Afrika Kusini na ubaguzi wa rangi, picha hii yazua taharuki

Kingsmann

JF-Expert Member
Oct 4, 2018
4,446
16,299
Mama wa mtoto katika shule ya awali ya Laerskool Schweizer-Reneke iliyopo katika jimbo la North West huko Afrika Kusini, amechukizwa vikali baada ya picha inayomuonesha mtoto wake wa kike na watoto wengine watatu wa Kiafrika wakiwa wamekaa peke yao mbali na watoto wengine wa kizungu kwenye darasa lao. Picha hiyo ambayo inasambaa kwa kasi mtandaoni, imesababisha hasira kubwa kwa raia wa nchi hiyo kutokana na kuwa na ishara ya ubaguzi wa rangi.

Picha hiyo ilitumwa kwenye kundi la WhatsApp la shule hiyo na mwalimu wa darasa. "Hii ilipaswa kuwa siku ya kufurahisha kwangu lakini sio,” amesema mzazi huyo. Mama huyo ambaye hakutajwa jina kulinda utambulisho wa mwanae, ameiambia tovuti ya TimesLIVE ya nchini humo kuwa siku ya kwanza katika darasa hilo ilianza vizuri.

Yeye na wazazi wengine waliwapeleka watoto wao na kuambiwa waondoke katika eneo la shule. Saa tatu asubuhi walitumiwa taarifa kutoka kwa mwalimu wa watoto hao kuhusu siku ilivyokwenda kupitia WhatsApp group. Picha hiyo ilionesha watoto 18 wa kizungu wakiwa darasani wamekaa dawati moja lililounganishwa katikati ya darasa, wakati watoto wanne wa Kiafrika wakiwa wamekaa kwenye dawati moja lililowekwa kwenye kona ya darasa hilo. "Nilichoona ni jumbe toka kwa wazazi wa kizungu wakisema asante asante kwenye WhatsApp group, lakini hakuna yeyote aliyesema kuhusu walivyotenganishwa,” alisema mzazi huyo.

Amesema baada ya kujadiliana na mzazi mwingine nje ya WhatsApp group, mzazi huyo aliwasiliana na mkuu wa shule kuuliza kuhusu ukaaji wa watoto hao darasani. TimesLIVE imedai mkuu huyo wa shule alisema hakuwa na taarifa za suala hilo. Wamedai kuwa wanasubiri jibu toka kwa shule hiyo.

Alipoulizwa kuhusu anavyojisikia kutokana na hali hiyo, mama huyo amesema ana matumaini kuwa mwanae mwenye umri wa miaka mitano bado ni mdogo kuweza kutambua kilichotokea.
"Lakini nimechukia,” alisema mama huyo aliyeahidi kuchukua hatua zaidi.

Source: Bongo5
skytanzania-20190109-0001.jpeg
 
Shule ya msingi ya Schweizer-Reneke Imekumbwa na kashfa ya kuwabagua Wanafunzi weusi katika shule yao

Tazama picha....
IMG_20190109_181553.jpg

Picha imezua hasira za watu kupitia mitandao ya kijamii.

Taifa la Afrika lilikomesha Sera ya kibaguzi ya Apartheid mwaka 1994 hivyo picha hiyo imezua hisia za uwepo wa ubaguzi katika jamii yao
 
huu ni ujumbe wa wazi kabisa kwetu watu weusi kuwa hata kama tunaoneana kivipi humu kwenye nchi zetu kwa msingi wa makabila,
vyama na mali lakini kwa mzungu wote anatuona takataka

sasa kweli hiyo ni picha imepigwa na kutumwa kwa wazazi ikiwa hivyo vipi yanayofanyika nje ya camera kama sio kutatatuana marinda ni nini
 
huu ni ujumbe wa wazi kabisa kwetu watu weusi kuwa hata kama tunaoneana kivipi humu kwenye nchi zetu lakini kwa mzungu wote anatuona takataka

sasa kweli hiyo ni picha imepigwa na kutumwa kwa wazazi ikiwa hivyo vipi yanayofanyika nje ya camera kama sio kutatatuana marinda ni nini
kwel kwani si wenyew tupo kwenye inch zao hizi issue tunaziona japo wanajarib kufichacha lakin ukwel mzungu hampendi mweusi ni bora aishi na mwarab au mhindi
than black people

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mama wa mtoto katika shule ya awali ya Laerskool Schweizer-Reneke iliyopo katika jimbo la North West huko Afrika Kusini, amechukizwa vikali baada ya picha inayomuonesha mtoto wake wa kike na watoto wengine watatu wa Kiafrika wakiwa wamekaa peke yao mbali na watoto wengine wa kizungu kwenye darasa lao. Picha hiyo ambayo inasambaa kwa kasi mtandaoni, imesababisha hasira kubwa kwa raia wa nchi hiyo kutokana na kuwa na ishara ya ubaguzi wa rangi.

Picha hiyo ilitumwa kwenye kundi la WhatsApp la shule hiyo na mwalimu wa darasa. "Hii ilipaswa kuwa siku ya kufurahisha kwangu lakini sio,” amesema mzazi huyo. Mama huyo ambaye hakutajwa jina kulinda utambulisho wa mwanae, ameiambia tovuti ya TimesLIVE ya nchini humo kuwa siku ya kwanza katika darasa hilo ilianza vizuri.

Yeye na wazazi wengine waliwapeleka watoto wao na kuambiwa waondoke katika eneo la shule. Saa tatu asubuhi walitumiwa taarifa kutoka kwa mwalimu wa watoto hao kuhusu siku ilivyokwenda kupitia WhatsApp group. Picha hiyo ilionesha watoto 18 wa kizungu wakiwa darasani wamekaa dawati moja lililounganishwa katikati ya darasa, wakati watoto wanne wa Kiafrika wakiwa wamekaa kwenye dawati moja lililowekwa kwenye kona ya darasa hilo. "Nilichoona ni jumbe toka kwa wazazi wa kizungu wakisema asante asante kwenye WhatsApp group, lakini hakuna yeyote aliyesema kuhusu walivyotenganishwa,” alisema mzazi huyo.

Amesema baada ya kujadiliana na mzazi mwingine nje ya WhatsApp group, mzazi huyo aliwasiliana na mkuu wa shule kuuliza kuhusu ukaaji wa watoto hao darasani. TimesLIVE imedai mkuu huyo wa shule alisema hakuwa na taarifa za suala hilo. Wamedai kuwa wanasubiri jibu toka kwa shule hiyo.

Alipoulizwa kuhusu anavyojisikia kutokana na hali hiyo, mama huyo amesema ana matumaini kuwa mwanae mwenye umri wa miaka mitano bado ni mdogo kuweza kutambua kilichotokea.
"Lakini nimechukia,” alisema mama huyo aliyeahidi kuchukua hatua zaidi.

Source: Bongo5View attachment 990332
Mbaya zaidi wamekalishwa wakigeuzia mgongo ubao which means wakichoka hawatatazama ubao
 
Kwa kweli nimejisikia vibaya sana hasa kubaguliwa kwa watoto wadogo namna hii, huu ubaguzi hauwezi kwisha so long tumezaliwa rangi tofauti, ni kwa vile tu labda bado wadogo hawataweza kukumbuka hili tukio lakini kama mimi ni mzazi WA mmoja wa hao watoto ningemuhamisha siku hiyohiyo maana hapo watanyanyasika tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndo mabebberu tukishindwana kwenye siasa tuna wakimbilia kuomba kupasha vijambio

Back
Top Bottom