Afrika tuna ubinafsi na mentality, shida sio wazungu

Aaron Arsenal

JF-Expert Member
Jul 24, 2014
24,504
28,691
Mentality ni nini kwa Kiswahili? "Ni njia ya kufikiria ya mtu au kikundi."

Hivyo katika watu ambao tuna shida ya "mentality" ni watu Weusi na Waarabu. Jamii hizi kwa asilimi kubwa zinaishi kwa itikadi sana hasa ya dini. Jamii hizi daima zinarusha lawama zake kwa watu wa magharibi, kila tatizo au migogoro ya kiuchumi nk ni kulalamika tu. Nimeudhuria sana mijadala ya watu weusi na Waarabu kuhusu maisha ya kiujumla ila nimeona mzungu ndio ameshushiwa zigo la lawama.

Lakini ukifuatilia sana kwa makini utaona jamii yetu ya Weusi pamoja na Waarabu ni wabinafsi mno na wote wanasali sana lakini ni wachoyo sana. Wao ni kupokea tu na si kutoa. Nchi zetu za Afrika na za Kiarabu zinapokea sana fedha kutoka Ulaya na Marekani lakini ndio wa kwanza kuwalalamikia hao hao katika shida zao. Hebu tuone jambo hili.

Mnamo mwaka 2015, Amerika ilitoa zaidi ya dola bilioni 8 kusaidia nchi 47 za Kusini mwa Sahara; na USAID inaboresha kanda 27 za nchi za barani Afrika. Na toka 2015 mpaka 2019 misaada inaongezeka. Hapo sijataja nchi za Ulaya.

Na nchi za Kiarabu ndio zinaongoza kupokea misaada kutoka Marekani nchi kama Afghanstan, Jordan, Misri, Palestina, Iraq nk. Afghanistan inapokea $ 4,533.51 milioni katika misaada ya kigeni ya Amerika ambayo ni kama $ 148 kwa kila mtu.

Hiyo ni misaada tu bado mikopo, Afrika tumekopa sana kiasi nchi zingine zimeshafikia mstari mwekundu wa kukopa, hazikopesheki sasa. Ukiwaza hizo pesa zinaenda wapi utastajabu sana, ndizo utasikia eti ndio zimekuwa "EPA" yaani watu walikula na familia zao, na wanabeba kwa magunia na kujiita vigogo, halafu hilo deni anabebeshwa muuza Nyanya na muuza dagaa. Halafu utakuta watu fulani tena wanajiita wasomi wanatetea upuuzi huu na kutoa oyeee, na viongozi wa dini bila hiyana nao wanaunga mkono asasi ambazo zimefanya ufisadi huu.

Huo ni ubinafsi mkubwa na laana nzito, tusitegemee Mungu atazibariki nchi kama hizi, bila kubadilisha mentality tutaendelea kulalamika mpaka Yesu atakuja. Vijiweni na mabungeni utasikia mabeberu wanatunyonya, kwani walikushikia panga au bunduki na kukulazimisha kukopa kwao? au walikushinikiza kufanya mikataba ya hovyo ukiwa guest? na kama wanakukera mbona unapokea misaada kutoka kwao? kataa basi kama una njia mbadala.

Taifa halifanikiwi kwa kuwa na chama cha siasa chenye nguvu, au kuwa na jeshi bora lenye silaha kali ama kuwa na raisi bora kiasi cha watu kuomba aendelee kutawala kinyume cha katiba, bali taifa linafanikiwa kwa kuitamka HAKI NA KUITENDA. Biblia inasema hivi,

"Haki huinua taifa...[Mithali 14:34]."

Na usitegemee hata mara moja nchi itabarikiwa kwa kuonea maskini, maskini ambao nguvu ndio mtaji wao, unamwekea kodi kuu, kiasi cha kulia usiku na mchana. Mtaji wa laki moja unaliwa kwa kodi mpaka unateteketea, kodi zisizo zingatia utu na kumuinua mjasiliamali mdogo, halafu na hizo hizo pesa za kodi zinapelekwa kwenye siasa au kwenye mambo ya hovyo. Lazima mlaaniwe tu. Nabii Daniel alimwashauri hivi mfalme mkuu mwonevu wa maskini na mkanyaga haki,

"Kwa sababu hiyo, Ee mfalme, shauri langu lipate kibali kwako; ukaache dhambi zako kwa kutenda haki, ukaache maovu yako kwa kuwahurumia maskini; huenda ukapata kuzidishiwa siku zako za kukaa raha. [Dan 4:27]."

Mfalme huyo alipuuza ushauri huo wa Daniel, lakini matokeo yake alipinduliwa na raia wake. Ushauri huo mpaka sasa unawafaa viongozi wote, kiongozi muovu ambaye anakanyaga haki na kuonea maskini kwa kodi na kutwaa haki zao, uiletea nchi matatizo na laana. Pia ukionea wafanyakazi na kuwadhulumu stahiki zao, tambua unaleta mabalaa katika nchi. Biblia inasema,

Ole wake aijengaye nyumba yake kwa uovu! Na vyumba vyake kwa udhalimu! Atumiaye utumishi wa mwenzake bila ujira, Wala hampi mshahara wake; [Yeremia 22:13].

Huwezi kuijenga nchi kwa dhuluma ya haki za wafanyakazi na nchi hiyo ikafanikiwa. Pia kuwadhulumu wakulima haki zao za ukulima, ni kumuuzi Mungu, na Mungu analipa. Biblia inasema,

"Angalieni, ujira wa wakulima waliovuna mashamba yenu, ninyi mliouzuia kwa hila, unapiga kelele, na vilio vyao waliovuna vimeingia masikioni mwa Bwana wa majeshi. [Yakobo 5:4]."

Hizo dhuluma zote utazikuta Afrika ni mwendo wa ufisadi na kung'ang'ania madaraka, Mungu haziakiwi apandacho mtu ndicho atakachokivuna. Lawama hazitatupigisha hatua kamwe. Adam baada ya kutenda dhambi kwa kula tunda, alivyo hojiwa na Mungu, lawama zote alimtishwa mkewe kuwa ndio kamsababisha kula tunda. Kwa maana nyingine alimwambia Mungu usingenipa huyu mwanamke au nisingekuwa na huyu mwanamke nisingetenda dhambi.

Mungu halimhukumu ADAM bila kusikiliza hizo sababu za kijinga na kumpa adhabu ambayo mpaka leo tunapitia machungu ya uchaguzi wake. Ndivyo ilivyo Afrika, ikiulizwa kwanini huko kwenu kumejaa umaskini mkubwa na uonevu? inajibu ni kwa sababu ya MZUNGU [BEBERU]. Maovu yetu tunayaficha kwa uvuli wa neno Beberu/ mzungu. Mungu atahukumu Afrika kwa uchaguzi wao mbovu na si kwasababu ya udhuru wa BEBERU.

Tubadilishe mtazamo wa fikra.

FB_IMG_1589345607012.jpeg
 
Ubinafsi chanzo chake ni ujinga.

Viongozi ujifikiria wao kwanza na sio walipa Kodi,

Mtaani mtu akipata pa yeye kuingia uziba njia hajali kuhusu jirani zake
 
Nadharia za kuwalaumu wazungu au mabeberu juu ya kushindwa kwa watawala wa kiafrica ziliasisiwa na wajamaa Kama kina Nyerere, Walter Rodney nk Kama sehemu ya kufichia udhaifu wao wa kushindwa kuleta mabadiliko chanya kwenye Jamii kwa kushift mzigo wa kushindwa hii falsafa ikaenezwa kwa watawaliwa wakiaminishwa ya kwamba matatizo yao yamesababishwa na external factors.

Ni Kama watawala wa kiafrica na kiarabu kuwaatupia lawama wazungu ili wananchi wao wasielewe wao ndio wasabibishi wa matatizo ya wananchi.

Mfumo wa ujamaa huwa hautoi majibu ya kutatua tatizo Bali umekazia kulaumu tatizo.

Kama kutawaliwa ni chanzo cha umasikini wetu miaka 60 sasa Africa iko huru kwann isiendelee Sasa.Unakopa unawekeza kwenye elephant project,unakopa unatumia kupambana na upinzani badala ya umasikini,unakopa unajenga makasri ( zuma, Mugabe,mobutu,),unakopa mnauwana kwa Vita Sasa hapa mzungu anahusika vipi,mbona wao awapigani hovyo.

Maana chanzo cha Vita Africa na uarabuni ni sababu ya udikteta.Sasa mzungu ndo kakwambia uwe dikteta.Sisi Kama sisi tujilaumu wenyewe juu ya kushindwa kwetu tusitafute wachawi.Wachawi ni mentality zetu
 
Umasikini wa Africa umetokana na internal factors na sio external factors Kama tulivodanganywa na kina Walter Rodney ( how Europe underdeveloped Africa).Key internal factors ni ukosefu wa mfumo Bora wa uongozi, ubinafsi ( mentality),rushwa na ufisadi ( high-level of selfness),uvivu,uwazi (demokrasia).Tutaendelea siku hivi visipokuwepo
 
Right engine+right fuel=success.

truth hurts ila lazima ukweli usemwe na huo ndo ukwel,nchi za Africa kiukweli tumekosa watu makini ambao wanaweza kuthink wisely kwa ajil ya watu wao sio kwa ajili ya wao Binafsi na familia zao.

Siku tukipata watu sahihi+katiba/policies nzuri=mafanikio.
 
Right engine+right fuel=success.

truth hurts ila lazima ukweli usemwe na huo ndo ukwel,nchi za Africa kiukweli tumekosa watu makini ambao wanaweza kuthink wisely kwa ajil ya watu wao sio kwa ajili ya wao Binafsi na familia zao.

Siku tukipata watu sahihi+katiba/policies nzuri=mafanikio.
Viongozi wabovu ni zao la Jamii mbovu.Mfumo mfu wa uongozi Africa unazalisha watawala na sio viongozi
 
Ni mjinga peke yake anayeamini matatizo ya mwafrika yamesababishwa na wazungu.Mambo mengine yako wazi sana kuhusu uwezo wetu wakufikiri na kutenda. ujinga ni mwingi na umetamalaki kwahiyo sababu yakushindwa kwetu ndicho kinachopelekea kutupia wazungu lawama.
 
Jamii hizi daima zinarusha lawama zake kwa watu wa magharibi, kila tatizo au migogoro ya kiuchumi nk ni kulalamika tu. Nimeudhuria sana mijadala ya watu weusi na Waarabu kuhusu maisha ya kiujumla ila nimeona mzungu ndio ameshushiwa zigo la lawama.
--------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------
Vijiweni na mabungeni utasikia mabeberu wanatunyonya, kwani walikushikia panga au bunduki na kukulazimisha kukopa kwao? au walikushinikiza kufanya mikataba ya hovyo ukiwa guest?
Nakubaliana na wewe kwa kiasi kikubwa. Nimenukuu hizo paragraph mbili ili wavivu wa kusoma angalau wapate mwangaza wa kilichomo
 
Ukimuona mtu au kiongozi anawalaumu mabeberu juu ya kushindwa kwake huna shaka juu ya upeo wake.Huyo ni sawa na mabus ya mwendokasi wamepewa kila kitu yaani kila kitu kuanzia njia,ruti,abiria,magari, monopoly,vituo lkn hawawezi.Viongozi wa kiafrica ni sawa na mabus ya mwendokasi.Itakuwa ni ajabu mwendokasi kuwalaumu daladala juu ya kushindwa kwao
 
Umasikini wa Africa umetokana na internal factors na sio external factors Kama tulivodanganywa na kina Walter Rodney ( how Europe underdeveloped Africa).Key internal factors ni ukosefu wa mfumo Bora wa uongozi, ubinafsi ( mentality),rushwa na ufisadi ( high-level of selfness),uvivu,uwazi (demokrasia).Tutaendelea siku hivi visipokuwepo
Dah una akili kubwa sana, watu kama nyie humu jf mmekuwa adimu wamebaki watukanaji tu
 
Back
Top Bottom