African Union Vacancies

Status
Not open for further replies.
Nadhani kuna haja ya kutafuta sababu ni kwa nini kuna watanzania wachache sana kwenye AU na UN. Najua kuwa sababu moja ni umaimuna, na wasio maimuna wanajua lugha moja tu, any other reasons?
 
Invisible Congrats kwa kuziweka hizo nafasi.......yaani umeniwahi, ilikuwa niziweke leo leo........lets keep this good spirit
 
Nadhani kuna haja ya kutafuta sababu ni kwa nini kuna watanzania wachache sana kwenye AU na UN. Najua kuwa sababu moja ni umaimuna, na wasio maimuna wanajua lugha moja tu, any other reasons?

Upo uwezekano wa umaimuna, lakini hii yaweza kuwa sababu ndogo sana. Tanzania tunao wasomi wengi na wa hali ya juu sana ukilinganisha na nchi zingine za magharibi.

Wasomi wengi wa kitanzania hawakujua umuhimu na maslahi ya kufanya UN hadi miaka ya karibuni hususa mwishoni mwa miaka ya tisini na hasa baada ya mahakama ya Rwanda pale arusha kuanzishwa. Leo tunao watanzania wengi sana wako kwenye mission mbali mbali ulimwenguni kote ambao wameajiriwa kati ya 2000 na 2007

Sababu nyingine ni kwamba kazi nyingi za UN ni za kujuana zaidi, wenzetu wa Africa magharibi na kwa kiasi Kenya walitutangulia huko, hivyo kila nafasi zilipotokea walichomekeana kinamna na wakazipata. wakenya wao walifaidika sana na uwepo wa shirika la Makazi pale Nairobi.

Wakati fulani, mkuu wa uajiri pale UN ICTR aliulizwa kwa nini alipendelea sana kuajiri wakenya hata kwa nafasi ambazo watanzania wanaweza. jibu lake lilikuwa Tanzania hakuna Wasomi. jambo hili lilipingwa sana na kwa bahati nzuri interview nyingi zikaandaliwa na UNDP DSM na matokeo yake alikubaliana kwamba Tanzania tunao wasomi wa kutosha na si wa kubeza hata kidogo.

Kujua lugha moja pia inaweza kuwa sababu, lakini hai affect sana. asilimia kubwa za ofisi/mission za UN ni za Kiingereza na mara nyingi kwenye matangazo yao huweka Lugha nyingine kama additional advantage but si lazima sana.

Sababu nyingine pia ni kwamba wale wanaobahatika kupata kazi UN hawajishughulishi kuwapa habari au kuwatafutia watanzania wenzao ukilinganisha na nchi zingine hususa za Magharibi.

Kiutendaji kwa wale wanaofanya kazi UN watakubaliana na mimi kwamba Watanzania kwa kazi si wababaishaji hata kidogo. kila mahali ambako kuna mtanzania kuna sifa tele zinazotuwakilisha vizuri.

Mwisho nawashauri wale ambao tayari wako UN, wawasaidia wengine kuwapa taarifa pindipo kunapokuwa na nafasi. Hivi karibuni UN itaajiri wafanyakazi zaidi ya Elfu nne kwa ajili ya kussupport jeshi la kulinda amani huko Darfur, ni matarajio yangu kwamba watanzania pia watakuwa wengi ktk nafasi hizo.
 
saharavoice,

Ni kweli kabisa unayosema

suala jingine linalotuangusha ni...........ni kuwa we are not risk takers, my own experience nimeshawahi kuwafanyia interview watanzania wawili kwenda mahala fulani.............wakanitolea nje................pamoja na kuwasiliana nao kwa pembeni ili kuwashawishi lakini wapi, jamaa mmoja mkenya na mwingine msudan, nilipowa-interview wakakubali na sasa hivi nawasiliana nao walishahamishwa kupelekwa sehemu nyingine...............hawa baadaye huja pata ajira ya kudumu UN kirahisi
 
Ogah,
Wengi wa watanzania wamezoea ajira za kudumu, Tanzania ni sehemu chache sana kuna contract za fixed term. sasa ukimwambia mtu aache aliko halafu asaini mkataba wa miezi mitatu, inakuwa ngumu kweli kweli. kuna mmoja alikataa kwenda Sierra Leone eti kwa sababu mandate ya ile mahakama inaisha 2009.

Kuna haja ya kuelimishana kuhusu mikataba ya UN na kuwatoa wasiwasa wenzetu kwamba, ukiingia UN umeingia, labda perfomance yako iwe mbovu.
 
Ogah,

E bwana mimi hutamani kupata hizo UN mission jobs...kama ipo namna ya kupata, mkuu saidia.
 
Nadhani kuna haja ya kutafuta sababu ni kwa nini kuna watanzania wachache sana kwenye AU na UN. Najua kuwa sababu moja ni umaimuna, na wasio maimuna wanajua lugha moja tu, any other reasons?

ni kweli sababu kubwa kabisa ni umaimuna na uoga wa watanzania kufatilia mambo
 
rose si uapply sasa dada yangu. kuzitamani tu haitoshi apply with confidence
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom