Afrika Kusini ya jana (1950s) na ya leo (2000s) kumbukumbu

Ahsante sana kwa mada nzuri iliyoielezea experience yako katika kutembelea nchi mbalimbali hasa hizi za SADC,SIASA ya SA imepindishwa mno na wanasiasa wetu kwa faida moja au nyingine ni ukweli usiopingika kuwa pressure iliyowekwa na Baba wetu wa Taifa akishirikiana na viongozi wengine ilisaidia kuondolewa kwa siasa ya kibaguzi hapo SA,ILA hii ilikuwa sehemu ndogo tu ya juhudi zote,ukomo wa siasa hii ya kibaguzi ulichangiwa zaidi na msukumo ndani ya nchi yenyewe hasa baada ya maandamano ya wanafunzi kupinga kutumika kwa lugha ya Africaans katika masomo yao(1976),pia msukumo mkubwa uliletwa na mkusanyiko chini ya UDF ambao ndio walichangia kwa kiasi kikubwa mabadiliko ya kisiasa ndani ya SA,Uchumi wa SA uliyumba sana miaka ya 1980s ukawa dhaifu na pressure kubwa kutoka mataifa ya Ulaya na USA,tuelewe kuwa hakuna popote ambapo jeshi la makaburu lilipambana uso kwa uso na wapigania uhuru(katika medani hii ya kivita hakuna nchi yeyote kusini wa Africa ambayo ilikuwa na uwezo wa kusimama kivita na jeshi hili)yaliyotokea Angola its a debate of another day ila elewa CUBA na URUSI hawakushinda ile vita ni propaganda tu tulizolishwa kuhusu real what happened katika medani ya kivita pale;always time na history ni mwalimu mkweli.

Mkuu nakubaliana na analysis yako hususan kuhusu haswa sababu ya kuanguka kwa siasa za ubaguzi wa rangi Afrika Kusini. Ni kweli sababu kubwa moja wapo ilikuwa ni mapambano yaliyokuwa yanafanyika ndani ya nchi hata kuifanya nchi kuwa ngumu kutawalika kufuatia tamko na chama cha ukombozi cha ANC (render the country ungovernable). Lakini pia sababu nyingine kubwa sana ilikuwa ni kushindwa kijeshi kwa jeshi la Makaburu kwenye vita vya Angola (Cuito Cuanavale 1986) walipopambana na majeshi ya Angola na Cuba. Hii sio propaganda, sema bahati mbaya hii haijaandikwa vya kutosha na nchi ya kwetu yenye historia kubwa sana kwenye mapambano ya ukombozi kusini mwa Afrika hatujaweza kupata wana historia kuandika kwa undani na upana kuhusu kipindi hiki muhimu sana katika historia ya Afrika na watu wake. Haifai kupotosha au kutoa majibu ya haraka haraka yasiyo ya kweli kuhusu hili sababu historia ndio mzizi wa utaifa na uhai wa utu(race) wetu. People without knowledge of their history and origin is like a tree without roots - Marcus Mosiah Garvey. Kwa hiyo tuweke umuhimu kwenye hili. Kama ulivyosema jeshi ya makaburu lilikuwa halijawahi kushindwa kwenye uwanja wa mapambano na nchi zote zilizokuwa mstari wa mbele kwenye ukombozi wa Kusini mpaka lilipogigwa kwenye vita ya Cuito Cuanavale (1986), Angola. Kama mnavyojua ukiangalia Jiografia Cuito Cuanvale iko ndani ya Angola na makaburu walikuwa wako kusini mwa Angola toka mwaka 1975 mpaka baada ya kusimama kwa vita hiyo 1986 ndipo yalikuwa kwa mara ya kwanza nje ya mipaka ya Angola, yakiwa yamekimbilia Namibia (ikiwa koloni la Makaburu). Kushindwa huko ndiko ilikuwa chanzo cha mazungumzo ya uhuru wa Namibia na kuanza kwa mabadiriko ndani ya Afrika Kusini. Kama unafuatilia utaona kuwa baada ya kutoka gerezani Nelson Mandela alitembelea Cuba ikiwa kati ya ziara zake za kwanza nje, na kwa maneno yake alisema amekwenda kutoa shukurani kwa wananchi wa Cuba kwa mchango wao kwenye ukombozi wa nchi yake. Na si hivyo tu pia utakumbuka kuwa rais wa Cuba wakati ule marehemu Fidel Castro alialikwa kuwa ndio mgeni rasmi kwenye sherehe za kuapishwa Mandela 1994. Sisemi Urusi (USSR) hapana nasema Cuba. Mchango wa Cuba kwenye ukombozi kusini mwa Afrika ulikuwa mkubwa sana na wala si propaganda. Ni kati ya historia muhimu sana kwa nchi kama Tanzania kuijua kiundani sababu kusema kweli Tanzania bila mchango wake kwenye ukombozi kusini mwa Afrika bado ukoloni kusini ungekuwa bado upo. Basi ni muhimu tufanye tafiti kuandika sura mbali mbali zilizowezesha ukombozi huu kutimia. Mungu Ibariki Afrika.
 
South Africa kweli wana siasa ndio wanaiangusha hata Sasa wazungu wengi nakimbia South Africa, wengi wanaenda Asia Kama china na kwengineko. Too much crimes. Inatisha Sana na inasikitisha Sana.
 
Nimeipenda sana jinsi ulivyofanya utafiti na kuiandika kwa makini I salute you,ni vema hii historia wengi wakaijua maana watanzania wengi nina imani hawajawahi kujua ukweli nini kilijili mpaka uhuru wa Namibia na SA ukapatikana,wengi tumelishwa zaidi na habari za wanasiasa ambayo walikuwa na malengo yao,huku ukweli wenyewe wakiufagilia chini ya zuria;we have the rights to agree or disagree ILA ni vema FACTS zikawa hivyo kwangu mimi ukweli ya haya ndio ninayaamini baada ya kufanya utafiti wangu,kusoma vitabu mbalimbali vilivyoelezea kwa undani kuhusu battle hii:matokeo ya vita ile ndiyo iliyoleta matokeo ya uhuru wa Namibia,SA,na kuondolewa kwa vikosi vya Cuba na wataalam wa kivita wa Urusi(kipindi hicho);in the battle fields SADF hawakushindwa kwenye vita hivyo ila walifanikiwa kufikia malengo yao(lengo ilikuwa kuzuia vikosi vya jeshi la Angola kuweza kuuteka mji wa Jamba ambako ndiko yalikuwa makao ya chama cha UNITA chini ya Gen.Savimbi,maana kipindi hicho almost eneo nusu ya Angola hasa south and south East yalikuwa chini ya UNITA) Katika mapambano hayo yaliwezesha lengo la majeshi ya serikali lisifikiwe,mapambano yaliyopiganwa maeneo hayo hadi kwenye viunga vya mji wa CUITO,na kutokana na amri ya political masters wa jeshi la Makaburu haikuwa lengo lao to overrun Cuito kwa hiyo kukawa na kama mwisho wa vita bila mshindi;Baada ya hapo mazungumzo yalifanyika na kilichotokea ndio kilipelekea uhuru wa Namibia,kuondoka kwa Wacuba Angola na kuwezeshwa kwa mazungumzo yz kumaliza siasa za ubaguzi wa rangi ndani ya SA;Please kama unaweza kitafute kitabu cha The Battle of Cuito Cuanvale by Leopard Scholtz;na kitabu cha Historia ya Savimbi(hiki kitakupa nafasi vile vile ya kujua kutofautiana kati ya Baba wetu wa Taifa Nyerere(RIP) na president KK wa Zambia kuhusu siasa za Angola na why Savimbi alikuja kuuawa not far na mpaka wa Angola na Zambia),otherwise MKUU huwa napenda sana uandishi kama wa kwako ambao facts zinaelezwa jinsi zilivyo.
 
Hakika. Ukipitia hapa utapata uhondo mzuri wa vita ilivyokuwa pale Cuito Cuanvale
Battle of Cuito Cuanavale 1988

Nikanini nimefurahi kumpata mchunguzi wa historia kama wewe nashukuru kwa kunitajia hivi vitabu nitavitafuta kwa udi na uvumba. Na tuendelee kuchambua ukweli kwenye historia yetu. Good luck
 
Nyerere alituachia hivyo je viko wapi Leo?
ATC ilikufa na standard gauge ya Tazara iko hoi.
Utu ni Bora kuliko vitu

Nyerere hakutuachia misingi ya UTU??
Ulisoma AZIMIO la ARUSHA? Huoni togetherness tuliyonayo waTanzania?
 
Nikanini nimefurahi kumpata mchunguzi wa historia kama wewe nashukuru kwa kunitajia hivi vitabu nitavitafuta kwa udi na uvumba. Na tuendelee kuchambua ukweli kwenye historia yetu. Good luck
please do that thanks
 
Back
Top Bottom