Infantry Soldier
JF-Expert Member
- Feb 18, 2012
- 15,893
- 16,317
Shikamooni wakubwa zangu wote wa hapa Jamiiforums. Mimi mdogo wenu (Last Born) Infantry Soldier nipo mzima kabisa wa afya. Thanks to God the Almighty.
Ndugu zangu watanzania eti;
Were there xenophobic attacks against black foreigners or there was diplomatic/political standoff between SOUTH AFRICA and NIGERIA?
Nimeamua kuuliza hivi kwa maana kwamba;
Mnamo mwanzoni mwa mwezi wa September mwaka jana 2019, vurugu mpya kabisa zilianza tena dhidi ya wageni waishio katika baadhi ya maeneo nchini Afrika ya Kusini.
Makumi ya watu waliuawa baada ya makundi ya watu wenye msimamo mkali kuvamia, kuiba na kuchoma moto maduka pamoja na magari katika maeneo kama Pretoria na Johannesburg.
Raia wa kutoka nchini Nigeria, ambao ndio waafrika wenye idadi kubwa waishio nchini humo, walikuwa miongoni mwa wahanga wakubwa waliolengwa katika mkasa huo.
Police wa Afrika ya Kusini walikamata watu wapatao 700 kutokana na vurugu hizo, habari ambazo zilisambaa ulimwenguni kote.
Raia kutoka katika mataifa mbalimbali walibeba vitu vyao na kuondoka nchini Afrika ya Kusini, miongoni mwao kulikuwa na raia takribani 600 kutoka nchini Nigeria, waliopanda ndege kwa gharama zao binafsi.
Hasira dhidi ya vurugu hizo zilitapakaa Afrika nzima na kisha Nigerians wakaamua pia kuchoma moto, kuiba na kushambulia Supermarkets kubwa zinazomilikiwa na raia wa South Africa pamoja na matawi ya kampuni ya mawasiliano ya MTN katika miji ya Lagos na Abuja.
OUR MOTTO: USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.