Afrika hatarini kuwa masikini wa kutupwa asema kikwete | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Afrika hatarini kuwa masikini wa kutupwa asema kikwete

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by lifeofmshaba, May 20, 2011.

 1. lifeofmshaba

  lifeofmshaba JF-Expert Member

  #1
  May 20, 2011
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 868
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  RAIS Jakaya Kikwete amesema Bara la Afrika lipo hatarini kuwa masikini wa kutupwa kuliko mabara yote duniani ikiwa viongozi wake hawatapata mbinu mpya za kiuongozi za kukabiliana na matatizo.

  Baadhi ya changamoto alizozitaja Rais Kikwete ni mabadiliko ya hali ya hewa, umasikini, kasi ya ongezeko la watu, baadhi ya viongozi kutowajibika, uwazi na mabadiliko ya teknolojia; akisema mambo hayo yatalifikisha Bara hili pabaya yasipofanyiwa kazi.  MAONI YANGU: mimi nadhani hawa viongozi wetu wanafanya theory na mzaha wakati watu wanateseka kiukweli
   
 2. i411

  i411 JF-Expert Member

  #2
  May 20, 2011
  Joined: Mar 23, 2011
  Messages: 810
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 45
  Kwani hii ni habari mpya, kila mtu akipata cheo afrika hii anaona dollar Signs $ na kuzitafuta harakahara mwishowe wanabolonga kilakitu anabakia kuzitafuta hizo $$$ tuu kwa kufilisi mali ya uma. Mara atataka kagari, kwenda dubai or kuanzisha biashara basi list aiishi ndo ufisadi huo unavyojipalilia.

  Unajua nchi za wenzetu watu wakipata tuu habari na kaushahidi fulani ni fisadi au kapata mamaliyake kwa kukwepa kodi baaasi. wanaziwajibisha serekali zao kuzichukua hizo malizote za ufisadi. Mimi nashangaa mbona bongo mafisadi tunawajua na malizao hazichukuliwi na serikali inabakia ikisema tuu bila vitendo. Namakesi yao ya hapa na pale mahakamani zinatupoteza hela za serikali yetu ya mkopo na hizo kesi zinahairishagwa tuu mpaka faili na makaratasi yapotee na kesi imeisha. sasa nimaana gani kupeleka makesi yao mahakamani. Kama Mtikila atasoma hapa mimi naomba azitaje zile mali zilizopatikana kwa ufisadi na mafisadi na tuiwajibishe serikali iziuze ili ipate elayake ituendeleze wabongo. wanaweza uza magari na majumba yao yakifahari ya mafisadi na kujenga mashule angalau watoto wengine wanaosomea chini ya miti bongo hii wawe na future bora. Kipindi cha mvua hakuna shule jamani kwa wale watoto wanaosomaga chini ya miti, nihawa watoto wa taifa la kesho tunawatendea haki kweli manake nusu ya mwaka hawezi soma chini ya mti shule imefungwa mpaka mvua ziishe. hebu fikiria mtindo huu unajitolea miaka saba ya shule ya msingi unategemea kufika kweli…

  Serikali Mtu kama najulikana ni fisadi na kunautata basi si mnaweza mkafreeze hizo mali zake magari,elazake benki tuu mpaka atakapo tuhakikishia yeye si fisadi alafu mtampa malizake atakapotuondolea wasiwasi wetu wanchi. Siyo tunataabika tuu na mafisadi wanaendelea kupeta na kutucheka wakipita na matinted V8 yao.
   
 3. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #3
  May 20, 2011
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  shit,
  jamaa hajui kwa nini Tanganyika ni maskini afu
  anajidai kujua Africa inapo elekea?
  wizi mtupu,watakao chukua maneno yake sijui kama
  wana akili nzuri,...
   
 4. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #4
  May 20, 2011
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,227
  Likes Received: 1,414
  Trophy Points: 280
  Hii statement ya mkulu ni contradictory, aliwahi kukiri kuwa wa-tz ni maskini na hajui kwa nini ni maskini: sasa huo umaskini wa africa anasubiri uje mara ya pili?, the fact is Africa ni maskini kuliko mabara yote for decades. Anachopaswa kusema sasa ni mikakati gani ipo sasa ya kuiondoa africa katika janga hili na si kuleta utabiri.
   
 5. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #5
  May 20, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Afrika au Tanzania? Jk anacheza mchezo hatarishi, vita ya maneno! Ayasemayo ndio yako Tanzania!
   
 6. Manumbu

  Manumbu JF-Expert Member

  #6
  May 20, 2011
  Joined: Oct 28, 2009
  Messages: 1,751
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  usanii per excellence! yani hadithi zetu zile zileeee! Mungu hawa ndo viongozi tunaowaimba kwenye wimbo wetu wa Mungu Ibariki Tanzania? sitaki kukubali kama uwa unatulisikiliza asilani! Miaka yote hii ya kuimba? Tusingekuwa hapa na watu kama hawa
   
 7. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #7
  May 20, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,522
  Likes Received: 19,945
  Trophy Points: 280
  kwa hiyo sisi tufanye nini? kama mmeenda kupigana halafu baunsa mnayemtegemea kakimbia nyie wengine mfanyeje? si mtakimbia? huyu JK nyumbani kwake kunawaka
   
Loading...