Afrika hakuna demokrasia ya kweli

Feb 25, 2016
1
0
Kwa mwendelezo wa matokeo ya chaguzi mbalimbali barani Afrika, unadhani nchi zetu zinatenda demokrasia kama viongozi wake wanavyotamka?

mwanaharakati
 
Toka marekani aweke mkazo kwenye kupambana na ugaidi demokrasia afrika inakufa. Kuisimamia wenyewe hatuwezi. Trump yuko sahihi, tulitakiwa kutawaliwa kwa miaka 100 ndio tupewe uhuru. Tuna maneno mengi kuliko vitendo.
 
Huwezi kuwa mlafi, mbinafsi halafu ukajifanya una democrasia ya kweli, haya ni maigizo tu..........Africa bado tuna safari ndefu kufikia huko.
 
Mpo sahihi sana wakuu! Demokrasia (kama inavyohubiriwa kote duniani) haipatikani kokote duniani. Hiki kinachotudanganya USA kuna demokrasia pia ni usanii.
Uchaguzi uliomwingiza White House George W. Bush Jr. hasa kilichotokea Florida ni ushahidi tosha.
Pia tujiulize mazuri ya demokrasia ni kuchagua viongozi tunaowataka tu au inaenda mbali zaidi?
 
Kufuatia yanayojiri katika uchaguzi wa Meya wa Jiji la Dar-es-salaam,yaliyojiri katika uchaguzi wa Uganda hivi karibuni na katika nchi nyingine za kiafrika kama vile Burundi, Zanzibar na kwingineko, na nikiyarejea maneno ya aliekuwa Raisi wa Afrika kusini, P.W.Botha kuhusu Waafrika kujitawala wenyewe,nakuomba mwenyezi mungu kwa mamaka yako, lete "gharika" utuangamize wote katika bara hili ili waje waishi watu wenye rangi nyingine na sio sisi kwani tumekuangusha vya kutosha.

Nasisitiza,tumekuangusha vya kutosha na hatustahili kuwepo katika huu uso wa dunia.

Umetupa maliasili tumekuangusha,umetupa ardhi nzuri tumekuangusha,umetupa hali ya hewa nzuri kuliko mabara yote tumekuangusha, umetuepusha na matetemeko tumetuangusha. Sasa kwa kushindwa kote huku, tuna uhalali gani wa kuendelea kuwepo?
 
Kufuatia yanayojiri katika uchaguzi wa Meya wa Jiji la Dar-es-salaam,yaliyojiri katika uchaguzi wa Uganda hivi karibuni na katika nchi nyingine za kiafrika kama vile Burundi, Zanzibar na kwingineko, na nikiyarejea maneno ya aliekuwa Raisi wa Afrika kusini, P.W.Botha kuhusu Waafrika kujitawala wenyewe,nakuomba mwenyezi mungu kwa mamaka yako, lete "gharika" utuangamize wote katika bara hili ili waje waishi watu wenye rangi nyingine na sio sisi kwani tumekuangusha vya kutosha.
Unakufa lini tusherehekee!!!
 
hahaha pole sana kamanda, hiyo ndo afrika, but ukitaka kuishi kwa amani na furaha katka bara hili la laana, sharti ni kuwa jitoe akiri yaan usijihusishe sana na mambo ya siasa, kuwa interested na vitu vingine kama vile music, movies and so on. but siasa kwa afrika bado mno.
 
Kwa mwendelezo wa matokeo ya chaguzi mbalimbali barani Afrika, unadhani nchi zetu zinatenda demokrasia kama viongozi wake wanavyotamka?

mwanaharakati
Ulaya wangekuwa na Demokrasia wangekuwa wanapindua wazalendo wa Afrika? Palipo na mapigano popote duniani kuna mkono wa mtu mweupe akisaidia upande wenye maslahi kwake na kuuza silaha. Hiyo ndio demokrasia?
 
Back
Top Bottom