidah Commando

JF-Expert Member
Sep 8, 2016
7,593
6,934
Ingelikua utajiri unaupata kwa kulialia, kulalamika na kutaka huruma basi Afrika, hususani hapa Bongo/Afrika ingeongoza kwa utajiri kuliko taifa/bara lolote duniani.

Point yangu ni hiii👇🏽
Kwa waliotazama mpira wa jana

Jana zimecheza timu 4
Al ahly tripoli na Orlando pirates
Berkane na Mazembe

Mpira ulimalizika,
Orlando ndani, tripoli nje kwa goli 3-2
Berkane ndani, Mazembe nje kwa goli 4-2

Nimefuatilia mitandaoni wadau wa michezo wakilalamikia ushindi wa Berkane dhidi ya mazembe, kwa mtu anaejua mpira hawezi kulialia na kulalamika eti Berkane wamebebwa, haingii akilini kwa mtu anaejua mpira akadai mazembe wameonewa.

Naamini asilimia 90 ama zaidi ya hiyo walikua wanatamani mazembe ashinde, na hao hao ndio wanalialia na kulalamika mara oh waarabu matapeli, figisu, fitina, refa amehongwa, mara oh ile sio red card, ile sio penalt, wengine wanawatukana waarabu kisa tu mazembe ametolewa.

Kama wamebebwa, je! Huyo mazembe alishindwaje kumfunga hizo goli 4 kwake!!! Badala yake akaishia na ushindi wa goli MOJA!!! mnadhani Berkane ni timu ndogo!!! Fuatilieni historia yake hapo nyuma ndio mtajua Berkane ni nani, Pesa pesa pesa ndio kila kitu.

Naamini kabisa ushindi wa jana kwa Berkane, lau ingelikua ndio mazembe ameshinda hizo goli 4, na mchezaji wa berkane amepata red card, na kupata penati msingekuja hapa kulialia na kulalamika wameonewa, labda wachache sana wanaoelewa na kutambua nini maana ya mpira.

Mechi ya Orlando na Tripoli sijaicheki, ila nimejaribu kupitia comments za wadau, tena ni wachache sana wakidai kuwa tripoli amenyimwa penati MBILI dhidi ya Orlando. Wadau hawa hawazidi 10, na sijaona kutukanwa kwa ORLANDO.

Lakinii, timu za wenzetu(NORTH AFRIKA) zikipata ushindi kelele nyingi sana, mara wanabebwa, marefa wanahongwa, hapo miaka ya nyuma walikua wanalalamika sana kuhusu ushindi wa Al ahly/Egypt eti kwakua RAIS WA CAF alikua ni mwarabu ndio maana, haya na sasa RAIS wa sasa tulienae ni Mwafrika na bado malalamishi yako pale pale.

Kwa wale mliotazama mechi ya Egypt na senegal mliona nini kilitokea ni wazi egypt alifanyiwa uhuni, mechi ya Algeria dhidi ya Cameroon ni wazi Algeria alifanyiwa uhuni, lakini huwezi kukuta wadau wakitukana na kulalamikia timu za waarabu zinaonewa, labda wachache sana sana. Sisapoti kutukana, kudhania n.k.

Kuweni wanaume bwana, wanaume wa shoka na tuacheni kulalamika na kujilizaliza, mpira haupo hivyo, wenzetu ndio maana wamefika mbali.

👇🏽
NO TO RACISM

(UBAGUZI WA RANGI BADO UNALITIKISA BARA LETU KULIKO JAMII/BARA LOLOTE HAPA DUNIANI) HUSUSANI HAPA KWETU BONGO, ILA WACHACHE WANAJITAMBUA👈🏾 WATU HAWA KWANGU NAWAPA KONGOLE.


Nawaombeni tuchangie kwa ustaarabu na sio kutukana, kukejeliana n.k.

Ahsanteni!
 
Yaani wewe jamaa huwa hujishtukii .

Wewe hao waarabu ulisemaga ni ndugu zako kiimani kwahiyo hatushangai kuwatetea hovyo..

Mechi ile ilikuwa ni aibu na rushwa ya wazi wazi hasa ile red.soze wa mazembe alianza kugusa mpira yeye bado akala umeme..!

Hsta kule afcon ulikuwa upo team za waarabu na uzuri zikafumuliwa ukawa unalia wameonewa..!

Haya vipi kuhusu tochi kipa wa mazembe alizokuwa anamulikwa au wakimulikwa wengine sawa? Ila waarabu wakifanyiwa unasema uhuni..!

Tumechoshwa na hao waarabu wako sijui wamekupa nini?
 
Yaani wewe jamaa huwa hujishtukii .
Wewe hao waarabu ulisemaga ni ndugu zako kiimani kwahiyo hatushangai kuwatetea hovyo....
Hii mada inahusu mpira, ila wewe umeanza kuingiza udini.

Rushwa ya wazi👉🏽 unaweza thibitisha?

Yah kule afcon nilikua timu za waarabu, kwa sababu wanajua mpira. Tusipangiane cha kushabikia, sawa kijana!

Kuhusu tochi wameingianazo sawaa, lakini hazikuleta madhara na hawakua serious kwa kipa na hata kwa wachezaji wenyewe, tofauti na ilivyokua kwa senegal dhidi ya egypt uonevu wa wazi haswaa.

Umechoshwa na hao waarabu eti, endelea kuchoshwa zaidi mpaka basi, anaeumia ni wewe mwenye chuki. Pole sana

Acha ubaguzi, na kemea ubaguzi.
 
Hii mada inahusu mpira, ila wewe umeanza kuingiza udini.

Rushwa ya wazi👉🏽 unaweza thibitisha...
Tangu mwanzo umekazana walifanyiwa uhuni hebu orodhesha kama nilivyosema swala la tochi, wewe umekazana uhuni,uhuni upi huo?

Basi kumbe kama unajua tusipangiane basi why unatulazimisha tuamini maoni yako?
Basi mimi nasema waarabu hawajui mpira utanilazimisha? Tusipangiane..!

Wewe tunakujua na udini wako wa kishamba ,dunia imebadilika hii hakuna zama za utumwa wa waarabu ambao bado unao kichwani,pia hata ukoloni wa wazungu haupo hapa ila wewe unao.

Nakuona tangu siku nyingi, unataka kusema waarabu ni superior wakifungwa basi wamefanyiwa uhuni, ila wakishinda wao ni sawa..?

Ok twende wakipiga wenzao tochi unadai hazina madhara!😂😂

Lakini wao wakipigwa tochi hivyo hivyo unadai wameonewa na uhuni wamefanyiwa!🤣🤣🤣

Kaa na kichwa chako ndugu mimi nimemaliza..!
 
Tangu mwanzo umekazana walifanyiwa uhuni hebu orodhesha kama nilivyosema swala la tochi, wewe umekazana uhuni,uhuni upi huo...

Waarabu wakishinda figisu
Waafrika wakishinda sio figisu

Waarabu wakishindwa sio figisu
Waafrika wakishindwa figisu 🤣🤣 ndio maana soka letu haliendelei, kelele nyingi vitendo zero.

Suala la ubaguzi limeshapitwa na wakati mkuu.

Kemea ubaguzi.
 
Back
Top Bottom