Africa Magharibi(ECOWAS) wana jeshi lao na vipi huku Mashariki(EAC)?

bryan2

JF-Expert Member
Jun 8, 2016
3,321
4,671
Tumesikia Jeshi la Shirikisho la nchi za Magharibi mwa Afrika(ECOWAS) wakijiandaa kuingia Gambia endapo ndugu Jammeh atakataa kukabidhi madaraka kwa Adama Barrow hapo 19 January.

Na vipi kwa nchi wanachama wa Afrika Mashariki(EAC) ikitokea kiongozi mmojawapo kung'ang'ania madaraka endapo mpinzani wake kashinda kwa haki kwenye uchaguzi?

______________
 
Aking'ang'ania madaraka watampongeza tu kwa sababu huku EA sio jambo geni hilo mfano mzuri ni huko Kwa Nkurunzinza na visiwani....

Kuhusu jeshi la pamoja sidhani kama lipo maana hata Idi Amini alivyopigwa alienda Tanzania peke yake na hii kwa sababu alikuwa anaingilia mipaka ya Tanzania.

Huko kwa Mjomba K sijui mambo yapoje maana tangu tupo primary mpaka leo yeye ndiye raisi wa nchi yake nadhani yeye na Mugabe hawana tofauti kabisa.
 
kwani ni lazima EAC nayo iige yanayofanywa na hizo taasisi zingine kila jumuiya zina malengo yake ambayo yanaweza yakatofautiana.
 
Tumesikia Jeshi la Shirikisho la nchi za Magharibi mwa Afrika(ECOWAS) wakijiandaa kuingia Gambia endapo ndugu Jammeh atakataa kukabidhi madaraka kwa Adama Barrow hapo 19 January.

Na vipi kwa nchi wanachama wa Afrika Mashariki(EAC) ikitokea kiongozi mmojawapo kung'ang'ania madaraka endapo mpinzani wake kashinda kwa haki kwenye uchaguzi?

______________
hili jesho lipo miaka mingi tu, nasikia jamaa keshazuia na redio na tv za binafsi hakuna kutangaza chochote, nimeona kwa nyuzi leo
 
Kifupi huwa ni jeshi la nchi mojawapo lakini hutumika kwa kivuli au baraka za ECOWAS.
Kwa mfano, Senegal inaweza kuingia Gambia kwa njia hiyo kama Jammeh hatasoma alama za nyakati!
 
kwani ni lazima EAC nayo iige yanayofanywa na hizo taasisi zingine kila jumuiya zina malengo yake ambayo yanaweza yakatofautiana.
Nato wanajeshi lao,UN wanajeshi Au wanajeshi lao ila sijapata kusikia EAC wakiwa na Chombo hicho
 
Back
Top Bottom