Afrika Kusini kulegeza masharti ya Lockdown kuanzia Mei Mosi ili kufufua uchumi wa taifa hilo

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,498
9,279
Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini ametoa hotuba kwa njia ya televisheni akisema kuanzia tarehe 1 Mei, Afrika Kusini itapunguza hatua za zuio dhidi ya maambukizi ya virusi vya Corona kuwa ngazi ya nne, na kuruhusu baadhi ya biashara kufunguliwa tena.

Rais Ramaphosa amesema kuna ushahidi wa kutosha unaoonyesha kuwa, hatua za zuio zilizochukuliwa kote nchini tangu tarehe 27 Machi, zimeonesha ufanisi katika kuzuia kuenea kwa virusi vya Corona, wakati huohuo pia kuna haja ya haraka ya kufufua uchumi.

Kabla ya hapo, rais Ramaphosa alitangaza kuwa Afrika Kusini imeingia katika kipindi cha pili ya mapambano dhidi ya virusi vya Corona, ambacho kipaumbele ni kutuliza uchumi na ajira, na kuweka mpango wa msaada wa kiuchumi na kijamii wenye thamani ya rand bilioni 500.
 
Back
Top Bottom