africa's highest mountain lies in Tanzania but the best view is from Kenya

Semilong

JF-Expert Member
Mar 5, 2009
1,712
219
8324_129651618172_63782793172_2649125_3353208_n.jpg


soma 27 mountain view
africa's highest mountain lies in Tanzania but the best view is from Kenya...
je ya kweli haya.....
wizara yetu ya utalii inautangaza vipi huu mlima???
 
..nadhani watalii wengi wanapenda kupanda mlima na siyo kuuona tu.

..pia kuna eneo la kusini mwa Tanzania ambalo vivutio vyake vya utalii havijatangazwa vya kutosha.

..tuache kufikiria Norther Circuit[Kilimanjaro,Serengeti,Ngorongoro,Manyara], tuitangaze Southern na Western Circuits ambako kuna Selous,Katavi,Gombe,Mikumi,Saadani, bila kusahau MAFIA.

..binafsi nadhani tukitangaza vivutio vya Tanzania, na Kenya wakatangaza vya kwao, nina hakika mtalii makini atachagua kutembelea Tanzania.

..tatizo letu hatujitangazi vya kutosha.

NB:

..unaweza hata kuchombeza kwamba Kenya ni more expensive wakati wana vivutio kidogo.
 
8324_129651618172_63782793172_2649125_3353208_n.jpg


soma 27 mountain view
africa's highest mountain lies in Tanzania but the best view is from Kenya...
je ya kweli haya.....
wizara yetu ya utalii inautangaza vipi huu mlima???

Kiongozi mzalendo pekee wa Tanzania alikuwa Nyerere. Hao wengine wote ni wazalendo wa matumbo yao! Ni Nyerere aliyepandisha bendera ya taifa na mwenge (kupitia marehemu Kapteni Nyirenda) kwenye mlima Kilimanjaro mara baada ya uhuru baada ya kuona kuwa wakenya wanadai kuwa mlima huo uko Kenya. Niliwahi kukutana na mwanafunzi mmoja wa Kenya aliyekuwa anasomea shahada ya Uzamivu (PhD) akadai kwamba wakati yuko shule ya msingi hadi sekondari alifundishwa kwamba mlima Kilimanjaro uko Kenya. Hawa mbumbumbu wa Wizara ya Utalii wanaendeleza bila kujijua kile ambacho wakenya wengi wanakiamini! Kwani ni lazima kutaja kwamba best view iko wapi? Kutaja mlima Kilimanjaro uko Tanzania haitoshi mpaka Wakenya nao wasaidiwe kutangaza mlima huo?
 
Buchanan,

..unajua tatizo letu Watanzania ni kuleta siasa kwenye masuala ya biashara na ushindani.

..hizi habari kwamba the best view ya mlima Kilimanjaro iko Kenya nimewahi kuisoma kwenye matangazo ya biashara ya tourist agents.

..Watanzania tunashindwa kwenye vita hii ya matangazo ya vivutio vya utalii kwa kutegemea serikali itafanya kila kitu, au itaweza kupambana na ma-tourist agents wa Kenya.

..tuachane na siasa. wakati Capt Nyirenda anasimika ile bendera Kilimanjaro Kenya ilikuwa haijapata uhuru. pia alisimika bendera ile kama tendo la kisiasa na halikuwa na mahusiano yoyote yale na utalii au biashara.
 
Tukiongeza bidii ktk matangazo najua tutashinda na sasa hivi tunaendelea kufanya vizuri cha msingi ni kuongeza bidii ktk kutangaza vivutio tulivyo navyo.
 
hayo mambo ya the best view sijui nini ni propaganda zisizo na maana, na usikute ni mtanzania anaeneza hizo propaganda hata akiwa nje ya nchi, jamani tubadilike tuitangaze nchi yetu.
 
JokaKuu, nashukuru kwa mchango wako ila niliona kitendo cha kupandisha bendera na mwenge kilikuwa na maana kwa Tanzania. Haijalishi kama Kenya ilipata uhuru au la maana wakenya walikuwa na maoni yao kuhusu mlima Kilimanjaro hata kabla ya uhuru wa Kenya! Pia mambo ya kibiashara huwa yanaanzia kwanza kwenye siasa kwa kuweka sera, kwa hiyo usije ukafikiri kwamba siasa inaweza kutenganishwa na biashara kwa asilimia mia moja!
 
ila ufisadi unatukatisha tamaa kujivunia utajiri wetu.

Mimi nafikiri tuwe wazalendo hata iweje! Huu ufisadi utaisha taratibu. Kama tukifanya haraka maana yake yanahitajika mapinduzi ya kijeshi, kisha baada ya mapinduzi ni kuwakamata mafisadi wote na kuwapelela mahakamani ili sheria ichukue mkondo wake! Kwa kuwa njia hiyo ina repercusions zake, njia hii inayotumika sasa inafaa na uzalendo wetu ndio utakaoutokomeza ufisadi!
 
Buchanan,

..hii posting yako ya pili imenipa mwangaza wa kujua nini unachoongelea.

..binafsi nadhani tuna vivutio vingi na vizuri zaidi ya Kenya.

..tuendelee kusisitiza kwamba mlima uko Tanzania na the best view is in Tanzania.

..pia tutangaze vivutio vyetu vilivyoko kusini na magharibi ya Tanzania.
 
hayo mambo ya the best view sijui nini ni propaganda zisizo na maana, na usikute ni mtanzania anaeneza hizo propaganda hata akiwa nje ya nchi, jamani tubadilike tuitangaze nchi yetu.

Yaani ukiambiwa watz tumekula usingizi, ujue ni usingizi wa pono kuhusu what's best for our country! Hii habari ya best view ndio usemi wa wakenya wanapozungumzia mlima Kilimanjaro. Watanzania kwa uvivu inawezekana wame-copy and paste hiyo statement toka kwenye advertisement ya wakenya kuhusu mlima Kilimanjaro!
 
Yaani ukiambiwa watz tumekula usingizi, ujue ni usingizi wa pono kuhusu what's best for our country! Hii habari ya best view ndio usemi wa wakenya wanapozungumzia mlima Kilimanjaro. Watanzania kwa uvivu inawezekana wame-copy and paste hiyo statement toka kwenye advertisement ya wakenya kuhusu mlima Kilimanjaro!
buchanananana
soma hapo 27 mountain view
hapo ndio hiyo statement imetoka, na nimekuonyesha hapo juu sasa sijui wewe unalalamika nini
soma thread kwanza na sio kurukia copy-paste tuu
 
Wakuu mi napenda sana hii integration ya mataifa ya East Africa. Lakini Iam really getting tired na hii atitude ya wakenya kupenda 'kununua kesi" Unajua ni vitu vya kijinga kijinga kama hivi vinawafanya watanzania wasiwaamini hawa jamaa. Yaani..old habits die hard kwa kweli..hawa jamaa wanapenda drama sana..sijui kwa nini..kwa akili yao wanaona huu ni ujanja wa hali ya juu..ila wanashindwa kuelewa..whatever happens..Kilimanjaro..hata ikiwa kichuguu ni mali ya wabongo...

Why enlist Kilimanjaro..unajua kabisa hata TZ macho yao yako hapo..harafu mlima ni wa watanzania perse...and yet our friends are doing..exactly the opposite kupromote mlima eti unaonekana vyema ukiwa kwao..and you expect Tanzanians to like you?????

I wish wakenya wangejua hizi simple mathematics za kuishi na watu bila drama..I dont know..labda mi ndo sielewi..lakini naona hawa jamaa..hawako serious kuishi na majirani zao vyema...

I always like Kenyans..lakini hawa jamaa zetu wanajisahau sana..wakiona watu wako kimya wanadhani wote ni wajinga..si kweli...Let them learn to live with people. Siyo kila mtu mkimya ni mjinga.

Masanja,
 
hayo mambo ya the best view sijui nini ni propaganda zisizo na maana, na usikute ni mtanzania anaeneza hizo propaganda hata akiwa nje ya nchi, jamani tubadilike tuitangaze nchi yetu.

Tunambiwa wafrika ni ndugu sasa nduguyako akisifia chako kuna ubaya gani ?
 
mlima uko nchini kwetu lakini wakenya wanafaidika zaidi yetu sisi kisa nini? jamaa wanaautangaza kushinda sisi na sio kosa lao kosa ni letu.serikali haikuwa makini sana kujitangaza toka mwanzo kwa vile hakuna rushwa kwenye kutangaza vivutio vya nchi.hakuna kiongozi aliyeona umuhimu wa kutangaza utalii nje kwa vile hawawezi kufaidika wao binafsi,faida inaenda moja moja kwenye pato la taifa ndio maana viongozi hawakujali.mambo ya madini yale ndio wanaangaika kusaini mikataba mpaka nje ya nchi huko kwa vile ulaji unaingia moja kwa moja tumboni kwa mtu.
tushukuru tu sasa hivi tumepiga kelele ndio maana matangazo yanarushwa na ushindani wa wakenya ndio umesaidia serikali yetu kuamka na kuona umuhimu wakutangaza vivutio vyetu la sivyo kazi ya kutangaza angepewa "kingunge" na kuambiwa asilimia 50 ya mapato kwenye utalii achukue yeye lol hivyo ndio jinsi serikali ilivyokuwa imejaa wavivu wa kufikiria na kutenda kazi.
 
unajua ukiona mtu anatangaza hadharani kuwa mke wako ni wake hii hatari sana lazima uogope na ufikirie kuchukua hatua... HATUA GANI?!!! Huenda serikali ya kenya ina mpango na huo mlima!! mbona hawakanushi?..anyway business.. lakini na sisi sio kilimanjaro tu mbona na hizo site zingine hatutangazi tatizo liko wapi??
 
Lakini ukweli hata hivyo ni kwamba muonekano mzuri ni kutokea upande wa Kenya. Wengi wetu ni mashahidi.

Kigoma, kusini n.k kuna vivutio kibao. Kinachotakiwa ni koboresha miundo mbinu na kujitangaza.
 
Oyaa wakuu hakuna haja ya kupaniki mimi nipo ughaibuni, na the easiest way ya kuelezea where I come from ni kutaja mlima huu. Discovery channel has done alot to unfold the so-called in Kenya, Mt Kili and the giant Serengeti! At last many ppl they know and it is for sure kwamba hivi vbitu viko Tz. I even spoke to a grade 11 kid who is taking Geography and she could easily tell me Mt Kili is in Tz. Nadhani Jmaa zetu wamegundua iot is a hard sell these kusema Kili ipo kwao ndio maana wwanakuja na matangazo ya dizaini hii!!!!!!!!
 
Back
Top Bottom