Bonde la Baraka
JF-Expert Member
- Sep 22, 2016
- 4,580
- 7,944
Hi!
Unafiki una tafsiri nyingi lakini zote huangukia katika maana moja.
Unafiki ni kufanya jambo au kusema jambo ambalo moyoni unalipinga, au unafiki ni pale mtu anapounga au kupinga jambo kwa maslahi yake binafsi huku akijua matokeo yake si mema mbele.
Unafiki pia ni sawa na kusema KUTOKUJALI.
Nchi karibu zote za kiafrika zimejaa hawa wanasiasa wanafiki na ndio waliosababisha tutambae baada ya kutembea na kukimbia.
Haiwezekani mtu ana nguo nyingi za chama chake na mfukoni ana kadi ya chama halafu ainue kinywa kusema yeye si mwanasiasa.
Tutawaamini vipi viongozi mithiri ya Julius Mtatiro ambaye alipinga/hajamtetea Makonda katika kashfa ya kutumia cheti cha mtu mwingine kujiendeleza kielimu lakini aliposikia rais kafukuza wenye vyeti fake au waliotumia vyeti vya wengine kujiendeleza akaja juu kupinga uamuzi ule ili tu ajizolee umaarufu wa kisiasa.
Haiwezekani mbunge kama Mama Kikwete na Ally Kesy kama sijakosea kuandika wapinge wanafunzi wanaopata ujauzito kurudi shule baada ya kujifungua huku wanao au watoto wa ndugu zao wanaowafadhili wakipata ujauzito hawaachi kuwasomesha na kuwaandalia mazingira mazuri baada ya kujifungua.