MK254
JF-Expert Member
- May 11, 2013
- 31,746
- 48,385
Yaani wanafunzi wanasubirishwa nje ili kundi la kwanza likamilishe somo kwenye ratiba yao, hii Afrika tumechelewa kweli maana siamini mambo kama haya yanatendeka kwenye karne hii miaka mingi sana tangu mkoloni aondoke. Vipau mbele hamna, utakuta wakulu wanasafiri kwa magari ya kifahari kwenye misafara hadi raha.
========
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Aboubakar Kunenge jana Jumanne Januari 6 amesema wanafunzi waliofaulu kuingia kidato cha kwanza mwaka huu watasoma kwa zamu kutokana na uhaba wa vyumba vya madarasa katika mkoa huo.
Akizungumza wakati wa ziara ya kukagua maandalizi ya shule kwa ajili ya wanafunzi hao, Kunenge amesema wamefikia hatua,ili wengine wasibaki nyumbani na itakapofika Februari 28,2021 wataendelea na utaratibu wa kawaida.
Kunenge amebainisha kuwa Tayari uongozi wa Mkoa umeomba kibali wanafunzi wote kuanza kwenda shule japo kwa zamu kutokana na uhaba wa madarasa ambapo wataanza Januari 11, 2021.