Afrika huu ndio wakati wa kuikuta Ulaya na Marekani Kiuchumi

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
12,298
12,600
Afrika tuna bahati kuwa kasi ya kuenea na kufa kwa COVID-19 sio kubwa, tumshukuru kwa hili kwakweli. Sina uhakika kama hii inatokwna na uhodari wetu katika kuupiga vita ugonjwa. Hii ni tunu kutoka kwa MwenyeziMungu wetu. Lakini hatunabudi kuitumia bahati hii kwa kuchapa kazi kwa bidii wakati wenzetu wa Ulaya na Marekani wakiwa wamejifungia kwenye makabati.

Tutakuwa wapuuzi kama na sisi tutaamua kuwaiga wao ambao ugonjwa ni mkubwa kwa kujifungia nasisi kwenye mafriji huku tukiwa na idadi ndogo sana ya maambukizi.

Tuendelee kuchapa kazi saaana huku tukiendelea na kuchukua tahadhari za kawaida za kujikinga huku tukiendelea kuchapa kazi na kuendelea kuwaombea wenzetu huko wapate nafuu maana huwa tunategemeana.

Huu ni ule wakati wa kusema Mungu atupe nini waafrika weusi. Huu ni ule wakati wa Africa kuwa donor countries kwa wazungu.

Tusifuate mkumbo wa kujifungia nyumbani Kama wao wakati hali yetu sio Kama ya kwao. Mbona sisi wakati tukihangaika na tabu za njaa, wakimbizi, kipindupindu, HIV, TB, unyafuzi, Ebola, vita vya wenyewe kwa wenyewe wao wanaendelea kuchapakazi?

Naomba serikali ifungue shule na vyuo na kuruhusu watoto waendelee na masomo na wazazi wao waendelee na kuchapakazi huku wote tukiendelea na njia mbalimbali za kujilinda.

Kufa kufaana
Krg
 
Endeleeni kufanya kazi mfe kama kuku.
Hayo ndio matatizo ya kutegemea wanasayansi na media za wazungu. Wao walikuwa wanatuaminisha kwamba mazingira yakichafuka itakayoathirika zaidi ni Afrika.

Walikuwa wanatuona sisi mazoba eti sisi tutyaunze mazingira kwa kuzuia shughuli zetu za uzalishaji lakini wao wayachafue mazingira kwa kufanya shughuli kubwa za uzalishaji kwa kisingizio kuwa sisi ndio tutakaoumia zaidi mazingira yakiharibika. Hii ni janja yao kuwa sisi tupande misitu ili izoe uchafu wao.

Msitu wa Amazon hauwezi kuungua halafu dunia ibaki salama
 
Uwii afrika hii nayoijua? Zaidi ya kulogana na uzandiki sijawahi ona jipya teh

Sent using Jamii Forums mobile app
Kaka hii kwetu imekuja kamma process ya civilization kama vile kufanya usafi, kunawa mikono, kupunguza misongamano, level seat kwenye vyombo vya Usafiri na ustaarabu mwingine ambao pia utapunguza maradhi Kama kipindupindu, TB, scabies, fungus, magonjwa ya ngono, HIV, nk ambavyo wenzetu walifundishwa tabia hiyo ya usafi kwa kukumbwa na magonjwa ya tauni, TB, kipindupindu siku za nyuma.
 
Acha bangi za asubui, wenzio wanavuta waende shamba,wewe unavuta ili upost,Waenzio wana miaka 250 toka wanajitambua na ninyi mnamiaka 60 wapi na wapi?

Labda ungesema Wadhungu wawabadilishwe, nguo , simu kila kitu ulicho nacho na unachokitumia ni cha kwao,hadi kitanda unacholalia, Utamaduni wetu ilikuwa kuvaa majani na kulalia ngozi za wanyama .
 
Pato la Tanzania kwa mwaka ( Tanzania GDP ) ni approximately USD 454 Billions.

Wakati,

Thamani za Kampuni za kimarekani kama Apple, Amazon na Alphabet kila moja ina thamani zaidi ya USD 1 TRILLION.

Hivyo Kampuni moja tu kati y hizo ina nguvu kiuchumi kuliko Nchi Nyingi tu Afrika, Tanzania ikiwemo.

Hivyo kabla hujataka kupambana na na US au EUROPE pambana at least hata na GOOGLE kwanza.

Maana Google haipo China lakini inawasumbua sana China ingawa ni taifa kubwa pia kiuchumi.
 
Acha bangi za asubui, wenzio wanavuta waende shamba,wewe unavuta ili upost,Waenzio wana miaka 250 toka wanajitambua na ninyi mnamiaka 60 wapi na wapi? Labda ungesema Wadhungu wawabadilishwe, nguo , simu kila kitu ulicho nacho na unachokitumia ni cha kwao,hadi kitanda unacholalia, Utamaduni wetu ilikuwa kuvaa majani na kulalia ngozi za wanyama .
Mtu Kama wewe umekwisha kabisa. Watu Kama nyinyi hakuna namna yoyote ile mnaweza kumuelewa JPM.
 
Pato la Tanzania kwa mwaka ( GDP ) ya Tanzania ni approximately USD 454 Billions.

Wakati,

Thamani za Kampuni za kimarekani kama Apple, Amazon na Alphabet kila moja ina thamani zaidi ya USD 1 TRILLION.

Hivyo Kampuni moja tu kati y hizo ina nguvu kiuchumi kuliko Nchi Nyingi tu.

Hivyo kabla hujataka kupambana na na US au EUROPE pambana at least hata na GOOGLE kwanza.

Maana Google haipo China lakini inawasumbua sana China ingawa ni taifa kubwa pia kiuchumi.
Aaaaah kaka hata Ugiriki ndiyo nchi iliyokuwa na maendeleo na ustaarabu enzi hizo, Kulikuwa na Rumi, Kulikuwa na ottoman, nk. Juzijuzi nilikuwa pale Detroit nikaonyeshwa ilipokuwa makao makuu ya General Motors na kiwanda chake, Sasa hivi ni museum tu.
 
Kaa chini utulie Wewe hujui lolote kwenye masuala ya uchumi na historia!
Hivi unaelewa mwaka 1497 Afrika ilikuwa karibu sawa kimaendeleo na ulaya? Ila Mambo yalianza kugeuka miaka ya 1650,s baaada ya propaganda za wazungu?

Hivi unaelewa kuwa mwaka 1750 hadi kufikia 1850 nchi ya uingeleza ilikuwa kinala wa kiuchumi ulimwenguni kote , huku miaka iyo ya 1750 nchi ya Marekani (USA) ikiwa haina kitu chochote mbaya zaidi ikiwa Ni koloni la Mwingereza, ?

Hivi unaelewa janga la ukame la mwaka 1873, pamoja na uvamizi wa Napoleon mwaka wa 1815, magonjwa ya mazao , , migomo ya wafanyakazi ya mwaka 1811, 1850,s pamoja na majanga ya vita ya 1914 yote haya yaliiporomosha uingereza kiuchumi, na Marekani iliyokuwa mtumwa wa uingereza akawa ndo Bwana wa uingereza?

Hivi huelewi kwamba Marekani ilitumia matatizo ya uingereza kujiimarisha kiuchumi na kijamii?

Hivi huelewi kwamba ilitumia mda mfupi sana kuipiku Uingereza na sasa inaitwa Super power?

Kinachokuharibu Ni ile tunaita colonial Legacy, yani unadhani mtu mweusi hapaswi kufanikiwa kumpita mzungu.

Mungu akiendelea kuweka mkono huu ndio wakati wa kutunga sera nzuri za kiuchumi, Ndio wakati wa taifa kuwekeza kwenye tafiti za kisayansi hata kwa kuwaarika waisrael nchini.

Huu ndio wakati wa kusomesha wanafunzi zaidi na kuwafadhili zaidi( maana suala la kupuzia Elimu ndicho pia kitu kiliiponza Uingereza miaka ya 1851) matokeo yake teknolojia ikabakia pale pale (conservative)

Huu ndio wakati wa kulima sana, huu ndio wakati wa kuongeza mishahara kwa wafanyakazi ili kuongeza purchasing power nchini.

Huu ndio wakati wa kuexport zaidi na kupunguza import.

Huu sio wakati wa kulumbana kisiasa, Mimi Ni chadema lakini wakati huu napaswa kuweka uchadema wangu pembeni na kusaport kila chenye tija.

Nawasalimia.

Acha bangi za asubui, wenzio wanavuta waende shamba,wewe unavuta ili upost,Waenzio wana miaka 250 toka wanajitambua na ninyi mnamiaka 60 wapi na wapi? Labda ungesema Wadhungu wawabadilishwe, nguo , simu kila kitu ulicho nacho na unachokitumia ni cha kwao,hadi kitanda unacholalia, Utamaduni wetu ilikuwa kuvaa majani na kulalia ngozi za wanyama .
 
Chadema wenzangu acheni kupinga kila kitu, au ndo tunatimiza maana ya jina upinzani?

Tunajidharaulisha sana vyama pinzani.

MTOA MADA YUPO SAHIHI MWANZO HADI MWISHO.

JAPO NATAKA NIMKOSOE KWAMBA TUSIFANYE HAYA KWA KUSHINDANA, MAANA KUSHINDANA KWETU SI LOLOTE ZAIDI YA KUJILISHA UPEPO,

TUFANYE KAZI KWA AJILI YA UTUKUFU WA MUNGU MKUU NA SIMBA WA KABILA LA YUDA. BAASI. MAANA KUPONA NI KWA NEEMA TU, WALA SIO ASILI YA MAUMBILE YAKO KAMA ULIVYOJISIFIA MTOA MADA.

TUCHAPE KAZI Na KUMSHUKURU MUNGU KTK WINGI WA TOBA
 
Afrika tuna bahati kuwa kasi ya kuenea na kufa kwa COVID-19 sio kubwa, tumshukuru kwa hili kwakweli. Lakini hatunabudi kuitumia bahati hii kwa kuchapa kazi kwa bidii wakati wenzetu wa Ulaya na Marekani wamejifungia kwenye makabati.

Tutakuwa wapuuzi kama na sisi tutaamua kuwaiga wao ambao ugonjwa ni mkubwa kwa kujifungia nasisi kwenye mafriji huku tukiwa na idadi ndogo sana ya maambukizi.

Tuendelee kuchapa kazi saaana huku tukiendelea na kuchukua tahadhari za kawaida za kujikinga huku tukiendelea kuchapa kazi na kuendelea kuwaombea wenzetu huko wapate nafuu maana huwa tunategemeana.

Huu ni ule wakati wa kusema Mungu atupe nini waafrika weusi. Huu ni ule wakati wa Africa kuwa donor countries kwa wazungu.

Tusifuate mkumbo wa kujifungia nyumbani Kama wao wakati hali yetu sio Kama ya kwao. Mbona sisi wakati tukihangaika na tabu za njaa, wakimbizi, kipindupindu, HIV, TB, unyafuzi, Ebola, vita vya wenyewe kwa wenyewe wao wanaendelea kuchapakazi?

Naomba serikali ifungue shule na vyuo na kuruhusu watoto waendelee na masomo na wazazi wao waendelee na kuchapakazi huku wote tukiendelea na njia mbalimbali za kujilinda.

Kufa kufaana
Krg
Safi Sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom