Afrika haipaswi kuwa uwanja wa mapambano ya Vita Mpya Baridi

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,010
1,032
Wakati mvutano kati ya China ukiendelea kutokea, bara la Afrika linatajwa kuwa uwanja mpya unaotumiwa na Marekani kuishambulia China. Marekani imekuwa ikishambulia nakukosoa ushirikiano kati ya China na Afrika, na kujaribu kutumia fursa mbalimbali kuupaka matope ushirikiano kati ya China na Afrika, na hata baadhi ya wakati kuonekana kama ni uchonganishi.

Kutokana na Marekani kutekeleza sera zake za kuzipuuza nchi za Afrika, na China kuwa na mahusiano ya karibu na nchi za Afrika, ni wazi kuwa uwepo wa China kwenye nchi za Afrika ni mkubwa kuliko ule wa Marekani. Kuna mifano mingi ya ushirikiano wa karibu kwenye sekta za uchumi, biashara na hata ujenzi wa miundo mbinu. Mfano mmoja ni mpango wa “Ukanda mmoja, njia moja” (Belt and Road Initiative) ambao umepokelewa vizuri na nchi nyingi za Afrika, na kusaidia kwenye ujenzi wa miundo mbinu kama reli, barabara na bandari.

Lakini ushirikiano huu pia umeonekana kuwa namanufaa kwa Afrika wakati wa majanga na changamoto mbalimbali kama vile ugonjwa wa Ebola katika nchi za Afrika Magharibi, ilivyotokea kimbunga cha Idai kilichotokea katika eneo la pwani ya kusini mashariki mwa Afrika, na hata wakati huu wa COVID-19. Kwa hiyo ushirikiano kati ya China na Afrika licha ya kuwa una changamoto zake, ni wazi kuwa umekuwa na manufaa kwa nchi za Afrika.

Hata hivyo tukiangalia hali halisi ya nchi za Afrika kwa sasa, Marekani ni rafiki wa nchi za Afrika kutokana na sababu za kihistoria, kisiasa, kiuchumi, lakini pia China ni rafiki yetu kwa sababu kama hizo hizo. Na tukumbuke kuwa nyingi za Afrika ni nchi huru na wanachama wa harakati ya nchi zisizofugamana na upande wowote, ndio maana nchi zote mbili ni rafiki zetu.

Ni wazi kabisa kuwa sera ya Marekani kwa sasa imeiweka Afrika pembezoni kabisa, na rais Trump amekuwa akitumia hata lugha chafu kuzitaja nchi za Afrika. Lakini ni wazi pia kuwa serikali ya Rais Trump ina uhasama na serikali ya China, na sasa tumezoea kuwa kila Rais Trump au waziri wa mambo ya nje wa Marekani anapoongea, wanatumia fursa hiyo kuipaka matope China.

Ni vizuri ikikumbukwa kuwa wakati wa vita baridi kati ya nchi za kambi ya mashariki (Warsaw Pact) na kambi ya nchi za Magharibi (NATO), nchi nyingi za Afrika zilichaguakutofungamana na upande wowote. Kama Marekani inazusha sasa vita nyingine baridi, basi ijue kuwa hasimu wake ni hasimu kwake, na sio hasimu wa wengine.
 
Back
Top Bottom