Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Afrika, baba mbaya.

Discussion in 'International Forum' started by Mwelewa, Oct 20, 2012.

 1. Mwelewa

  Mwelewa JF-Expert Member

  #1
  Oct 20, 2012
  Joined: Jan 5, 2011
  Messages: 1,412
  Likes Received: 976
  Trophy Points: 280
  ♥ AFRIKA ♥
  Ni nani asiyekufahamu AFRIKA?
  Ni nani asijekutaja jina lako AFRIKA?
  Pengine wapo ila ni wachache. Unajua kwa
  nini? Leo nitakuambia AFRIKA.
  Ila kabla sijakuambia naomba tukuliane kwa mambo mawili.
  Mosi, unihakikishie usalama wangu.
  Pili, unisokilize hadi mwisho.
  Nakwambia haya kwa sababu tabia yako
  AFRIKA.Tabia yako ya Kigeugeu
  unayoijenga kwa juhudi za mikono yako mwenyewe.
  Umekuwa mtu wa kuua wasio na hatia eli
  unawaaita wahuni waende wakajifunze
  adabu kwa mama zao. Umesahau kuwa
  wewe ni baba.
  Usichoke, endelea kunisikiliza AFRIKA. Juzi nilishangazwa na taarifa kuwa eti
  unakua kiuchumi kwa asilimia sita.
  Nikajiuliza na "watoto wa kitaa" nao
  wanakua kwa wastani huu. Kukua kwa
  maana ya kupata sehemu bora kwa ajili ya
  malazi bila kusahau "msosi". Unatudanganya sana AFRIKA.
  Nakumbuka wakati naanza chuo, mwaka
  wa kwanza uliniita "NON-PRIORITY". Eti
  sina sifa za kupata "Loan" ila nina sifa za
  kusoma elimu ya juu.
  Haina "noma" AFRIKA. Umeaamua kugeuza juhudi za mama zetu wapendwa
  kuwa mtaji wa vimada wako huko
  unapokujua mwenyewe.
  Vita, chuki, dhuluma na ubabe ndio sifa
  zako siku hizi. Eti unamfanyia ubabe
  Daudi Mwangosi, ukiwa umebeba mabomu na maji ya kuwasha.
  Haina "kweree bhana" si unaniona mi
  muhuni tu. Sina lolote na kamwe sitofua
  dafu mbele ya virungu vya wale "majamaa"
  FFU.
  Matajiri wa " Uchina" wanakutamani mno. Na lazima watakupata tu. We ni wabei
  ghali ila unajiuza kwa dhamani ya kutupa.
  Wakati watoto wako wanalia njaa, wewe
  umekuwa mtu mnyonyaji na mporaji wa
  wanyonge AFRIKA.
  Ni nani kakuroga AFRIKA? Inamaana hauwezi kubadilika AFRIKA? Najua wewe
  si msikivu. Ila kwa hili naomba nisikilize.
  Acha rushwa, acha "undumilakuwili"
  AFRIKA. Uache tena kwa dhati. Huku
  ukidumisha siasa safi na utawala bora.
  Naomba nimalizie kwa hili AFRIKA, yaliyopita si ndwele, tugange mapya.
  CHANZO CHA MATATIZO YAKO NI
  WEWE MWENYEWE AFRIKA.
   
Loading...