Afrika wanaosema tupo nyuma yako, ukigeuka unaweza usiwaone: Tujifunze Siasa za Samuel Doe wa Liberia

GUSSIE

JF-Expert Member
Dec 2, 2014
3,866
11,099
Liberia ni Taifa lililoundwa na watumwa weusi kutoka Marekani, Waliporudi liberia walikuta wenyeji walianzisha Taifa lao ,Bendera ya liberia inafanana sana na ya Marekani

Samuel Doe yeye aliingia madarakani kwa kufanya mapinduzi kwa Raisi aliyekuwepo akiwaahidi wananchi nchi itakuwa ya asali na maziwa, Raia walimshangilia sana wakiona tangu nchi kupata uhuru wake Sasa wamepata Mzalendo Rais Samuel Doe

Samuel Doe alipoingia tu madarakani kitu cha kwanza akaanza kupambana na mawaziri wa awamu iliyomtangulia, Akawakusanya mawaziri wote akawapeleka Ufukweni yaani Beach, Akawavua Nguo zote Kila mmoja akamuegesha kwenye mti wake akawapiga risasi wote huku Raia wakishuhudia na kushangilia

Katika mauaji hayo ya mawaziri, Waziri aliyepona ni Ellen Johnson aliyekuwa waziri wa fedha kwa wakati huo, Ellen ingawa alipona lakini alipata taabu sana

Samuel Doe Kama kawaida ya watawala wa kuahidi nchi ya maziwa na asali Muda wote alikuwa akichungulia hazina au chungu cha fedha hivyo kuilazimisha Ellen Johnson alipoti Kila Siku Ikulu Kupanga matumizi ya Doe

Samuel Doe aliamua kupendelea kabila lake kwenye uongozi haijalishi Mtu wa kabila lake amesoma au La, Doe na watu wa kabila lake walikula bata na kudharau mamilioni ya waliberia

Kuna muda Samuel Doe alianza kukufuru kwa mauaji aliyokuwa akiyafanya kwa Kila Mtu aliyehisi ni mpinzani wake alifika muda akatamka " Mungu hawezi Kumpa Mtu kazi asiyoiweza "akimaanisha mauaji anayoyafanya ni halali kabisa

Nyuma ya Samuel Doe walikuwepo watu waliokuwa wanamwambia tupo nyuma yako mmoja wapo ni Prince Johnson aliyekuja kumsaliti baadae

Mambo ya Samuel Doe ni mengi, Lakini nahitimisha kwa mwisho wake ulikuwaje :

Baada ya kugoma ushauri toka kwa Rais Ellen Johnson ambaye wakati huo alikuwa waziri wa fedha uchumi Wa liberia uliyumba sana maisha yakaanza kuwa magumu, Ellen akiamua kukimbilia World Bank alikokuwa anafanya kazi awali na kuendelea na maisha yake

Prince Johnson Rafiki mkubwa wa Joe aliingia msituni na kuja kupindua nchi alichomfanyia Doe ili atoe pesa alikoficha alifanya yafuatayo

1.Alimkata Doe masikio yote mawili lakini Doe hakutoa pesa

2.Alimchuna ngozi ya uume Doe hakutoa pesa

3.Alimkata vidole vyote Doe hakuonyesha pesa

4.Akamkata uume Doe hakuonyesha pesa

5.Alimburuza mtaani mpaka akafariki

Leo hii Prince Johnson ameokoka na anatangaza injili

Ellen Johnson ni Rais mstaafu aliyekabidhi madaraka kwa George weah

Kuna mengi ya kujifunza kwa hawa watu wanaokusifu na kusema tupo Nyuma yako wengi ni wanafiki na waongo kuanzia maaskofu, mawaziri mpaka wachungaji na mashehe, Siku Ukigeuka unaweza usiwaone
 
Unanikumbusha hili tukio la Maaskofu wa ULIPO TUPO!

7b7b1016c9c0894f6a22ecf69e5a4a4b.jpg
 
Kwani kwenye huu uzi nani katishiwa?
Unajuaje kama S.Doe aliamua kuishi hivyo na alikuwa tayari kwa matokeo ya jinsi alivyoamua kuishi maisha yake? Maisha siyo rahisi hivyo kama unavyofikiri na Binadamu hatuumbwi sawa, unafikiri ni kwa nini kitaa wezi huchomwa moto wakishikwa lkn bado huiba? Tena wengine hunusurika kuchomwa moto tayari alishavikwa tairi shingoni lkn huendelea kuiba, unafikiri ni kwa nini?

Acheni vitisho vya kitoto, fanyeni kazi msaidie familia zenu zinazowahitaji Tundu Lisu, Mbowe &Co. wako vizuri wao na familia zao ni mamilionea, Tundu Lisu mwakani atalipwa zaidi ya milioni 200 na Serikali achilia mbali milioni 10 kila mwezi kama mshahara na mshahara mwingine kama Kiongozi wa chadema, hivyo hata akifa leo hii Familia yake ataiacha vizuri wewe utaiachaje Familia yako kama ukifa au unafikiri Tundu Lisu atakuja kuilisha? Acha kupoteza muda wako hapa kumpigania mtu siajabu asiyekujua wala kukufahamu, fanya kazi!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata Mzee Nyerere angepinduliwa katika majaribio nane aliyokwepa maadui zake Pia wangemtungia uongo mwingi

Ni Kama vile Hitler, katika Second World War ingetokea Geman ingeshinda vile vita ingegeuzwa story Na makatili wangekuwa kina Winston Churchill Na Roosevelt

Ukishinda vita unakuwa Kwenye position nzuri ya kumsilibia Adui yako

Mapinduzi ya Znz yanaitwa matukufu kwa Kuwa yalifanikiwa Na Kama yangeshindwa kina Abeid Karume tungewaita Manduli
 
Viongozi wa dini ni kama vile wanakejeliwa na huu uzi. Lakini tukumbuke kuwa nchi nyingi za kiafrika zinakwama kwa sababu ya kutomheshimu Mungu.

Hii nchi ilikabidhiwa kwa Mungu siku moja kabla ya uhuru. Huwa inakumbwa na mambo ya hatari kama yaliyotokea kule Kibiti lakini huwa yanapita.

Sasa isiwe ni kwa sababu tunakula, tunashiba, tukitaka kwenda kutembea baharini tunakwenda, basi ndio tukaanza kuwakejeli viongozi wa dini. Uwepo wa nguvu ya Mungu ni mkubwa sana nchini mwetu.

Tusijenge mazingira ya kuwakejeli viongozi wa dini, hawa ni watu ambao mara
nyingi tu wanakesha wakiwa wamepiga magoti wakati mwingine wanafunga ili Tanzania ibakie kama ilivyo.
 
Unajuaje kama S.Doe aliamua kuishi hivyo na alikuwa tayari kwa matokeo ya jinsi alivyoamua kuishi maisha yake? Maisha siyo rahisi hivyo kama unavyofikiri na Binadamu hatuumbwi sawa, unafikiri ni kwa nini kitaa wezi huchomwa moto wakishikwa lkn bado huiba? Tena wengine hunusurika kuchomwa moto tayari alishavikwa tairi shingoni lkn huendelea kuiba, unafikiri ni kwa nini?

Acheni vitisho vya kitoto, fanyeni kazi msaidie familia zenu zinazowahitaji Tundu Lisu, Mbowe &Co. wako vizuri wao na familia zao ni mamilionea, Tundu Lisu mwakani atalipwa zaidi ya milioni 200 na Serikali achilia mbali milioni 10 kila mwezi kama mshahara na mshahara mwingine kama Kiongozi wa chadema, hivyo hata akifa leo hii Familia yake ataiacha vizuri wewe utaiachaje Familia yako kama ukifa au unafikiri Tundu Lisu atakuja kuilisha? Acha kupoteza muda wako hapa kumpigania mtu siajabu asiyekujua wala kukufahamu, fanya kazi!
Hata Tido muhando kuna watu walikuwa Nyuma yake wakati anaingia mikataba kwa niaba ya Serikali

Hata Rugemarila na Seth kuna watu walikuwa Nyuma yao Leo wale watu wametoweka

Hata Leo hawa mabosi wa hazina yaani Treasury wanaidhinisha mambo kwa Sasa, kuna Siku watabaki wenyewe kisutu wakisomewa mashtaka wakati ujao

Hakuna kutishana, Hata wewe wanaokwambia tukana au tetea kuna Siku utabaki mwenyewe na itabidi ujitetee mwenyewe

Maisha ni safari lakini huwa mbaya pale umri umeshastaafu na huna nguvu unaanza kupelekwa kisutu kusomewa mashtaka mbele ya wajuu kuu zako ukiwa na mkongojo

Utawala wa kikatili Africa haukuanza Leo, Hata Familia Ya Doe na Prince Johnson ilikutanishwa na TB Joshua, Prince Johnson aliomba msamaha ingawa mtoto wa Doe alikasirika sana
 
Master Sergent Samuel Doe Cayon alitumia maarifa makubwa sana ya kupindua serikali ya Liberia akiwa askari wa cheo cha chini.
Yeye alitumwa na wakubwa zake kijeshi waliokuwa wamepanga mapinduzi lakini hawataki kuhusishwa na mapinduzi hadi mapinduzi yakamilike yaani kumuua raisi Tolbert.Walituma kikosi kidogo kikiongozwa na Master Sergent Samuel Doe kufanya kazi hiyo.
Baada ya Master Sergent Doe kumuua Raisi Tolbert ilimbidi awape taarifa makamanda hao one by one.
Ndipo Doe akagundua kuwa kama amefanikiwa kumuuwa raisi Tolbert ,kwanini asiwaue hao makamanda waoga,waliotaka kula bila kunawa nae kuwa raisi?
Na ndicho alichofanya alipobisha hodi ilikuwa mauti kwao.
Nakumbuka miaka ya mwanzo wa utawala wa Doe alivutia watu wengi na watu wakitamani cheo hicho na kujiita Master Sergent au Jina lake Samuel Doe Cayon.
 
Viongozi wa dini ni kama vile wanakejeliwa na huu uzi. Lakini tukumbuke kuwa nchi nyingi za kiafrika zinakwama kwa sababu ya kutomheshimu Mungu.

Hii nchi ilikabidhiwa kwa Mungu siku moja kabla ya uhuru. Huwa inakumbwa na mambo ya hatari kama yaliyotokea kule Kibiti lakini huwa yanapita.

Sasa isiwe ni kwa sababu tunakula, tunashiba, tukitaka kwenda kutembea baharini tunakwenda, basi ndio tukaanza kuwakejeli viongozi wa dini. Uwepo wa nguvu ya Mungu ni mkubwa sana nchini mwetu.

Tusijenge mazingira ya kuwakejeli viongozi wa dini, hawa ni watu ambao mara nyingi tu wanakesha wakiwa wamepiga magoti wakati mwingine wanafunga ili Tanzania ibakie kama ilivyo.

Vitendo vyao ndivyo husababisha kukejeliwa kwao, tumefundishwa kwenye hizi dini tulizoletewa tusifuate au kuabudu watu bali tufuate mafundisho na maandiko..
 
Back
Top Bottom