Afrika naona tunadhulumiwa na kubaguliwa

Namtih58

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
235
46
Kila mwaka nazidi kuona ubaguzi wa aina fulani Jumuiya ya Kimataifa.

Endapo shida iko afrika, Jumuiya ya Kimataifa inajikokota kuyapeleka majeshi/msaada. Siasa zinazidi kwenye mikutano yao, lakini wana collect data kweli ya walokandamizwa, walouwawa .......

Basi ngonja mizozo itokee kwingine, majeshi karibia yote yanamwagwa.
La kushangaza ni kuwa hata nchi za Afrika zinachangia, lakini ikifika ni kuchangia hapa kwetu AU, basi viongozi wote utadhani wamepotelea mvunguni.

Je ni mimi au kuna wengine wenye maoni kama yangu?
 
Hakuna mtu mwenye wajibu wa kuisaidia Afrika bali waafrika wenyewe, kwa hiyo kama hatusaidiwi ni nafasi yetu kujitutumua wenyewe.

Hii entitlement culture ndiyo inatufanya tuwe ombaomba daims. Tunahitaji vingi, kimoja ni uongozi bora lakini isaada tunaweza kuendelea bila ya kuwa nayo, kama tuna uongozi bora na mipango mizuri.
 
Moja ya matatizo yanayofanya tuendelee kuonewa ni kuamini kuwa sababu ya kutoendelea kwetu ni kwakuwa tunaonewa/tunadhulumiwa!!!!!!!!
 
Moja ya matatizo yanayofanya tuendelee kuonewa ni kuamini kuwa sababu ya kutoendelea kwetu ni kwakuwa tunaonewa/tunadhulumiwa!!!!!!!!

Pengine sikujieleza vema.

Shida zilizoko Afrika ni mzigo wetu sisi waafrika wala siwalaumu wenzetu.
Kinacho nikera mimi, ni kwamba, kila mwaka tunachangia UN. Infact mara ya mwisho kuangalia ni mataifa tajiri ambayo hayakuwa yametimiza majukumu yao ya kuchangia Jumuiya ya Kimataifa.

Sasa ikiwa nitachangia Insurance, siku gari langu likipata ajali mbona wasinihudumie kwa kasi kama mwenzangu aliyechangia kama mimi.

Na wasipo nihudumia kama mwenzangu huko sikunibagua?
 
Mimi nadhani muda wakulaumu umoja wa mataifa au nchi nyingine duniani kwa matatizo ya Afrika ulipita 1999. As long as tunaendelea kualumu mtu mwengine kwa matatizo yetu tutabaki hivi hivi.
 
Ninachoona mimi ni kwamba muda wa kuonewa na kubaguliwa ulikuwa kipindi cha ukoloni,kwa hivi sasa naamini nchi zote za Afrika ziko huru.
Ila tatizo tulilonalo waafrika ni kwamba tumeukubali ukoloni mamboleo(ina maana katika mikusanyiko ya kujadili mambo yetu kama waafrika na kutoa maamuzi yetu wenyewe kulingana na mazingira yetu.Chaajabu tunakubali kutolewa maamuzi yetu na wageni na cha kusikitisha tunakubali natuna yasimamia kwa nguvu zote na yale yetu tunatupilia mbali)
Hivyo basi,na hawa wageni siku zote wanatumia sana akili kutuchanganya;ukweli ni kwamba hapendi kuona tunakuwa na maendeleo ya kweli na ustawi mzuri.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom