Afrika haitakuwa kwenye hali mbaya dhidi ya Covid-19

moyafricatz

JF-Expert Member
Nov 27, 2015
2,900
4,865
Napenda kuwajibu hao wanaosema kuwa Africa tutakuwa katika hali mbaya zaidi kuliko hata Italy, France na Germany.*

Ni nani asemaye neno na likatimia ikiwa Bwana hakuliagiza? MAOMBOLEZO 3:37-38

1. Usisahau kuwa ni katika Africa ambapo Mungu alimtajirisha Abraham (Misri)

2. ISAKA alitembelea Africa na akabarikiwa.

3. Ni katika Africa ambapo Yakobo alikimbilia akabarikiwa wakati dunia nzima ilipigwa na njaa.

4. Ni katika Africa Yusufu aliinuliwa na kuwa waziri mkuu (Misri)

5. Ni katika Africa ambako wana wa Israel walipona na mapigo ya Mungu yaliyowapata dunia nzima.

6. Ni katika Africa ambako Musa alizaliwa na akawa mkuu sana ili kuwaokoa wana wa Israel


7. Ni katika Africa ambako wana wa Israel walibeba (mali) fedha, dhahabu na vito vya thamani ili kujengea hema ya kukutania

8. NI KATIKA AFRICA AMBAKO MKOMBOZI WETU *YESU* ALIPATA KIMBILIO WAKATI HERODE ALIPOTAKA KUMUUA AKIWA MTOTO MCHANGA. *Africa ni sehemu ya Makimbilio.*


9. Bwana Yesu alipokuwa akielekea kusulubiwa, ni Mtu Mwafrica (Simon wa Kirene) aliyemsaidia kuubeba msalaba. ( *Africa imeugusa msalaba* )


Ninapinga na kukataa kila neno baya linalotamkwa dhidi ya Africa. Kwa jina la Bwana Wetu Yesu Kristo Aliye Hai.

Wazungu wanamahospitali makubwa yaliyojaa kila aina ya dawa, lakini *AFRICA TUNAYE MUNGU MWEZA WA YOTE *

*ZABURI 91: 1.7* Mabaya hayatakupata, wala tauni haitakaribia katika hema yako

*EXODUS 23:25.* Nanyi mtamtumikia BWANA, Mungu wenu, naye atakibarikia chakula chako, na maji yako; nami nitakuondolea ugonjwa kati yako.

*Isaya 60:2* Tazama giza litaifunika dunia, na giza kuu litafunika kabila za watu bali Bwana atakuzukia wewe. Utukufu utaonekana juu yako.

Zaidi ya yote tufuate maelekezo ya serikali bila kuyapuuza na tuishi kwa tahadhari. Na pia usipoze imani kwa Mungu wako

Ukiamini haya basi sambaza kwa wengine ili washuhudie uweza wa MUNGU WETU

Ubarikiwe sana mwana wa MUNGU
 
Kama nyuzi za JF au maoni ya watu yangekua yanazuia corona, basi kirusi hicho kingeshatokomezwa duniani. Tusubiri muda si mrefu ukweli utajulikana tu.
 
hakika umenena vyema. Na hawa wanaoendelea kufikiri Africa itapata madhara kama waliyoyapata wao watushuhudia kitu ambacho hawakutegemea kukiona. Pia na nyinyi ambao mpo Africa halafu mnaombea mabaya Africa mtapotea wenyewe japo naomba Mungu awatunze muone neema yake juu ya Africa.
 
Mambo haya ni magumu kwa akili za kibinadamu, ila imani tu inahitajika kwa sasa tuwe na tahadhari na tuzidi kumuomba Mungu, tutavuka tu.
 
Habari za Jioni wana Jukwaa!!

Ninalo jambo la kuwaambia kuwa zipo sababu kadhaa za kuzingatia hasa kipindi hiki cha Corona
Africa kwenye theology inaonekana kuupa support kubwa Ukristo support; Leo nitatotoa mifano kadhaa

Moja, baraka nyingi za Ibrahimu, Isaka ba Yakobo walizipatia au waritajirikia Africa

Mbili, Musa alipata Elimu Africa (Misri)

Tatu, Yakobo na familia yake yaani wana wa Israel kipindi cha Njaa waliponea Africa

Nne, Yesu alipozaliwa mfalme alipotoa Amri ya kuuwawa kwa watoto wote wenye umri chini ya miaka 5 alipona alipokimbilia Africa

Mwisho na ndio yenye Mashiko kwa siku ya Leo ya Pasaka, Yesu Kristo alipokuwa anaenda kusulubishwa Goligota, Msalaba ulipokuwa mzito na mateso Yusuph Mkrene alimsaidia Msalaba mpaka goligota. That means, kwenye mateso ya Yesu waafrika tulimsaidia Yesu mwana wa Mungu ambae ndie Aliefufuka.

Kwa maneno haya, Corona haitapiga Africa kama walivyopigwa hao jamaa. Na ukitaka kujua hilo angalia trend na jinsi tulivyo na cautions ndogo lakini Corona haijatugalagaza kama ilivyowagalagaza Ulaya na Marekani na China

Bwana Yesu atatuvusha salama Sisi waafrika hawa jamaa na takwimu zao watapotelea mbali.

Kila atakaeliitia Jina la Yesu ataokolewa. Tuombe tuchukue tahadhari kaugonjwa kenyewe haka ni kadogo sana

Heri ya Pasaka!!
 
acheni kujidanganya, Africa watakufa watu wengi sana ndani ya miezi 3 ijayo,kama Europe na ubora wao wa huduma za afya ila wanakufa maelfu sembuse Africa ambapo mtu hana hata pesa ya panadol !!!
America wamekufa watu 2000 ndani ya saa 24 , licha ya kuwa na medical staff na medical facilities za kutosha
 
Kwa ulichoandika hapo wewe ni moja ya matahira wa Afrika!
Tahira anaweza kusurvive kwenye hili janga kuliko werevu
USA na werevu wao wanawaka na akili zao. Mi naomba Yesu atuponye akili za waganga na matabibu zimeshachemka
Hata hawa tunaowaona vichaa waliopo duniani wana cautions gani wanazochukua dhidi ya Corona??
Ila umeshawahi kuona kichaa kaugua Corona kama sio 'nyie mnaojiita na kujiona mnazo akili'?
Nakubaliana na mawazo ya serikali tuombe Mungu atatuvusha haya majanga hayatatupata kwa jina la Yesu
Tuseme wote Amen!!!
 
acheni kujidanganya, Africa watakufa watu wengi sana ndani ya miezi 3 ijayo,kama Europe na ubora wao wa huduma za afya ila wanakufa maelfu sembuse Africa ambapo mtu hana hata pesa ya panadol !!!
America wamekufa watu 2000 ndani ya saa 24 , licha ya kuwa na medical staff na medical facilities za kutosha
Mkuu tuliambiwa mpaka tarehe 15.04.20 tutaambukizwa kama watu buku
Kiko wapi?? Wanadamu sio Mungu bhana
Tuendelee kuomba Yesu Kristo atatuvusha salama. Wewe amini tu hata na familia yako itavushwa salama Kristo ni habari nyingine. Rais ameshasema tunakakemea kwa jina la Yesu kakorona kulee.
Hapa ndio unaona haja ya kuwa na Rais Mcha Mungu
 
Mkuu tuliambiwa mpaka tarehe 15.04.20 tutaambukizwa kama watu buku
Kiko wapi?? Wanadamu sio Mungu bhana
Tuendelee kuomba Yesu Kristo atatuvusha salama. Wewe amini tu hata na familia yako itavushwa salama Kristo ni habari nyingine. Rais ameshasema tunakakemea kwa jina la Yesu kakorona kulee.
Hapa ndio unaona haja ya kuwa na Rais Mcha Mungu
Acheni ubaguzi, tukemee kwa Jina la Mtume Muhammad pia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom