Afrika ni bara la misiba na ni chanzo kikubwa cha umaskini

hazole1

JF-Expert Member
Jan 3, 2015
4,319
3,911
Nikipiga hesabu wakati mwingine unakuta katika wiki siku mbili ndio nimefanya kazi siku zote nimeshinda misibani na nikipiga hesabu wakati mwingine sisi watu wa mjini ndio tunahangaika sana na misiba na tunapoteza pesa nyingi sana unakuta sometime mnasafiri kwenda mbali sana kuzika na mnapita katika mazingira magumu na usafiri washida mnaning'inia kwenye mafuso na sometime unakuta hata sio ndugu ila mlikua mnafahamiana au mlikua mnakaa nae mtaa mmoja.

Na kupitia mazingira magumu na kutumia usafiri mbovu wa kubeba watu kwenye mafuso imeweza kusababisha msiba juu ya misiba wengi wamepoteza maisha kwa kupitia huu mfumo sasa hiyo imekua ni hasara kubwa kubwa kwa taifa na hii wakati mwingine inaonyesha waafrika ni kiasi gani hatuna akili na ni wavivu kufikiria.

Kuanzian na mimi na watanzaia wote kwa ujumla hili swala inabidi tulifikile upya kwa mapana na marefu najua sisi wote tutakufa na lazima tuzikane lakini tuangale tunazikanaje na swala la kwenda na muda na tuangalie wenzetu wazungu wanafanyaje nakumbuka nilishaangaliaga msiba mmoja wa kizungu niliona watu nane tu msibani nasisi tubadilishe mfumo wetu wa jinsi ya kuzikana kama itawezekana.
 
Tatito sio akili au kutofikiria sisi ni wa-Afrika mila na desturi zetu zipo so communal,kwahiyo kubadilisha hiyo kitu si kazi rahisi kuliko unavyodhani halafu si lazima kila kitu tuwe sana na wazungu despite merits or demerits. Differences is what make us,tukienda uzunguni tukute hivi au vile kadhalika uchinani,uhindini na kote.
 
Nikipiga hesabu wakati mwingine unakuta katika wiki siku mbili ndio nimefanya kazi siku zote nimeshinda misibani
Na nikipiga hesabu wakati mwingine sisi watu wa mjini ndio tunahangaika sana na misiba na tunapoteza pesa nyingi sana unakuta sometime mnasafiri kwenda mbali sana kuzika na mnapita ktk mazingira magumu na usafiri washida mnaning'inia kwenye mafuso na sometime unakuta hata sio ndugu ila mlikua mnafahamiana au mlikua mnkaa nae mtaa mmoja

Na kupitia mazingira magumu na kutumia usafiri mbovu wa kubeba watu kwenye mafuso
Imeweza kusababisha msiba juu ya misiba wengi wamepoteza maisha kwa kupitia huu mfumo sasa hiyo imekua ni hasara kubwa kubwa kwa taifa na hii wakati mwingine inaonyesha waafrika ni kiasi gani hatuna akili na ni wavivu kufikiria


Kuanzian na mimi na watanzaia wote kwa ujumla hili swala inabidi tulifikile upya kwa mapana na marefu najua sisi wote tutakufa na lazima tuzikane lakini tuangale tunazikanaje na swala la kwenda na muda na tuangalie wenzetu wazungu wanafanyaje nakumbuka nilishaangaliaga msiba mmoja wa kizungu niliona watu nane tu msibani nasisi tubadilishe mfumo wetu wa jinsi ya kuzikana kama itawezekana.

Umeanza vizuuurii ila humo kwenye wekundu ndo umevurunda Jombaa!!kwanza kabisa umenidhalilisha mimi binafsi na waafrika wengine ambao wana akili timamu na ni wazuri katika kufikiria kuliko hata wewe!!Rafiki, unapoongelea jambo kama hujafanya utafiti usijumuishe hata siku moja,wewe ongelea kile ulichokifanyia utafiti,huwezi nambia umefanyia utafiti waafrika wote na umegundua kuwa hawana akili na ni wavivu kufikiria.Tatizo tulilonalo waafrika ni mfumo tunaoishi ambao"WENYE MAMLAKA HAWANA MAWAZO NA WENYE MAWAZO HAWANA MAMLAKA" HIVYO FUTA KAULI YAKO NA UTUOMBE RADHI!!
Kitu kingine utambue kuwa sisi ni waafrika tuna mila na tamaduni zetu hivyo hatuwezi kuishi kama wazungu msiba kuwa na watu nane au milioni sio hoja,hoja ni kwamba utamaduni wetu waafrika upo katika mfumo wa ushirikiano kijamii zaidi,hivyo tunashirikiana katika mambo tofauti ya shida na raha,ukweli ni kwamba kama umebahatika kwenda ulaya,wazungu wengi wanaishi maisha ya kipweke sana sio kama sisi waafrika tunaushirikiano mkubwa sana.Hivyo cha msingi uangalie msiba upi una kuhusu na upi haukuhusu,utakuwa mtu wa ajabu sana kama utakuwa unahudhuria kila msiba.HIVYO UNAPOTUMA POST YAKO HEBU NA WEWE JARIBU KUFIKIRIA KABLA HUJAITUMA!
 
Mbalamwezi

Na hicho ndio kitu kinacho mchelewesha muafrika ni mgumu sana kuukubali ukweli na kujaribu kuufanyia utafiti.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu umesema kwamba sisi watu wa mjini ndiyo tunaohangaika zaidi na misiba. Kwa mawazo yangu mimi naona watu wanaoishi kule vijijini ndiyo wanaoumia zaidi na misiba kuliko tulioko huku mjini. Hii ni kutokana na ukweli kwamba kule vijijini ndiko watu wengi walio ndugu wanakoishi kwa wingi zaidi pia kuna mshikamano mkubwa zaidi kati ya ndugu na ndugu na pia kati ya majirani na majirani. Pia kutokana na mazingira yaliyopo ni rahisi kwa watu ndugu au majirani kufahamiana kwa undani hata kama wanaishi katika vijiji mbalimbali. Katika hali hiyo uwalazimu kuhudhuria karibu kila msiba wa ndugu na majirani na hata wakati mwingine usafiri kwa miguu au baiskeli tena umbali mrefu.

Yaani kwa kule vijijini mimi uwa naona watu wanapoondoka kwenye msiba mmoja ni kama vile uwa wanarudi majumbani mwao kutafuta nauli ili kujiandaa na safari nyingine kuelekea kwenye msiba mwingine mpya kwani kwa kweli uwa hawatulii sana kabla ya kupata taarifa ya msiba mwingine ambao watalazimika kuhudhuria.

Binafsi nimeshuhudia watu wengi huko vijijini wakihudhuria misiba na wakati wa kutaka kurudi majumbani mwao wanakuwa hawana hata nauli. Hata nauli za kuijia msibani mara nyingi wanakuwa wamekopa.Kwa hiyo kwa mtazamo huo unaozingatia mshikamano uliopo vijijini kwenye mambo ya misiba, ukaribu (undugu au ujirani), hofu ya kutengwa usipohudhuria msibani, kiu ya kujuana na ndugu wapya misibani, matatizo ya kiuchumi kwa wahudhuriaji wa misiba (nauli,michango n.k) umbali mrefu na ubovu wa miundo mbinu huko vijijini ni sehemu ya changamoto zinazoweza kuthibitisha kwamba watu wa vijijini ndiyo wanaoteseka zaidi na misiba kuliko sisi tulio mjini.
 
Back
Top Bottom