Afrika haitamsahau “baba wa mpunga chotara”Yuan Longping

ldleo

Senior Member
Jan 9, 2010
177
250
1FFB7EEA-3EA0-4435-9193-B2ECF3AD56AB.jpeg

“Kuwanufaisha watu wote wa dunia ni moja ya matumaini yangu ya maisha.”“Baba wa mpunga chotara” (yaani hybrid rice) Yuan Longping alisema hayo alipoulizwa kwa nini amehimiza upandaji wa “mpunga chotara” barani Afrika.

Katika mkutano wa kwanza wa wakuu wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika FOCAC uliofanyika mwaka 2006, China iliahidi kujenga vituo 10 vya vielelezo vya kilimo vyenye umaalum barani Afrika. Mwaka huo, kwa mara ya kwanza Yuan Longping aliongoza timu yake ya mpunga chotara kwenda Madagascar, na kuanza juhudi zake za kuzisaidia kilimo Afrika kwa miaka 15.

Wakati ule, uzalishaji wa mpunga chotara nchini Madagascar ulikuwa ni tani 2.5 tu kwa kila hekta,lakini sasa umeongezeka mara zaidi ya tatu na kufikia tani 8 kwa kila hekta. Uzalishaji wa mpunga chotara wake pia ni mara moja hadi tatu zaidi ya mipunga ya aina za nchi hiyo.

Kutoka kuitwa“mpunga shetani” hadi sasa kuitwa “tsarabe”-kitu kizuri katika lugha ya kienyeji ya Madagascar, na pia kuchapishwa katika noti ya Ariary ya Madagascar toleo jipya yenye thamani ya elfu 20, mpunga chotara wa Yuan Longping umewawezesha watu milioni 25 kujitosheleleza kwa chakula. Hivi sasa mbali na Madagascar, mpunga chotara wa China unapandwa na kupata mavuno mazuri katika nchi 16 za Afrika.

Lakini kwa bahati mbaya, labda Mungu hataki aendelee kuchoka namna hiyo, tarehe 22, Mei mchana kwa saa za Beijing, Yuan Longping anayezingatia usalama wa chakula wa Afrika aliaga dunia akiwa na umri wa miaka 91. Yuan Longping alizaliwa katika zama zenye machafuko, alishuhudia njaa na mateso mengi, kwa hivyo aliamua kuondoa kimsingi mzizi wa tatizo la kukosa chakula. Na ametumia maisha yake yote kujizatiti kwenye utafiti wa mpunga chotara.

Baada ya Yuan kufanikiwa kutafiti mpunga chotara na kuhimiza upandaji wake, wachina hawakosi chakula tena na kumbukumbu kuhusu njaa pia imekuwa historia. Kwa China inayochukua asilimia 20 ya watu wote duniani, kujitosheleza chakula kunahesabiwa kuwa mchango mkubwa kwa dunia nzima. Hali kadhalika, kama Afrika ya leo inaweza kulinda usalama wa chakula, basi msukosuko wa chakula duniani tayari umetatuliwa kwa kiasi kikubwa.

Katika semina ya maendeleo ya ushirikiano wa kilimo kati ya China na Afrika iliyofanyika mwezi Juni mwaka 2019 wakati wa Maonyesho ya kwanza ya Uchumi na Biashara ya China na Afrika mkoani Hunan, Yuan Longping aliwaambia washiriki kutoka nchi mbalimbali za Afrika kuwa “sio tu China ina usalama wa chakula, nchi za Afrika pia zinatakiwa kuwa nao, ni lazima tufanye ufundi wa mpunga chotara uote mzizi barani Afrika.”Yuan Longping aliahidi kuwa kila mwaka China itatuma wanasayansi vijana kwenda nchi husika za Afrika na kutafiti upandaji wa mpunga chotara.

Ingawa Yuan aliaga dunia, lakini naamini kutokana na kupokezana vijiti na wataalam wa kilimo wa China vizazi baada ya vizazi, na kusaidia nchi za Afrika kuendeleza kilimo na mpunga chotara, ipo siku, kama wachina, waafrika pia tutaweza kujaza bakuli zetu zote kwa chakula. Nchi yoyote yenye nguvu kubwa zaidi duniani ni ile inayoweza kuhakikisha usalama wa chakula kwa watu wake.

Balozi wa Tanzania nchini China Mbelwa Kairuki akituma pole zake kwa wachina kufuatia kifo cha Yuan Longping, alimtaja kama shujaa wa chakula na mchangiaji muhimu wa jamii ya kimataifa yenye hatma moja.

Amesema kwa kupitia utafiti wake wa kisayansi katika kuanzisha uzalishaji wa mpunga chotara,Yuan Longping amesaidia mamilioni ya watu duniani kuondokana na njaa ikiwemo barani Afrika.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom