Afrika Kusini: Jacob Zuma akana mashtaka ya ufisadi mwanzoni mwa kesi yake

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,500
9,279
Jacob Zuma alisema NAPINGA makosa yote 18 ya ulaghai, ufisadi, ulaghai, ukwepaji wa kodi na utakatishaji fedha haramu.

Mashtaka hayo yanahusiana na matukio ya zaidi ya miongo miwili - katika siku za mwanzo za demokrasia ya Afrika Kusini - pamoja na mpango mkubwa wa silaha wenye utata.

Bwana Zuma na washirika wake wanasisitiza kuwa kesi hiyo ni ya kisiasa. Umati wa watu umekusanyika nje ya ukumbi wa mahakama huko Pietermaritzburg kuashiria kuwa Bwana Zuma bado ana umaarufumiongoni mwa wafuasi wake.

Lakini sasa kuna ushahidi mkubwa wa ufisadi uliofanikiwa katika kipindi cha uongozi wa madarakani, na Waafrika Kusini wengi wanataka kuona haki ikitendeka.

Zuma pia anakabiliwa na madai mapya ya ufisadi na huenda akafungwa jela kwa kukiuka amri ya mahakama katika kesi nyingine tofauti. Waafrika Kusini wanaamini kesi hiyo inaweza kuashiria mabadiliko ya nchi hiyo.

Baadhi ya mashujaa wa ukombozi wa Afrika Kusini waliohai wamemshtumu Bw. Zuma– kumlinganisha na jambazi na kuonya itachukua muda mrefu kurekebisha uharibifu alioufanya dhidi ya taasisi changa za nchi.

BBC
 
Duuu ama kweli mpanda ngazi hushuka. Kwahiyo mwamba licha ya alikua rais pia anaburuzwa mahakamani na akikutwa na hatia jela inamuhusu

Daaa katiba katiba katiba

Bongo ndio kwanza wakina sabufa la bunge wamejiwejea kinga ya kutoshtakiwa tutafika kweli ndugu zanguni?

Daaaaa napata hasira Sana nikifikiria kuhusu katiba yetu mbovu hii hivi tutafika levo za SA kweli?
😓😓😓😥😪
 
Back
Top Bottom