Africa was not ready for 2010 world cup

ELNIN0

JF-Expert Member
Nov 26, 2009
4,161
1,460
JF,

Nathubutu kusema kwamba Africa hatukuwa tayari kwa mashindano haya. tumepeleka timu 6 na jana kabla ya game za mwisho nilisema africa haitapitisha timu hata moja kwenye last 16 na hii itakuwa aibu kubwa kwa bara letu.

Wenzetu wanatuzidi katika maandalizi kwa ujumla wake. nidhamu, umakini na ufundi wametuzidi mbali mno. Kila timu ya africa tuliyopeleka ina mapungufu yake na wote macho yetu ni dro kwa ghana dhidi ya Ujerumani, kitu ambacho ni sawa na panya kuamua pambano dhidi ya paka.

Hata kama Ghana itapita last 16 lakini ukweli utabakia palepale kwamba waafrica kwa ujumla hatukujiandaa kwa mashindano haya ambayo kwa mara ya kwanza yamefanyika katika ardhi yetu.

Mkihitaji data za udhaifu wa kiufundi katika kila timu nitawafafanulia.
 
Schoolmate nikwambie kitu?

Africa is not ready for this century world cup!!!
 
katika soka kuna kufunga...kufungwa...na kutoka sare...na asiyekubali kushindwa si..............malizia
 
Naomba huzo data za udhaifu wa kila timu. Kumbuka kuenyesha pia strength ya timu zingine ambayo timu za afrka hazina
 
sielewi kwa nini iwe kosa la timu zote za Afrika! faida ya fainali hizi kufanywa afrika kusini ni kwa waafrika kusini tu.

Nafikiri tungelaumu kuwa afrika kusini imekuwa mwenyeji wa kwanza kutolewa kwenye first round matches lakini tusilaumu timu nyengine za Afrika. They didnt ask for Afrika Kusini ku host, they dont gain a thing kwa Afriak Kusini ku host kombe hilo.
Ni sawa na kutarajia Italy i host kombe kisha tulalamike Malta (for example) haijaingia raundi ya pili.

Tusigeuke wazungu tukajibebesha makosa ya Waafrika wote kwa kile wanachojidai kuwa wao hawajui hasa kuwa afrika ni bara na sio nchi moja.
Uovu wa Wasomali ni wao wenyewe, na ujuha wa watanzania ni wetu wenyewe, haubebi Mkenya.

Ukisema Afrika Kusini haikuwa tayari kuandaa mashindano haya nitakubali tena sana.
 
Naomba nipingane na wewe mkuu.

What was your expectations? winning a world cup trophy?
While I totally agree with you that there are weaknesses on preparation side for the most of the African teams, personally looking back to history and facts I did not expected an African team to reach last two (final).

1. Its pity no an African coach into this finals
2. We realy saw individual players from Africa but not "teams"
3. Even in refereing (we are still poor)
4. Tactically poor

What we saw in this world cup from African teams can be cascaded down to our poor successes in economy, politics, life, planning, self reliance (name it). At least we have achieved to show the world that Africa is no longer a DARK continent. I must say South Africa have put this continent into another shadow from the WEST perceptions.

Nkosi Sikeleli Africa
 
ni kweli kabisa ulichosema,si mpira tu hata mambo yetu binafsi hatuwezi kuyafanya kama watu wa mabara mengine!
Tunashindwa kusimamia hata rasili mali tulizonazo ili tupate faida na tuendelee ki uchumi! madini yetu wanafaidi, hata ardhi yetu pia achilia mbali nafasi za biashara!
WAAFRIKA MPAKA LINI TUBADILIKE?
inasikitisha sana
 
Gaijin:

Kumbuka "mtoto wa mwenzio ni mwanao", pia timu ya kutoka Afrika hata kama si nchi yako bado ni timu ya waafrika wote.
Hili halipingiki. Remember Africa we have a different culture when it comes to familiy ties etc.

Tusifikiri kizungu na kuamua mambo ya waafrika.
 
Inawezekana Africans tulijiandaa ila hatukuwa serious katika mashindano haya makubwa.
Au Tulijiandaa ila hatukujua tunachokifanya.
Au pia tulijiandaa lakini wachezaji wetu waliamua kutuhujumu.
 
Africa has never been ready, is not ready and if circumstances continue as they are, IT WILL NEVER BE READY!
 
katika soka kuna kufunga...kufungwa...na kutoka sare...na asiyekubali kushindwa si..............malizia

Uu ushindani wa kila siku kufungwa sisi haiwezekani. Vile vile nafikiri timu za Africa zipunguzwe mpaka mbili ili kuwe na mchuano kabla ya qualification. Atleast tutapata washindani.
 
si umeona ufaransa waafrika weeeeeengi! wamefika wapi? waafrika tunamaskhara na hatuna bahati! hata wangejiaandaa miaka kumi mambo yangekuwa yaleyale; watu wanafika golini "clear chance" mtu anakosa goli tena sio mara moja mara mbili.

wasisingizie kitu; wa-SA wamewapa support ya haja na kutosha lakini mmmh! AIBU.
 
Schoolmate nikwambie kitu?

Africa is not ready for this century world cup!!!

Schoolmates duh umeniua kusema century hii yote hatuko tayari kwa mashindano ya kidunia. lakini mate vipi kuhusu nigeria? naona mpira mzuri sana ni nidhamu tu ndiyo imewaangusha. je nao tuwaweke katika kundi hili?
 
Back
Top Bottom