Afrika kuweni macho viongozi wa kuchaguliwa kidemokrasia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Afrika kuweni macho viongozi wa kuchaguliwa kidemokrasia

Discussion in 'International Forum' started by Dingswayo, Nov 12, 2011.

 1. Dingswayo

  Dingswayo JF-Expert Member

  #1
  Nov 12, 2011
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 4,011
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Waziri Mkuu wa Tunisia, Beji Caid el Sebsi, amesema ni lazima nchi za Afrika ziwe macho na viongozi wake wanaochaguliwa kidemokrasia kama kweli wanaendesha nchi zao kwa misingi ya kidemokrasia, kwa sababu uzoefu umeonyesha kwamba, wapo wanaoingia madarakani kama wanademokrasia lakini hubadilika na kuwa madikteta.

  Akifungua mkutano wa mwaka wa Taasisi ya Vyombo vya Habari vya Afrika na Viongozi (AMLF), mjini Tunis jana, alisema Tunisia iliongozwa na mtu mmoja kwa robo karne akiaminika kwamba ni kiongozi mzuri, lakini yaliyofanywa baada ya kutokea kwa mapinduzi ya nguvu ya umma, hadi leo wanastaajabu matatizo, ambayo ameyaacha nchini humo.

  Alisema ingawaje Tunisia ilikuwa ikipigiwa mfano kwa maendeleo miongoni mwa nchi za Afrika, ukweli ulio dhahiri kwa sasa ni kwamba, kuna maeneo mengi ya nchi hiyo yaliachwa nyuma sana, hakuna miundombinu na yamekuwa ni changamoto kubwa kwa serikali ya mpito.

  Hata hivyo, pamoja na kusifu hatua zinazopigwa nchini kwake kwa sasa kwa kuruhusu uhuru zaidi wa vyombo vya habari, alionya kwamba, si kila mapinduzi yanayotokea katika nchi yanahakikishia wananchi demokrasia na uhuru zaidi, kama juhudi za kweli za kutoa demokrasia kwa mwananchi hazitachukuliwa na serikali hasa kuhakikisha maendeleo yanafikia kila jamii.
  Alisema mapinduzi ni lazima yalenge kutoa nguvu kwa wananchi na kuwapo kwa utawala bora wa kidemokrasia, ambao utawahakikishia wananchi kuchagua viongozi wake.

  Alisema kwa mara ya kwanza katika historia ya Tunisia, Oktoba, mwaka huu, ulifanyika uchaguzi wa wabunge ulio huru na wa kidemokrasia, ambao ulisimamiwa na tume huru ya uchaguzi.

  Alitoa rai kwa mataifa mengine ya Afrika, kama Misri na Libya, ambayo yameshuhudia mapinduzi kama ya Tunisia, kutambua kuwa bila kufungua milango ya demokrasia na kuwapa watu uhuru na rasilimali zinazolenga kuwakomboa, mapinduzi yaliyofanyika hayatakuwa na maana.

  Kauli ya kuwawezesha wananchi pia ilitolewa na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Dk. Donald Kaberuka, ambaye alisema umaskini una msingi mmoja, kwamba, si tu ni kielelezo cha ukosefu wa raslimali, lakini pia unaelezwa katika kuwanyima wananchi uwezo wa kuhoji waliopewa madaraka, kuwawajibisha ili wafanye maamuzi yanayoleta maendeleo ya wote.

  Alisema ingawa kuna watu wanashikilia dhana kwamba, utawala wa kiimla unaweza kuleta maendeleo, ukweli ni kwamba, maendeleo hayo hayawi endelevu, kwa sababu kwa kawaida watawala wanajisahau kwa kuwa hawahojiwi na hawawajibishwi na wananchi.

  Alisema vyombo vya habari vina wajibu muhimu wa kuwapa wananchi uwezo wa kuchukua hatua, kuwawajibisha watawala na kushirikishwa katika maamuzi ya kuendesha nchi zao.

  “Demokrasia inaleta maendeleo, harakati za maendeleo ni lazima ziwahusishe watu ndani ya nchi; tatizo kubwa la maendeleo ya Afrika ni kuwatenga baadhi ya wananchi,” alisema Dk. Kaberuka na kuvitaka vyombo vya habari kufanya kazi ya kuwawezesha wananchi wawe na uwezo wa kuhoji na kuwawajibisha watawala wao.

  Mkutano huo unaoendelea mjini hapa, unahudhuriwa na wamiliki wa vyombo vya habari kutoka barani Afrika, watendaji wakuu wa vyombo vya habari, mashirika yasiyo ya kiserikali yanayojihusisha na maendeleo ya umma na vyombo vya habari.

  Huu ni mkutano wanne kufanyika tangu kuundwa kwa AMLF mwaka 2008 nchini Sierre Leone na kisha kufuatiwa na mikutano mingine ya mwaka iliyofanyika Lagos 2009, Camerron 2010 na huu wa sasa, ambao uliletwa hapa kwa kutambua nguvu ya mitandao ya kijamii (social media), katika kuleta maendeleo hasa baada ya kufanikiwa kwa mapinduzi ya Tunisia, ambayo yamepeleka msukumo mkubwa wa mageuzi katika mataifa mengi ya Kiarabu.

  Mada kuu ya mkutano huu, ni vyombo vya habari vya kawaida kama magazeti, redio na televisheni, zina nafasi gani katika ulimwengu wa sasa wa mawasilino ya mitandao ya kijamii kama facebook, youtube na twitter.
  CHANZO: NIPASHE

 2. k

  kaeso JF-Expert Member

  #2
  Nov 12, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 551
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  aliyoongea yana ukweli ndani yake
   
 3. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #3
  Nov 13, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Waziri Mkuu wa Tunisia, Beji Caid el Sebsi

  Waziri Mkuu wa Tunisia, Beji Caid el Sebsi, amesema ni lazima nchi za Afrika ziwe macho na viongozi wake wanaochaguliwa kidemokrasia kama kweli wanaendesha nchi zao kwa misingi ya kidemokrasia, kwa sababu uzoefu umeonyesha kwamba, wapo wanaoingia madarakani kama wanademokrasia lakini hubadilika na kuwa madikteta.

  Akifungua mkutano wa mwaka wa Taasisi ya Vyombo vya Habari vya Afrika na Viongozi (AMLF), mjini Tunis jana, alisema Tunisia iliongozwa na mtu mmoja kwa robo karne akiaminika kwamba ni kiongozi mzuri, lakini yaliyofanywa baada ya kutokea kwa mapinduzi ya nguvu ya umma, hadi leo wanastaajabu matatizo, ambayo ameyaacha nchini humo.

  Alisema ingawaje Tunisia ilikuwa ikipigiwa mfano kwa maendeleo miongoni mwa nchi za Afrika, ukweli ulio dhahiri kwa sasa ni kwamba, kuna maeneo mengi ya nchi hiyo yaliachwa nyuma sana, hakuna miundombinu na yamekuwa ni changamoto kubwa kwa serikali ya mpito.
  Hata hivyo, pamoja na kusifu hatua zinazopigwa nchini kwake kwa sasa kwa kuruhusu uhuru zaidi wa vyombo vya habari, alionya kwamba, si

  kila mapinduzi yanayotokea katika nchi yanahakikishia wananchi demokrasia na uhuru zaidi, kama juhudi za kweli za kutoa demokrasia kwa mwananchi hazitachukuliwa na serikali hasa kuhakikisha maendeleo yanafikia kila jamii.
  Alisema mapinduzi ni lazima yalenge kutoa nguvu kwa wananchi na kuwapo kwa utawala bora wa kidemokrasia, ambao utawahakikishia wananchi kuchagua viongozi wake.

  Alisema kwa mara ya kwanza katika historia ya Tunisia, Oktoba, mwaka huu, ulifanyika uchaguzi wa wabunge ulio huru na wa kidemokrasia, ambao ulisimamiwa na tume huru ya uchaguzi.

  Alitoa rai kwa mataifa mengine ya Afrika, kama Misri na Libya, ambayo yameshuhudia mapinduzi kama ya Tunisia, kutambua kuwa bila kufungua milango ya demokrasia na kuwapa watu uhuru na rasilimali zinazolenga kuwakomboa, mapinduzi yaliyofanyika hayatakuwa na maana.
  Kauli ya kuwawezesha wananchi pia ilitolewa na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Dk. Donald Kaberuka, ambaye alisema umaskini

  una msingi mmoja, kwamba, si tu ni kielelezo cha ukosefu wa raslimali, lakini pia unaelezwa katika kuwanyima wananchi uwezo wa kuhoji waliopewa madaraka, kuwawajibisha ili wafanye maamuzi yanayoleta maendeleo ya wote.

  Alisema ingawa kuna watu wanashikilia dhana kwamba, utawala wa kiimla unaweza kuleta maendeleo, ukweli ni kwamba, maendeleo hayo hayawi endelevu, kwa sababu kwa kawaida watawala wanajisahau kwa kuwa hawahojiwi na hawawajibishwi na wananchi.

  Alisema vyombo vya habari vina wajibu muhimu wa kuwapa wananchi uwezo wa kuchukua hatua, kuwawajibisha watawala na kushirikishwa katika maamuzi ya kuendesha nchi zao.

  “Demokrasia inaleta maendeleo, harakati za maendeleo ni lazima ziwahusishe watu ndani ya nchi; tatizo kubwa la maendeleo ya Afrika ni kuwatenga baadhi ya wananchi,” alisema Dk. Kaberuka na kuvitaka vyombo vya habari kufanya kazi ya kuwawezesha wananchi wawe na uwezo wa kuhoji na kuwawajibisha watawala wao.

  Mkutano huo unaoendelea mjini hapa, unahudhuriwa na wamiliki wa vyombo vya habari kutoka barani Afrika, watendaji wakuu wa vyombo vya habari, mashirika yasiyo ya kiserikali yanayojihusisha na maendeleo ya umma na vyombo vya habari.

  Huu ni mkutano wanne kufanyika tangu kuundwa kwa AMLF mwaka 2008 nchini Sierre Leone na kisha kufuatiwa na mikutano mingine ya mwaka iliyofanyika Lagos 2009, Camerron 2010 na huu wa sasa, ambao uliletwa hapa kwa kutambua nguvu ya mitandao ya kijamii (social

  media), katika kuleta maendeleo hasa baada ya kufanikiwa kwa mapinduzi ya Tunisia, ambayo yamepeleka msukumo mkubwa wa mageuzi katika mataifa mengi ya Kiarabu.
  Mada kuu ya mkutano huu, ni vyombo vya habari vya kawaida kama magazeti, redio na televisheni, zina nafasi gani katika ulimwengu wa sasa wa mawasilino ya mitandao ya kijamii kama facebook, youtube na twitter.  CHANZO: NIPASHE

  Umesema kweli Mkuu wa Tunisia nakupa pongezi sana. :poa
   
Loading...