Afrika inakwenda kombo-tujimumushe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Afrika inakwenda kombo-tujimumushe

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mwankuga, Dec 25, 2010.

 1. mwankuga

  mwankuga JF-Expert Member

  #1
  Dec 25, 2010
  Joined: Aug 30, 2010
  Messages: 329
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45
  Mwaka 1962,Mfaransa R.DUMONT aliandika kitabu kiitwacho THE FALSE START OF AFRICA,ambacho kimefupishwa na kutafsiriwa na GABRIEL RUHUMBIKA mwaka 1974.Katika dibaji ya kitabu hicho kinasema hivi;"Afrika inakwenda kombo!Jina la kitabu chako ni kali sana.Kitawakasirisha Waafrika.Unafahamu jinsi wasivyopenda kutolewa makosa.Utasemwa kama unawanyanyasa kama mkoloni mwenyewe;kwani kuyatoa makosa mataifa mapya haya na viongozi wake ni kuunga mkono,waliokuwa wakidai kwamba Waafrika hawajawa tayari kujitawala".

  UKURASA WA 39."WATEULE WANAISHI KAMA MTOTO WA MFALME.
  "Haiwezekani kuendeleza nchi kwa kuongeza maradufu wafanyakazi wa ofisini au kwa kugawia marafiki vyeovinavyowapatia mishahara bila kufanya kazi,ila tu kwa kuunganisha watu wenye utashi wa kazi ili kutekeleza matakwa yanayomfaidisha kila mmoja.Kama mambo yasiporekebishwa,uendeshaji wa serikali ndio utakaoteketeza nchi za Kiafrika".

  "Kwa waziri mdogo ana motokaa ya serikali ambayo mara nyingi si motokaa ndogo,pamoja na dereva,kwa matumizi yake binafsi.Raisi wa nchi ndogo kama Dahomey hawezi kutoka nje bila kutanguliwa na safu za za askari wa pikipiki,na wengi wa hawa maraisi wanaota kushindana na ikulu ya Ufaransa."pg 40

  "Wafanya kazi wa serikali,wabunge na mawaziri wameunda kundi lililoneemeka sana na linalojijali lenyewe peke yake.Uingereza mbunge anapata mshahara wa mtumishi wa cheo cha kati.Ufaransa anapata ule mshahara wa cheo cha juu.Kwa sababu ya ile siasa ya UZUNGU MWEUSI ilitaka makoloni ya Wafaransa yaamini kuwa na yenyewe pia ni Ufaransa,mbunge wa nchi ndogo sana na masikini kama Gaboni anapokea mshahara mkubwa kuliko wa mbunge wa Kiingereza"

  "Maraisi na mawaziri wajanja wanarundika akiba kwa siku za uzee katika mabenki ya Switzerland,na wake zao wananunua majumba makubwa makubwa kandokando ya ziwa Geneva huko huko Switzerland"pg 41.

  "Awe mbunge au mtumishi wa serikali,mara tu Mwaafrika akisha pata anaona lazima ndugu zake,siku nyingine kijiji chake chote,nao wafaidi.Ukarimu ambao ni jadi ya Waafrika unastahili sifa unapomaanisha tuseme mtu kumwelimisha mpwa wake masikini mpaka kufikia kumaliza masomo yake"pg44

  "Maofisini nafasi nyingi sana za kazi zinajazwa kwa kufuata undugu,na sio ujuzi wa kazi.Mkubwa wa ofisi ya waziri kwa kawaida ni mtu wa kabila la waziri yule.Maofisa hasa mawaziri wanapoteza vibaya sana muda wao wa nadra,ambao wangeweza kutumia kusoma ripoti za wizara zao au ktembelea sehemu zilizo na matatizo na kuyachunguza".

  Ngoja niishie hapo,lakini inasemekana kuwa Hayati J.K Nyerere amewahi kuwalazimisha waziri kukisoma kitabu hicho kwani kimefichua tabia nyingi ambazo Waafrika wamerithi kutoka kwa wakoloni.

  Naipost thread hii ili kutaka kuwahamasisha wana jamii kujenga utamaduni wa kusoma vitabu mbalimbali.Pia naomba mkitafuta kitabu hicho,kwa sababu ya tabia hizi za viongozi wetu kutaka ufahari,maisha ya peponi,matanuzi ya kutisha tofauti na maisha ya wananchi waliowengi.Kimsingi tuna matatizo mengi sana ambayo ni lazima tushikamane kwa upendo kukatisha ndoa ya viongozi wetu na mafisadi.Hawa viongozi wetu ni hatari sana kuliko tunavyoana.

  Nasubiri mrejesho kutoka kwenu wadau,baada ya hapo tutakuja kwenye maisha ya sasa ya viongozi wetu kwa kusema mambo maovu na pasipo kujali.Naomba kuwasilisha.
   
 2. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #2
  Dec 25, 2010
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Nakubaliana na wewe mkuu! This is a true color ya utawala wa kiafrika na halina ubishi hata chembe. anayebishi na seme sasa tumuone. copy ya hicho kitabu twaweza kuipata wapi? Soma na kile cha ''it's our turn to eat'' cha wakenya humo pia utajionea tabia halisi ya wakoloni weusi!
   
 3. mwankuga

  mwankuga JF-Expert Member

  #3
  Dec 26, 2010
  Joined: Aug 30, 2010
  Messages: 329
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45
  Mkuu nitajitahidi kukitafuta kitabu hicho,kuhusu kitabu cha "THE FALSE START OF AFRICA" kinaweza kupatikana katika bookshop ya UDSM.
   
 4. BIN BOR

  BIN BOR JF-Expert Member

  #4
  Jan 10, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 752
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Kwa bahati mbaya au nzuri nilikisoma kitabu hicho nikiwa darasa la pili kikanichanganya akili nikaichukia hali ya kisiasa ya Afrika hata sasa. Ukisoma maelezo yake kinasema hata Nyerere aliwalazimisha mawaziri wake wote wakisome na kukielewa kitabu kile. Nahisi ni Nyerere aliyelipia ile tafsiri ya kiswahili ya babu yangu Ruhumbika. Jamani sio siri, Afrika inakwenda kombo na hasa Tanzania.
   
 5. j

  jamal_tanga Member

  #5
  Jan 10, 2011
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 15
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  sudan zinajitenga kuwa inchi mbili sasa zanzibar nayo ina fuatia nadhani wanhaki ya kuwa huru
   
 6. BIN BOR

  BIN BOR JF-Expert Member

  #6
  Jan 10, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 752
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Ninaitamani siku tutakayojitenga na Zanzibar.....................na ije siku hiyo mapema.
   
 7. nuraj

  nuraj JF-Expert Member

  #7
  Nov 3, 2013
  Joined: Dec 16, 2011
  Messages: 310
  Likes Received: 163
  Trophy Points: 60
  Maneno aliyoandika Rene' Dumont miaka ya sitini, yakajidhihiri kwa ufasaha katika tawala za kiafrika. Miaka imeenda ikarudi, ikaingia demokrasia na vyama vingi huku vyama vya upinzani vikijinadi kuleta ukombozi na kubadilisha hali hiyo, leo hii natafakari kwa kina kujaribu kuiona tofauti lakini sioni, zaidi tu sana inadhihirika kuwa hata tunaojaribu kuwaamini kuwa wanahubiri mabadiliko, mapinduzi na ukombozi nao ni walewale, wanatusukuma kwenye mwanzo ule ule mbovu wa Afrika. Ama niseme tu mara hii kwamba, ''Tanzania inakwenda kombo''
   
 8. nuraj

  nuraj JF-Expert Member

  #8
  Nov 3, 2013
  Joined: Dec 16, 2011
  Messages: 310
  Likes Received: 163
  Trophy Points: 60


  Maneno aliyoandika Rene' Dumont miaka ya sitini, yakajidhihiri kwa ufasahakatika tawala za kiafrika. Miaka imeenda ikarudi, ikaingia demokrasia na vyamavingi huku vyama vya upinzani vikijinadi kuleta ukombozi na kubadilisha halihiyo, leo hii natafakari kwa kina kujaribu kuiona tofauti lakini sioni, zaidi tusana inadhihirika kuwa hata tunaojaribu kuwaamini kuwa wanahubiri mabadiliko,mapinduzi na ukombozi nao ni walewale, wanatusukuma kwenye mwanzo ule ule mbovuwa Afrika. Ama niseme tu mara hii kwamba, ''Tanzania inakwenda kombo''

   
Loading...