Afrika inahitji Taasisi Imara siyo Viongozi Imara

PANAFRICA

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
335
496
Haya ni maneno yaliyotamkwa na Rais mstaafu wa Marekani Barrack Obama alipofanya ziara nchini mwaka 2014."Africa needs strong institution rather than strong men".
Hivi kweli watanzania tulimuelewa?

Tunawe mikono na kuvaa barakowa
Corona IPO na hatari.
 
HATA OBAMA ANAKOSEA PIA, TAASISI MUHIMU INAUNDWA NA VIONGOZI IMARA, TIMAMU NA WENYE UTHUBUTU KATIKA KUCHUKUA MAAMUZI SAHIHI NA KWA WAKATI SAHIHI
 
Hii ni kweli ili hata kama kiongoz akiwa mbovu system inamshape automatically

Its not over until its over...
Ni kweli cionawana Trump ni mbishi kiasi kwamba anapingana na wataalamu wa sayansi katika mambo nyeti.....ila system inamnyoosha vizuri wa marikani hawapati mathara ya utendaji wake mbovu.....lakini kupata institution imara hapa Africa it's a dream our leaders are selfish
 
Nyumba imara inatengenezwa na matofali imara so ili uwe na taasisi imara basi lazima uwe na watu imara,muunganiko wao ndio utakao kupa taasisi imara.
 
Kuna kitabu kimoja, kama una muda na hujawahi kukisoma kitafute ukisome, ni keki kabisa kwenye hili uliloliongea. "Why Nations Fail" kimeandikwa na Daron Acemoglu pamoja na James A. Robinson
 
Nyumba imara inatengenezwa na matofali imara so ili uwe na taasisi imara basi lazima uwe na watu imara,muunganiko wao ndio utakao kupa taasisi imara.
Viongozi imara wanaoweza kujenga taasisi imara, ni wale wanaojitabanaisha kuongoza kwa kutanguliza maslahi mapana ya nchi na vizazi vijavyo.
Ni kwa bahati mbaya sana kwani viongozi wetu huangalia zaidi maslahi mapana ya uchaguzi ujao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huo ni ukweli kabisa, viongozi wenye nguvu wanakuja na kupita ila uwepo wa taasisi imara mnajihakikishia ustawi mzuri wa muda mrefu.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom