Africa na mambo yake/ Gambia..

Crocodiletooth

JF-Expert Member
Oct 28, 2012
18,611
20,936
KAZI SASA IMEANZA AFRICA
~~~~~~~

Mamlaka za Gambia zimetangaza kuizuia kutua nchini humo ndege ya Rais Ellen Sirleaf Johnson ambaye pia ni Mwenyekiti wa hivi sasa wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Magharibi mwa Afrika ECOWAS.

Rais wa Liberia alitarajiwa kuwasili nchini Gambia leo kwa ajili ya kufanya juhudi za kuikoa nchi hiyo isitumbukie katika mgogoro wa kisiasa baada ya Rais Yahya Jammeh kutangaza kuyapinga matokeo ya uchaguzi wa Rais ambapo mpinzani wake Adama Barrow aliibuka na ushindi.

Nabkeur Ndiaye, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Senegal ameliambia shirika la habari la Reuters kwamba, Rais wa Liberia ambaye ni Mwenyekiti wa hivi sasa wa Jumuiya ya ECOWAS alikuwa aelekee Gambia leo lakini ndege yake ilizuiwa kutua mjini Banjul.

Ripoti zaidi zinasema kwamba, Yahya Jammeh alitangaza kwamba, hatamruhusu mwenyekiti huyo wa Ecowas kutua nchini Gambia.

Hayo yanajiri katika hali ambayo, Rais Yahya Jammeh wa Gambia ametangaza kuwa hatambui matokeo ya uchaguzi wa Rais uliofanyika nchini humo Disemba Mosi.

Jammeh ametangaza msimamo huo ikiwa imepita karibu wiki moja tangu uchaguzi huo ufanyike na mgombea wa muungano wa upinzani kuibuka mshindi. Yahya Jammeh ametaka ufanyike uchaguzi mwingine mpya wa rais.
[HASHTAG]#THIS[/HASHTAG] AFRICA BANA.
;>>RECOLONISATION MATTERS.
 
Kama Jammeh atafanikiwa kwenye hii issue ya kukataa matokeo, hizo sijui ECOWAS, AU na unions zote zivunjwe tu. Hakuna haja ya Nchi kutaka kujichomoa ICC na kung'ang'ania kubaki AU.
Uko sahihu kabisa...tena utakuta hawa uliowataja wanakija kusuruhisha Kwa kumwacha mharifu madarakani....africa bado Sana hili Ni bala la giza ndio maana wote tunaoishi humu Ni weusi
 
nchi za Africa hatuna democracia kabisa, yani tunafata trend moja nchi moja ikikataa matokeo yani inasambaa Africa nzima, hapo Zanzibar, ilitolea kule Nigeria sema ilikuwa solved immediately , mi nafikiri hizi jumuiya licha ya kusimamia uchumi, biashara,muingiliano wa kijamii, lazima tuwe na sheria zinazosimamia democracy na kuwaadhibu maraisi wanaochkulia democracy kama kawaida, hizi ECOWAS, EAC, SADC, hazina maana kama.mambo kama.haya yanafanyika

NChi nyingi za Africa zinaanza kujitoa na mahakama.ya kiraia ICC, nahsi Gambia alianzisha na nchi nyingine zinafata, we unafkiria kwa nini zinajitoa katika mahakama hiyo ya ualifu????, na kwanni Gambia kama sikosea ameshajitoaa
 
Mi niuleze hizi moja zetu za EAC, ECOWAS, AU,SADEC hazina nguvu za kuzuia kuingozi kukaa madarakani ikiwa kakiuka katiba? Hadi twenda ulaya?
 
Mi niuleze hizi moja zetu za EAC, ECOWAS, AU,SADEC hazina nguvu za kuzuia kuingozi kukaa madarakani ikiwa kakiuka katiba? Hadi twenda ulaya?

Hizo taasisi walianzisha wao wenyewe ndio maana waliziweka zikiwa Hazina neno ili zisije kuwatafuna siku mmoja wakiamua Mwenda kijecha jecha
 
Politics ( Everyone promises Paradise......)


0b6c21557eaf0b581b3c36a2c3bede10.jpg
 
Si tuliiona Video anampigia simu na kumpongeza? sasa imekuwaje tena!
Eti anadai kaghairi

Kwa mazingira yanayoendelea Gambia ambapo uchaguzi ulimalizika salama na Rais aliyekuwepo madarakani kufikia hatua hadi ya kumpigia simu mgombea wa upinzani na kumpongeza kwa ushindi.....

Halafu baada ya wiki anaghairi........

Nadhani sababu ya huyo jamaa kuamua kupiga U turn itakuwa ni kauli ya huyo mgombea aliyeshinda kuahidi kuwa atairejesha nchi hiyo kwenye mahakama ya Kimataifa ya ICC.

Tukumbuke kuwa wakati wa enzi ya utawala wa huyo Rais aliyepita ni kuwa alishaamua kuitoa nchi hiyo huko ICC.

Kitendo cha kiongozi mpya kutangaza kurejea ICC, keshagundua kuwa makazi yake mapya yatakuwa gerezani.......
 
Jammeh yupo sahihi,alifanya ustaarabu sana kukubali kushindwa na ata kumpigia simu aliyemshinda,Adama Barrow, na kumpongeza.Huo ni ustaarabu uliopitiliza.

Tatizo kalianzisha mwenyewe mgombea aliyeshinda kuanza vitisho vya kumuweka jela Yahya Jammeh, katika mazingira hayo mlitaka Jammeh akae kama kondoo asubiri kwenda kufungwa?

Busara ni jambo muhimu sana na bahati mbaya Adama Barrow alikosa busara hiyo, huwezi kumtishia mtu anayejiandaa kukuachia madaraka wakati bado yupo mamlakani.Ameyataka mwenyewe.

Namuunga mkono Yahya Jammeh kwenye hili.
 
Huyo jamaa wa ajabu sana alishakubali kushindwa sasa sijui kala maharage ya wapi usije kuta amewasiliana na Jach cheini wa Zangibai
 
Uchaguzi ujaoo Mm nitakuwa na kazi kuu ya kuhamasisha watu wasiende kupiga Kuraa Hata awe no Nani amegombeaa...
 
Nilishangaa sana kusikia yahya jamee eti amekubali kushindwa! Africa? Helou maza! Hahahaaaaa trump anasema twahitaji kutawaliwa mala ya pili
 
Back
Top Bottom