Afrika imejaa siasa za kinafiki, Tanzania haiwezi kuzikwepa

Phillipo Bukililo

JF-Expert Member
Dec 29, 2015
18,487
13,612
Wale matajiri wa kinigeria ambao walipeta sana katika awamu ya rais Goodluck Jonathan, kwa sasa matumbo yao yanawaka moto kwa hofu ya kufuatiliwa na awamu ya Muhammad Buhari.

Awamu ya Buhari inawatengeneza matajiri wake ambao siku kiongozi huyu akitoka kwenye uongozi, matumbo yataanza kuwaka moto. Hizo ndizo siasa za bara la Afrika.

Matajiri wa awamu ya Mwinyi hawakuwa salama wakati Mkapa. Waliotesa wakati wa Mkapa hawakupeta katika uongozi wa Kikwete. Wale waliokula bata enzi za Kikwete awamu hii wanaiona chungu.

Marais wa zamani na anayekuwa kwenye usukani wanaposimama kwa ajili ya picha za ukumbusho, huwa wanaonekana marafiki walioshibana sana, lakini zile rafu na vikumbo vinavyoendelea chini kwa chini, havifanani kabisa na sura zao za tabasamu kwa ajili ya picha.

Picha za marais wakiwa pamoja sehemu fulani huwa zinanikumbusha kuwa waafrika tuna aina fulani ya tamaduni za kimaisha ambazo zimeingilia siasa zetu na kuziharibu sana.

Sio ajabu awamu ya Mzee Rukhsa ilikuwa rahisi kukutana na watu pale samora avenue wakiwa wamevaa vibaraghashia lakini ukiwauliza majina wanakwambia wanaitwa John au Simon.

Sio ajabu wakati wa Mzee Mkapa watu wakaibuka na mtindo wa kutupia cheni ya dhahabu shingoni.

Sio ajabu enzi za Kikwete watu wakaanzisha tabia ya kutupia suti za nguvu.

Sio ajabu enzi za Magufuli watu wanaanza kuvaa mashati ya maua maua. Yote haya yanafanyika ili jamii ijisogeze kwa kiongozi mkuu. Ni aina fulani ya kumuunga mkono kiongozi wa nchi kifikra lakini kuna ujumbe mwingine wa watu hawa kutotaka meza kuu iwasahau, ili vile vinono viwafikie pia.

Siasa za kiafrika ndio zinazowafanya wamiliki wa gazeti la Marekani linalotunza taarifa za matajiri duniani maarufu kama FORBES, wasiwatilie maanani matajiri wa bara letu, kwa sababu utajiri wao ni vigumu kuutenganisha na mbinu chafu za kisiasa.
 
Wanasema afrika tajiri Na umaskini hakuna utofauti.
Kwa7bu unaweza ukalala umaskini Na ukaamka tajiri au ukalala tajiri ukamka umaskini afrika yote hayo yanawezekana.
 
Wanasema afrika tajiri Na umaskini hakuna utofauti.
Kwa7bu unaweza ukalala umaskini Na ukaamka tajiri au ukalala tajiri ukamka umaskini afrika yote hayo yanawezekana.
You are right brother, piga picha watu ambao wameshazoea kuendesha magari ya bei mbaya kutokana na dili za serikalini, ghafla wanalazimika kupandishwa karandinga kuelekea segerea. Piga picha mtu anatoka nyumbani asubuhi anaagana na mkewe na watoto vizuri tu halafu mchana akiwa ofisini anakuja kubebwa na jamaa wa TAKUKURU, ratiba yote ya maisha ya familia inakuwa imebadilika ghafla tu. Utajiri wa waafrika wengi unao uhusiano na dhuluma, ndio maana huwa haudumu.
 
Back
Top Bottom