Afrika wanaosema tupo nyuma yako, ukigeuka unaweza usiwaone: Tujifunze Siasa za Samuel Doe wa Liberia

Viongozi wa dini ni kama vile wanakejeliwa na huu uzi. Lakini tukumbuke kuwa nchi nyingi za kiafrika zinakwama kwa sababu ya kutomheshimu Mungu.

Hii nchi ilikabidhiwa kwa Mungu siku moja kabla ya uhuru. Huwa inakumbwa na mambo ya hatari kama yaliyotokea kule Kibiti lakini huwa yanapita.

Sasa isiwe ni kwa sababu tunakula, tunashiba, tukitaka kwenda kutembea baharini tunakwenda, basi ndio tukaanza kuwakejeli viongozi wa dini. Uwepo wa nguvu ya Mungu ni mkubwa sana nchini mwetu.

Tusijenge mazingira ya kuwakejeli viongozi wa dini, hawa ni watu ambao mara nyingi tu wanakesha wakiwa wamepiga magoti wakati mwingine wanafunga ili Tanzania ibakie kama ilivyo.
Ni uzushi tu, unataka kusema bila wao Mungu hayupo nasi.
 
Liberia ni Taifa lililoundwa na watumwa weusi kutoka Marekani, Waliporudi liberia walikuta wenyeji walianzisha Taifa lao ,Bendera ya liberia inafanana sana na ya Marekani

Samuel Doe yeye aliingia madarakani kwa kufanya mapinduzi kwa Raisi aliyekuwepo akiwaahidi wananchi nchi itakuwa ya asali na maziwa, Raia walimshangilia sana wakiona tangu nchi kupata uhuru wake Sasa wamepata Mzalendo Rais Samuel Doe

Samuel Doe alipoingia tu madarakani kitu cha kwanza akaanza kupambana na mawaziri wa awamu iliyomtangulia, Akawakusanya mawaziri wote akawapeleka Ufukweni yaani Beach, Akawavua Nguo zote Kila mmoja akamuegesha kwenye mti wake akawapiga risasi wote huku Raia wakishuhudia na kushangilia

Katika mauaji hayo ya mawaziri, Waziri aliyepona ni Ellen Johnson aliyekuwa waziri wa fedha kwa wakati huo, Ellen ingawa alipona lakini alipata taabu sana

Samuel Doe Kama kawaida ya watawala wa kuahidi nchi ya maziwa na asali Muda wote alikuwa akichungulia hazina au chungu cha fedha hivyo kuilazimisha Ellen Johnson alipoti Kila Siku Ikulu Kupanga matumizi ya Doe

Samuel Doe aliamua kupendelea kabila lake kwenye uongozi haijalishi Mtu wa kabila lake amesoma au La, Doe na watu wa kabila lake walikula bata na kudharau mamilioni ya waliberia

Kuna muda Samuel Doe alianza kukufuru kwa mauaji aliyokuwa akiyafanya kwa Kila Mtu aliyehisi ni mpinzani wake alifika muda akatamka " Mungu hawezi Kumpa Mtu kazi asiyoiweza "akimaanisha mauaji anayoyafanya ni halali kabisa

Nyuma ya Samuel Doe walikuwepo watu waliokuwa wanamwambia tupo nyuma yako mmoja wapo ni Prince Johnson aliyekuja kumsaliti baadae

Mambo ya Samuel Doe ni mengi, Lakini nahitimisha kwa mwisho wake ulikuwaje :

Baada ya kugoma ushauri toka kwa Rais Ellen Johnson ambaye wakati huo alikuwa waziri wa fedha uchumi Wa liberia uliyumba sana maisha yakaanza kuwa magumu, Ellen akiamua kukimbilia World Bank alikokuwa anafanya kazi awali na kuendelea na maisha yake

Prince Johnson Rafiki mkubwa wa Joe aliingia msituni na kuja kupindua nchi alichomfanyia Doe ili atoe pesa alikoficha alifanya yafuatayo

1.Alimkata Doe masikio yote mawili lakini Doe hakutoa pesa

2.Alimchuna ngozi ya uume Doe hakutoa pesa

3.Alimkata vidole vyote Doe hakuonyesha pesa

4.Akamkata uume Doe hakuonyesha pesa

5.Alimburuza mtaani mpaka akafariki

Leo hii Prince Johnson ameokoka na anatangaza injili

Ellen Johnson ni Rais mstaafu aliyekabidhi madaraka kwa George weah

Kuna mengi ya kujifunza kwa hawa watu wanaokusifu na kusema tupo Nyuma yako wengi ni wanafiki na waongo kuanzia maaskofu, mawaziri mpaka wachungaji na mashehe, Siku Ukigeuka unaweza usiwaone
Unataka kusemaje? Hizi nyimbo na tungo zilikuwa zinapostiwa na wapinzani miaka hiyo. Vipi mtu wa chama lao imekuwaje kuja na tungo hizi?. Nini kin
mekupata?
 
Viongozi wa dini ni kama vile wanakejeliwa na huu uzi. Lakini tukumbuke kuwa nchi nyingi za kiafrika zinakwama kwa sababu ya kutomheshimu Mungu.

Hii nchi ilikabidhiwa kwa Mungu siku moja kabla ya uhuru. Huwa inakumbwa na mambo ya hatari kama yaliyotokea kule Kibiti lakini huwa yanapita.

Sasa isiwe ni kwa sababu tunakula, tunashiba, tukitaka kwenda kutembea baharini tunakwenda, basi ndio tukaanza kuwakejeli viongozi wa dini. Uwepo wa nguvu ya Mungu ni mkubwa sana nchini mwetu.

Tusijenge mazingira ya kuwakejeli viongozi wa dini, hawa ni watu ambao mara nyingi tu wanakesha wakiwa wamepiga magoti wakati mwingine wanafunga ili Tanzania ibakie kama ilivyo.
Nchi hii tuna Mungu na bado umaskini wa kutupwa hivi? Tu a Mungu kuliko China na Marekani??
Acha uchawa
 
M
Master Sergent Samuel Doe Cayon alitumia maarifa makubwa sana ya kupindua serikali ya Liberia akiwa askari wa cheo cha chini.
Yeye alitumwa na wakubwa zake kijeshi waliokuwa wamepanga mapinduzi lakini hawataki kuhusishwa na mapinduzi hadi mapinduzi yakamilike yaani kumuua raisi Tolbert.Walituma kikosi kidogo kikiongozwa na Master Sergent Samuel Doe kufanya kazi hiyo.
Baada ya Master Sergent Doe kumuua Raisi Tolbert ilimbidi awape taarifa makamanda hao one by one.
Ndipo Doe akagundua kuwa kama amefanikiwa kumuuwa raisi Tolbert ,kwanini asiwaue hao makamanda waoga,waliotaka kula bila kunawa nae kuwa raisi?
Na ndicho alichofanya alipobisha hodi ilikuwa mauti kwao.
Nakumbuka miaka ya mwanzo wa utawala wa Doe alivutia watu wengi na watu wakitamani cheo hicho na kujiita Master Sergent au Jina lake Samuel Doe Cayon.
Madikiteta woote wananza na nyimbo za kuvitia watu utadhani ni watu kumbe mashetani.
Dikiteta lazima awe na kundi linalomwezesha kuwa hivyo.
 
Nchi hii tuna Mungu na bado umaskini wa kutupwa hivi? Tu a Mungu kuliko China na Marekani??
Acha uchawa
Umaskini na utajiri hutafutwa kwa akili na ubunifu. Mungu yupo mkuu iwe unakubali au unakataa.

Uchawa ni neno na dhana iliyozaliwa miaka hii ya Samia, miaka ya nyuma hakukuwa na hasira za wasio wafuasi wa rais dhidi ya wale wanaounga mkono kinachofanywa na serikali.

Neno chawa chanzo chake ni hasira wanazokuwa nazo wale wafuasi wa marais waliotangulia. Wanaishi na donge linalowaumiza mioyo yao.
 
Mtajuana wenyewe bwana. Sisi tuko na Rais Tundu Lissu
 
nchi za Africa zilitakiwa angalau kuanza kupewa uhuru miaka ya 90's kwenda mbele akili zikiwa zimetengemaa.
kuna mmoja Africa ya kati anaitwa Jean Bokasa,mwingine Mobutu wa Zaire zote hizi ni takataka akuna viongozi hapo.
 
Mungu ni zaidi ya akili zetu za kibinadamu, ukiongea kwa jeuri unajiona kama una haki lakini kiroho Mungu ni zaidi ya chochote ukijuacho.
Kama ni hivyo basi wasijifanye wao ndio wamiliki wa Mungu, mpaka wanawakoromea wale wasio toa sadaka nono, eti ooh! Wewe tajiri hautaki kutoa sadaka hizo mali zinaweza kuporomoka wakati wowote! Lakn ukitoa sadaka nono hayo maneno hauwezi kuyasikia, je wao ndio wamiliki wa Mungu?
 
Back
Top Bottom