Johnny Sack
JF-Expert Member
- Jan 21, 2017
- 8,820
- 18,812
Waafrika tunahitaji kuthamini uhai na utu wetu Kati yetu na ndipo tutapata heshima, tukifanyiana unyama tunaonekana Kama wanyama na hata wengine hawataona tabu kutuua Kama wanyama.
Baada ya biashara ya Utumwa kukomeshwa miaka ya 1860 baadhi ya weusi waliokuwa watumwa waliorudishwa Africa na kukabidhiwa nchi ya Liberia, wazungu waliwasaidia kama kuwapa mikopo na miundombinu nyingine ya kujenga nchi ya kisasa ya kwao wenyewe
Hawakutaka hata kujiita Waafrika maana waliona kama ingekuwa matusi kwao, walijiita Americo- Liberians kujitofautisha na wenyeji waliowakuta.
Waliwakuta Waafrika wengine ambao walikuwa wakiishi porini, hawajui Kiingereza wala hawana ustaarabu kama wa kwao walioutoa huko Uzunguni.
Sasa nao wakawa wanajiona ni wazungu weusi, wakawa wanashirikiana na wakoloni wa Kifaransa na Waingereza kipindi kile nao wakawa wakoloni, wakawa ndio nao wanaitawala Africa. Wakawa wanawakandamiza na kuwabagua waliowakuta kama wazungu walivyokuwa wakiwafanyia.
Waliwafanyia kazi za sulubu bila malipo, wakawapiga marufuku kujichanganya nao, yaani ilikuwa marufuku Mwafrika aliyekuwepo kujichanganya maeneo anayoishi Mwafrika (mtumwa) aliyetoka Marekani.
Na hata kuoa ilikuwa marufuku Mwafrika kumuoa mtumwa mwanamke aliyetoka Marekani au mtoto wake.
Pia kwa kuwa biashara ya Utumwa haikukoma mara moja, ilikuwa ikiendelea kufanyika kwa kificho na Wareno na Wahispaniola kuchukuwa watumwa kuwapeleka Huko Brazil na visiwa vingine vya Carribean.
Sasa, hawa Waafrika waliokuwa wameonja Utumwa chini ya mzungu ukoje waliwakamata kwa nguvu Waafrika waliowakuta na kuwauza Watumwa kwenye biashara ilivyokuwa ikiendelea kinyemela.
Hayo ni kwa kifupi tu ya ubaguzi wao ambao upo hadi leo, kwa waliowahi kuishi Marekani watakuwa shahidi kuwa African-American ni wabaguzi na wanaotweza Waafrika kuliko hata Wazungu.
Wana elimu duni kuhusu Africa kuliko hata mzungu ambaye Africa sio asili yake, kuna tetesi kuwa Mohammed Ali alipoenda kupigana pambano lake la ngumi Zaire mwaka 1974 aliikejeli Africa na kusema ni afadhali hata babu yake aliuzwa mtumwa kipindi kile na yeye akawa Mmarekani.