Afrika Kusini: Meya wa mji wa Durban atimuliwa kwa tuhuma za rushwa

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,495
9,275
Wakati huo huo Chama cha ANC chenye viti vingi bungeni kimeamua kumfukuza Meya wa mji wa Durban, Zandile Gumede.

Hivi sasa yuko chini ya uchunguzi wa utakatishaji fedha na rushwa katika kesi ya udanganyifu wakati wa kupata mkataba wa zabuni. Kashfa hiyo haimhusu Gumede pekee, lakini inawahusu pia madiwani zaidi ya sitini kutoka mkoa wa KwaZulu-Natal.

ANC imemaliza mgogoro unaodumu zaidi ya miezi miwili katika Manispaa ya jiji la Durban. Zandile Gumede, Meya wa mji huo kwa miaka mitatu, alikuwa tayari amesimamishwa na kamati ya mkoa tangu mwezi Juni. Na kwa sasa ametimuliwa kabisa na chama cha Cyril Ramaphosa.

Zandile Gumede na madiwani 62 wa manispaa ya jiji na mkoa wanatuhumiwa ubadhirifu wa mali ya umma.
 
Back
Top Bottom