Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,010
- 9,875
Shirika la afya duniani (WHO) limeonya kuwa Afrika haiwezi kuhimili wimbi la pili la Covid-19, likisema kuwa litakuwa na athari kubwa hususan za kiuchumi.
Onyo hilo linatolewa wakati maambukizi yakiendelea kuongezeka katika nchi nyingi ambazo zililegeza sheria za kupambana na maambukizi hayo hivi karibuni.
WHO linasema virusi havitaweza kudhibitiwa kama Mataifa ya Afrika yataendelea kufungua shughuli zake bila kuweka tahadhari za kuzuia maambukizi ya virusi vya Corona.
Imeonya pia juu ya kurejea kwa vipindi vya amri za kutotoka nje ambazo inasema Afrika haiwezi kuvihimili.
Mkurugenzi wa WHO kanda ya Afrika, Matshidiso Moeti, pia amesema hatua zimewekwa kuhakikisha bara hilo linapata sehemu yake ya chanjo yoyote inayotengenezwa.
Afrika imeripoti zaidi ya visa milioni 1.6 vya virusi vya corona tangu mlipuko huo ulipoanza huku watu 39,000 wakifa kutokana na maradhi hayo.